Ninachojua Mungu Anakupenda Sana :-Maneno ya Muna kwa Wema

Imekuwa ikizoeleka kwa sisi binadamu kuwa mwenzako  anapopatwa na jambo  basi inakuwa ndio njia ya kumkomesha na kufurahia mapito yake, lakini hii imekuwa tofauti kwa wema na muna ambao pamoja na kwamba wamekuwa hawaongea kwa muda sasa lakini inapoteokea mmoja wao anapatwa na tatizo basi mwingine anatokea na kumpa maneno ya faraja mwingine.

Baada ya siku iliyopita kusambaa kwa picha ikimuonyesha wema akiwa faragha na mtarajiwa mume wake, basi Muna alionekana kuguswa na maneno mengi yaliyosambaa katika mitandao ya kijamii hivyo kaumua kumfariji kwa maneno yenye nguvu.

Katika ukurasa wake wa instagram, Muna aliandika “Ninachojua Mungu anakupenda sana na mkae kijua kuwa Mungu anakipenda kila kiumbe chake,  hata akosee vipi jua kuwa Mungu akienda sana tena sanaa,ukishakua kuwa Mungu anapenda kila kiumbe chake basi kaa ukijua kuwa ipo siku Mungu atatenda kwako, ninamwamnini sana Mungu na ipo siku ataenda muujiza wa kukujibu.

Wema na Muna waliwahi kuwa marafiki wakubwa na hata kufanya kazi pamoja lakini baadae urafiki wao ulishindikana na kugombana sana na kurushiana maneno na matuzi sana lakini mwisho wa siku kila mmoja amekuwa mwenye busara kwa yale yanayomkuta mwenzake.

Sakata la Wema, Muna Nae Aingizwa Ndani.

Baada timu za wasanii mbalimbai wakijaribu kila mmoja kumtetea msanii wake , kuna tetesi zilizoibuka zikidai kuwa mwanadada Muna aliwahi kutaka kutoa ushaidi na uthibitisha kuwa mwanadada wema sepetu aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na boss wa efm na kwamba hata mpenzi wake alikuwa akijua hilo lakini aliamua kunyamaza kimya.

moja ya kurasa za udaku zilizotoa tetesi hizo zinasema kuwa muna alikkuwa akijua swala hilo lakini alikaa kimya kwa muda na hata alipoambiwa kuhusu swala la ushahid alisema anauwezo wa kutoa ushaidi kwa hilo.

Hata hivyo muna alikana tetesi hizo na kusema kuwa anaomba watu wasimuingize katika maswala ya kishetani kwa sababu kwa sasa yeye amejikita zaidi kumtumikia Mungu wake.

Ikumbukwe kuwa Muna na Wema waliwahi kuwa marafiki wakubwa sana na kufikia hatua ya kufanya kazi pamoja lakini walipokuja kugombana walijikuta wakitajiana siri nyingi walizowahi kuzijua kwa upande wa kila mtu, lakini pia ikumbukwe kuwa Majizo ana mahusiano na Lulu ambae pia ni rafiki wa Muna.

 

Wema Atia Neno Swala la Muna Mtandaoni.

Mwanadada Wema sepetu ambae hapo awalia likuwa rafiki wa mwanadada muna amefunguka na kutia neno katika ukurasa wake huku akimwita  Muna kuwa ni mnafiki na tabia mbaya ya kujifanya mcha Mungu wakati anaweza mpaka kumkana na kumtukana mama yake mzazi.

Wema anasema kuwa mara nyingi sana Muna alikuwa akimtumia patrick kama njia ya suluhisho ya matatizo yake na ndio maana hata sasa mtoto huyo amefariki na mungu ameazana kumuumbua kabisa.

Kwa mujibu wa Wema ni kwamba muna na mama yake wamekuwa hawapatnani siku nyingi lakini mara zote, muna alikuwa akipatana na mama yake kupitia mtoto wake partick ambae kwa sasa ni marehemu na walikuwa wakipatanishwa na mtoto huyo na ndio maana ndugu waliumizwa na sana na kuondoka kwa mtoto huyo, hivyo kwa mujibu wa Wema , ni kwamba Muna na mama yake ni maadui wakubwa.

Wema anasema ” moja moja yanaanza kufichuka kujitia mcha mungu wakati  nyuma ya pazia  hata mama yako mzazi una mtusi  na huna maelewano na kabisa,  na nilichosikia ni kwamba marehemu PAT ndio alikuwa kama suluhisho kila Muna alipogombana na mama yake na ndio maana hata ndugu walikuwa wakimpenda sana yule mtoto., hata Muna alikuwa akigombana na mama yake alikuwa akirudisha moyo nyuma kwa sababu ya mjukuuu wake  PAT ili  kuleta amelewano yao.

Ikumbukwe kuwa Muna na Wema waliwahi kuwa marafiki wakubwa sana hapo awali lakini walikuja na kugombana na hata kipindi cha msiba wema na mama yake walikuwa wakipinga uamuzi wa Muna na kumsapoti sana aliyekuwa akisemekana kuwa ni baba wa mtoto.

 

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.