Mashabiki Waingilia Kati Penzi la Diamond na Zari

Wakati Diamond mwenyewe akiwa amekaa kimya hataki kuongelea mahusiano yake na mzazi mwenzie tangu mwanamke huyo aliposema rasmi kuwa ameachana na Diamond na kisha kufanya  mahojiano katika chombo kikubwa cha habari Duniani, mashabiki wa pande zote mbili wameonekana kukerwa na kuhuzunishwa sana na kuachana kwa wawili hao huku wakijitahidi kutoa ushauri kwa pande zote mbili kwamba wanataka wawaone wakiwa pamoja.

Katika mitandao ya instagram imekuwa ni kama desturi kukuta kuwa karibia kila picha inayowekwa na zari au diamond ni lazima itaongelea mahusiano yao ya kimapenzi kutoka kwa mashabiki wao.Wapo wanaoongea maneno makali kuonyesha kuwa na hasira kwa kuvunjika kwa penzi hilo na pia wapo wanaoonekana kuwa na hisia za huzuni kwa wote wawili na watoto wao pia.

amuru tanzania

please  shemeji zarimond do not hesitate to say no with big no,learn to say no in a small letter.go back to your gentleman.

mrlv3462

u look so pretty ila unapendeza sana ukiwa na baba watoto wako mond.

sihakaadam

acha ujinga wewe rudi kwa mwenzako muelewane na muleee watoto wenu , mimi ninaamini kuwa wanaume unawajua vizuri tu…cha msingi piga moyo konde na urudi kwa mwenzio.musiwape maneno wapambe nuksi.

tiritendebe

mamy naomba umsamehe jamani

paulinafaustine

Zari maisha ni safari ndefu jamani,jaribu kutuliza akili yako na utafakari  hata wazazi wetu  walipitia mapito hayohayo  lakini walivumilia mpaka hapo walipofika , kwaio maisha ya ndoa yana misuko suko kwaio piga moyo konde.

Zari na Diamond waligombana na kufikia maamuzi aliyotamka zari baada ya kuchoka kupokea skendo za mzazi mwenzie kuwa na wanawake kila siku huku sababu kubwa iliyomuumiza zari ni ukaribu wa Wema sepetu na Diamond ulioanza hivi karibuni.

 

Yawezekana Haya Ndio Yaliyomtoa Zari kwa Diamond.

Ikiwa inakaribia wiki sasa tangu mwanamama Zarina Hassan  kuandika ujumbe mzito ulioibua hisia kali kwa mashabiki wa muziki wa bongo  baada ya kuandika rasmi kuwa anaachana na uhusiano wa kimapenzi alikuwa nao na mwanaume wake aliyezaa nae watoto wawili ambae pia ni msanii mkubwa na maarufu bongo na nje ya bongo Diamond Platinumz.

Pamoja na kwamba hakuna alichojibu mwanaume huyo baada ya kuachiwa kwa ujumbe huo na mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa instagram siku ya wapendanao lakini hisia za mashabiki zimekuwa kali juu ya  kuachana kwa wawili hao.Wapo walianza kuangalia kwa upande wa pili sababu ndogo ndogo ambazo zinawezekana zilikuwa zikimsumbua mwanamama huyo kwa muda mrefu , huku wachambuzi wa mapenzi wakisema kuwa katika mahusiano kitu chochote kidogo kinapokuwa kinajirudia rudia huweza kuwa kikwazo kikubwa.

Uwepo wa skendo nyingi za kuwa na wanawake, kila kukicha katika mitandao kumekuwa na sababu za kuchepuka kwa Diamond na wanawake tofauti tofauti ambapo kwa mwanamke wa kawaida anaweza kuchoka kusikiliza kila siku swala la mwanaume wake kuwa na wanawake wa aina tofauti tofauti tena wasioweza kulinganishwa nae kwa kitu chochote.

Ukaribu wa Wema Sepetu na Diamond uliozuka hivi karibuni,Diamond na Wema walikuwa mahasimu wakubwa baada ya kuachana na sababu moja wapo ya Dai kuachana na wema ni Zari,hivyo inampa Zari wakati mgumu kukubali tena kuoana wawili hao wapo karibu ilhali mwanamke huyo alishakuwa na  mapenzi na mume wake kabla.

Jambo lingine linalosemekana kuachana kwa wawili hao ni kukosekana kwa watu wa karibu hasa wakubwa ambao wangeweza kuwa na msaada katika kuwashauri swala zima la mahusiano , tena ukizingatia kuwa Zari hana wazazi wote wawili hivyo hakuwa na maamuzi ya busara kutoka kwa watu wakubwa wa kumshauri huku upande wa Diamond wazazi wake hasa mama amekuwa ni mtu wa  kukubali maamuzi ya mtoto wake.

Jambo lingine ni utajiri wa Zari,mwanamama huyo anahela kiasi kwamba anachotaka kutoka kwa Diamond ni mapezni ya kweli na sio cha zaidi, hivyo Zari anaonekana kuchoshwa na drama za kila siku kutoka kwa Diamond ilhali kwake alikuwa akitafuta upendo wa kweli na sio pesa kama wanawake wanaotembea na mzazi mwenzie wanavyotaka.

 

Kuachana Kwa Zari na Diamond ni Kiki.

Ikiwa bado mashabiki wakisubiri tamko kutoka kwa msanii mkubwa Diamond Platinuzm kuhusu kuachana na mama watoto wake (Zari the bossy)  ambae siku ya wapendanao alitoa tamko rasmi la kuachana na msanii huyo huko katika mitandao ya kijamii kumekuwa kunazuka kwa maneno madogo maneno kutoka kwa wawili hao yanayowafanya mashabiki waanze kuamini kuwa wili hao wamekuwa wakifanya hayo yote ilimkpata kiki ya kuuza album mpya ya Diamond ambayo inatoka hivi karibuni.

Wakionekana kujibishana kwa style ya tofauti , Diamond Platinuzm katika ukurasa wake wa instagram aliweka picha ya kpande cha video ya Maromboso na kuandika maneno yanayohusiana na kile alichokisema zari siku anatoa tamko ilo la kuachana kwao.Ambapo ua jesi ni picha ya ua ambalo Zari aliweka na kuandika caption ya kuachana na Diamond siku ya valentine.

“haya mashairi changanya na ua jesi….dah @Mbosso kama ulinitabiria mdogo wangu”

Katika snapchat ya Zari aliweka video ikionyesha anasikiliza wimbo wa Diamond unaokwenda kwa jina la sikomi na kuandika ‘”utakoma tu mwenzangu”

Hata hivyo baada ya kuvamiwa sana na mvua ya maneno kutoka kwa mashabiki zake, zarianaanza kuonekana kama anajirudi kwa kile anacokuwa akikiandika kuhusu Diamond.

Hata hivyo siku ya jana katika kurasa za wasanii kutoka WCB, kulienea kwa video ikionyesha  kuwa kuna ujio wa wimbo mpya wa Diamond huku ikisemekana kuwa ni wimbo mpya ambao Diamond amemuimbia Zari kama kumuomba msamaha kutokana na skendo za kuwa na wanawake wengi na kutengeeza kiki baaada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.