Ni matatizo ya Kifamilia Yaliyoniachanisha na Aslay-Tessy

Mwanadada Tessy Chocolate amefunguka na kuelezea kwa nini ameachana na baba wa  mtoto wake aslya ambae ni msanii wa bongo fleva naefanya vizuri sana katika anga hizo.

Akiongea na moja ya waandishi wa habari kutoka Ayo Tv, Tessy anasema kuwa kuachana kwake na Aslay ni mambo ya kawaida tu ya kifamilia ambayo yanaweza kutokea kwa mtu yoyote katika ndoa .

Hatuko pamoja tena na hayo ni matatizo tu ya kifamilia  ambayo nadhani yanaweza kutokiea kwa kila mtu, au kila mtu anaweza kuyapitia ila ni ya kawaida tu ya kifamilia.

Hata hivyo Tessy alipoulizwa kwanini hakuwa wazi tangu hapo awali kuhusu kuvunjika  kwa mahusiano yao, alijibu kuwa amekuwa hapenzi sana maisha yake yakae katika mitandao ya kijamii.

Hakuna aliyewahi kunikataza kuongelea kuachana kwetu lakini ninasema tena sipendi mahusiano yangu yakae katika mitandao ya kijamii, kwa sababu hayo ni maisha yangu binafsi.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.