Aslay Afunguka Kumzimia Wema

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Totoa’, Aslay amesema kuwa anavutiwa na uigizaji wa mrembo Wema Sepetu katika filamu na kudai endapo siku ataamua kuingia katika uwanja wa uigizaji rasmi basi ni lazima atafanya naye kazi.

Aslay ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

Kauli hiyo imekuja baada ya mashabiki zake kumtaka aigize kwa madai wamemuona na uzoefu kupitia kazi za muziki ambazo huwa anaigiza kwa dakika chache juu ya jambo fulani.

“Endapo ntaigiza basi msanii wa kwanza kufanya naye kazi ni Gabo Zigamba kwa sababu ananivutia sana na kazi zake ila kwa upande wa kike natamani kucheza na Wema Sepetu, Irene Uwoya, Riyama na wengine wengi”, amesema Aslay.

Pamoja na hayo, Aslay ameendelea kwa kusema “sijawahi kufikiria kama ninaweza kuigiza ila huwa najaribu tu kidogo kidogo kuigiza tatizo kukaa mbele ya kamera ndio shida. Kiukweli navutiwa na movie ila kama mashabiki zangu wananiona najua kuigiza basi nashukuru sana na nitajaribu kufanya hivyo siku moja”.

Mbali na hilo, Aslay amesema katika vitu ambavyo huwa vinamchukiza zaidi ni kuona baadhi ya watu wakimzushia sifa mbaya kuwa anaringa jambo ambalo sio la kweli kwa upande wake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.