Taiya Haoni Shida Kufananishwa na Thea,

Baadhi ya mashabiki wa filamu na maigizo nchini Tanzania wamekuwa wakimfananisha mwigizaji Taiya Odero na Thea kuwa wanafanana kwa muonekano na jinsi wanavyoigiza katika filamu mbalimbali.

Akiongea na Clouds Radio Taiya anasema kuwa kwake yeye sio mbaya pale wanapomfananisha na msanii mkubwa na mkongwe kama Thea kwa sababu kwanza katika wasani aliokuwa akipenda kuwaangalia kipindi anaingia katika tasnia alikuwepo thea pia hiyo kwake anajivunia.

Watu wengi wamekuwa wakinifananisha na thae kutokana na ninavyoigiza japo mimi nafanya kama mimi lakini kunifananisha na mwigizaji mkubwa kama thea sioni shida kwa sababu ni moja kati a wasanii niliokuwa nawaangalia sana  na kutamani kufanya nao kazi.–Alisema Taiya  ambae kwa sasa anacheza vizuri nafasi zake katika tamthiliya ya Kapuni.

Hata hivyo mwanadada thea alipowahi kuulizwa kuhusu kufanana na mwigizaji huyo  alisema kuwa haoni kama amefanana nae kwa sababu kila mtu ana utofauti wake.

Familia Yaingilia Kati Hali ya Afya ya Taiya

mwanadada anaefanya vizuri sasa hivi katika tamthiliya ya Kapuni inayoonyeshwa katika televisheni ya maisha magic bongo Taiya Odero amezidi kuwapa hofu wazazi na ndugu zake kwa sababu ya kupuputka kwa mwili wake ambao umekuwa ukiisha siki hadi siku bila kuwa na sababu yoyote.

Familia ya mrembo huyo imeanza kupata wasiwasi juu ya afya ya mtoto wao baada ya kumuona kila siku mwili unazidi kuisha na bila kuwa na sababu ya maana ya kupungua kwake.

Moja ya watu wa karibu wa mwanadada huyo ambae hakutaka kutajwa na sababu moja ama nyingie ameelezea kuwa  famila ya mrembo taiya imekuwa na wasiwasi sana juu yake na kutaka akapime ili waweze kujua kinachomsumbua lakini hata pale Taiya alipokataa na kusema hana matatizo yoyote familia yake wawalisema watalazimika kumpeleka wao wenyewe.

familia yake sasa ni kama wamepoteza amani kwa sababu yake yeye na afya yake,wanataka kumpeleka hospitali ilikujua afya yake ingawa  muda wote yeye mwenyewe amekuwa akisema yuko sawa na hana tatizo lolote la kiafya ila  amekuwa akipunguza kula vyakula vya kunenepesha tu.

Hata hivyo taiya mwenyewe alisikika akisema kuwa hana tatizo lolote la kiafya lakini kamandugu wanaomjali ni lazima watakuwa na wasiwasi kwa kiasi fulani.

sina tatioz kama ndugu ni lazima  waingiwe na hofu  na mimi niko kwenye  kuwaelewesha kuwa sina taizo lolote-Alisema Taiya.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.