Kejeli Za Hamisa Zinavyozidi Kumnufaisha Zari, Ni Baada ya Kumwita Changudoa

Bado mambo yamekuwa si mazuri kwa maadui wawili yaani Hamisa Mobeto na Zari kutokana na wivu walionao baada ya kila mmoja kutaka kuvutia penzi la msanii mkubwa Diamond Platinumz  upande wake ingawa inaonekana kuwa mwanaume mwenyewe yuko sana upande wa Zari.

Kumekuwa na kelele nyingi na matusi  baina ya watu hawa wawili tena kufikia hatua ya kuingia hadi watu wa karibu katika  familia zao,hivi karibuni hamisa alipost katika mtandao wake wa snapchat na kumwita zari changudoa mzee jambo ambalo pia liliibua maneno mengi kwa mashabiki wa pande zote mbili.

Sio hali ya kawaida kwa mtu kuitwa hivyo na bado akaweza kukubali jambo hilo , lakini hii imekuwa tofauti kwa Zari kwa sababu hata baada ya kuitwa hivyo alijibu na kukubali kuwa ni kweli yeyey ni changudoa mzee lakini uchangudoa alionao ndio umemfanya yeye kuwa pale alipo kama Bossy lakini uchangudoa wake ndio uliomfanya aweze kukaa na mwanaume ambae wanamgombania.

Katika ukurasa wake huu wa snapchat, Zari The Bossy alijibu tuhuma za kuitwa changudoa kwa kusema  Bora mimi changudoa mzee mwenye mafanikio na bado ananipenda sana kuliko wewe  kijana mwenye miaka 20, mama uliyeacha mara mbili na tuzo juu. 

Zari amekuwa akionyesha mali zake na mijengo yake aliyonayo katika nchi mbalimbali ikiwepo afrika ya kusini,na amekuwa akijinadi kuwa pamoja na kwamba mke mwenzake huyo amekuwa akimwita changudoa ni wazi kuwa yeye ni changudoa na amekuwa na mafanikio kwa sababu hiyo.

Katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakipokea maneno hayo kwa taswira tofauti na hata wengine kuwa wanamshauri sana Hamisa kuacha kugombana na Zari kwa sababu amekuwa akimzidi sana katika nyanja zote tena hasa swala zima la mali na utajiri.

Hii ni faida kwa zari kwa sabau kila anapovamiva kwa matusi na Hamisa amekuwa aikubali na kufanya kupata sapoti kubwa ya mahabiki kuwa yeye hataki kumlipiza vibaya Hamisa bali kukubali kila anachoambiwa.

 

Zari Amchezea Mchezo Mchafu Hamisa

Mwanamitindo na mjasiriamali hamisa mobeto amejikuta katika mtego mzito aliowekewa na adui yake mkubwa na mwanamke wanae-share nae mwanaume Zari The Bossy baada ya mwanamama huyo kuamua kumuwekea mtego uliomfanya Hamisa kuwa karibu na ndugu wa damu wa Zari The Bossy anaejulikana kama William Bugeme.

Kuna baadhi ya picha zilizokuwa zikisambaa ambazo zimekuwa zikimuonyesha Hamisa akiwa na mwanaume huyo ambae watu wanasema kuwa inawezekana huo ni mpango wa Zari The Bossy kumeweka karibu mwanadada Hamisa Mobeto ili aweze kupata mtu wa kum-keep busy ili asiweze kuwa karibu na mzazi mwenzie Diamond Platinumz.

Moja ya watu wa karibu na mwanamama Zari The Bosyy  amethibitisha ilo na kusema kuwa hamisa amekuwa mjinga na kushindwa kutambua kuwa nukaribu wake na Buggeme unaweza kuwa ni mtego mkubwa kutoka kwa zari ili ahakikishe kuwa hayupo karibu na mumewe.

mnajua kuwa huyo hamisa amenasa kwa begeme lakini hajui kuwa huo wote ni mpango wa zari katika  kumtoa kwa baba watotro wake,asipoangalia atajikuta anatumika na bado anabwaga  kwani huyo mwanaume yupo kimaslahi zaidi wala sio kwa mapenzi hata kidogo.

mwanamke huyo ni mjanja sana,haongei ila inaongea pesa tu,bugeme toka zamani anafahamiana na na hamisa sasa ameamua kumtumia huyo huyo ili ili kumaliza kamcgezo kake,unafikiri diamond akiona ameingia kwenye penzi na mwanaume mwingine lazima  amuache.

William Bugeme alishawahi kutoka na wasanii wengine wa bongo kama Linah Sanga pamoja na Kabula.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.