Swala la Kutopata Mtoto kwa Sasa, Jux Asema Vannesa Ndio Chanzo.

Msanii wa muziki bongo Juma Jux ambaye yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee, ameweka wazi sababu inayowafanya wachelewe kupata mtoto na mpenzi wake huyo, ambaye wako kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jux amesema yeye na Vanessa kupata mtoto ni jambo ambalo bado hawajalipanga, kutokana na kazi aliyonayo mpenzi wake Vanessa Mdee, akisema kwamba anahitaji muda wa kujiandaa zaidi ili hata akiwa kwenye wakati wa kulea, hakuna jambo ambalo litasimama kwenye kazi zake na kumuathiri.

download latest music    

Msichana anapopata mtoto kuna miezi 9 ya kubeba ujauzito, Vanesa ni mwanamuziki kuna vitu vingi anafanya, kuna deals fulani amesaini, sasa hawezi kuwaambia watu siwezi kufanya hivi kwa sababu nina ujauzito, haileti maana, kuna vitu ambavyo inabidi viende sawa, kwa msichana kukaa miezi 9 hafanyi kazi yoyote na hukutayarisha chochote kwa muda huo, inakuwa ngumu, ikiingia kwa bahati mbaya sawa lakini lazima umakini uwepo”, amesema Jux.

Wawili hao wana zaidi ya miaka minne kwenye mahusiano, lakini mpaka sasa hawajahalalisha mahusiano yao kuwa wanandoa au kupata mtoto, jambo ambalo linaibua minong’ono mingi kwa mashabik

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.