Ray Kigosi-Wema Anastahili Adhabu Ya Kufungiwa

Msanii mkongwe wa sanaa ya Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’  amefunguka na kuweka wazi kuwa msanii mwenzake Wema Sepetu anastahili kabisa adhabu aliyoipata ya kufungiwa kufanya filamu kwa miaka miwili.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Sammisago Tv, Ray ameweka wazi kuwa ni sawa tu kwa adhabu aliyoipata Wema kwani kitendo alichofanya hakikuwa kizuri kabisa hasa kama msanii ambaye ni kioo cha jamii;

Wema alistahili mkupewa adhabu ya kufungiwa unajua tatizo la Watanzania wanapenda tuambiane vitu vya kusifiana sifiana tu lakini tusiseme pale mtu anapokosea kwaiyo mimi nikiwa kama msanii mkongwe ambaye nimekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu nasema kabisa kuwa Wema alikosea sana sana kwa sababu ukiangalia Wema ni Brand kuna watu wengi wengi sana ambao wanamuangalia hao wanaomuangalia wafanye nini yeye ni kioo cha jamii  kimsingi kabisa amefanya kosa lakini tumeshamuona Wema akiomba msamaha mara nyingi sana imefika wakati sasa abadilike”.

Kila msanii wengi amekuwa na maoni yake juu ya sakata la Wema wapo ambao wamemchana laivu kuhusu kosa lake lakini wapo ambao wamemkingia kifua kama vile Wolper.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.