Ugonjwa Wa Mama Yangu Unafelisha Muziki Wangu- Y Tony

Msanii wa Bongo fleva Y Tony aliyefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Wivu wangu’ amefunguka na kueleza ugonjwa anaoumwa mama yake mzazi ndio unamkwamisha kimuziki.

Msanii huyo ameifungukia Enews ya EATV na kueleza kuwa kitu kinachomsumbua Kwenye maisha yake na kumuangusha mpaka kushindwa kutoa nyimbo kwa wakati ni kuwa mama yake mzazi ni mgonjwa takribani miaka 13.

Mama yangu amekuwa anasumbuliwa na miguu kwa miaka kumi na tatu yaani hatembei yani yupo tu chini amekaa na hiyo ndio inakwamisha hatakati zangu za muziki kwani ni lazima nimuangalie mama yangu Kwanza maana yeye ndio kila kitu kwangu”.

Lakini pia Y Tony amekataa kata kata tetesi zinazodai kuwa ameonekana akimpeleka mama yake kwa waganga wa kienyeji na kudai yeye sio mshirikina na hata mama yake ameokoka na kuongeza kuwa wameshaenda Makanisa karibia yote ili mama yake akaombewe bila mafanikio.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.