Mwanamaigizo steve nyerere amefunguka na kusema kuwa bila jitihada za msanii Khaleed maarufu kama TID , hakuna msanii angeweza kwenda kufanya kazi ulaya au nje ya nchi kwa sababu TID ndio msanii aliyefungua milango kwa wasanii wengine kwenda kufanya matamasha nje ya bongo.
Steve Nyerere na TID walikuwa na tofauti kidogo kwa zaidi ya mwaka lakini alipokuwa akiongea na EATV katika kipindi vha FNL steve nyerere amethibitisha kwamba kwa sasa wameamua kumaliza tofauti zao na kwamba wako vizuri hakuna ugomvi wala tofauti zozote.
TID ni msanii mkubwa wa kimataifa ambae aalifungua njia kwa wasanii kufanya kazi nje ya nchi, bila TID hakuna msanii angejua kuna nje , TID ni kitengo cha burudani kinachofanya kazi za utalii kimataifa.TID ni msanii mwin gine kabisa anapaswa kupewa Dibaji, ameweza kuipeperusha bendera ya Taifa.
Steve Nyerere anasema kuwa yeye na TID ni kama ndugu wa baba mmoja kwanini wagombane na ndio maana waliamua kupata na kumaliza tofauti zao. kama inakumbukwa mwaka huu Steve alimtuhumu TID kuwa aliongwa milioni 2 kwa ajili ya kutohamaisha maandamano yaliyokuwa yanatangazwa sana katika mitandao ya kijamii.