Bilnass :-‘Kutongoza Mwanamke , Its Too Old’
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Bilnass amefungua na kuweka wazi njia rahisi anayoitumia ili kuwapata wanawake anaoingia nao katika mahusiano siku zote huku akikataa swala la kutongoza ambalo kwake anaona kuwa ni kama njia ya kizamani.
Akiongea katika kipindi cha kikaangoni, Bilnass anasema kuwa mara nyingi amekuwa mtu wa kuanzisha mahusiano ya kirafiki na mwanamke anayetaka kuwa nae katika mahusiano huku hivyo kwa sababu nakuwa tayari alishatengeneza urafiki inakuwa sio kazi kubwa kuanzisha nae mapenzi.
Mahusiano yangu mengi hayaanziagi kwenye kufukuzana,thats too old, imakaa kizamani sana naanza kwa kuwa na urafiki na huyo mtu na unajua ukishakuwa na urafiki na mtu inakuwa rahisi sana ila ile kuanza kumfukuzia mtu sijawahi.
Bilnass amekiri kuwa katika mahusiano kwa sasa ingawa hajataka kuweka wazi aliyenae sasa hivi huku akikiri kuwa alishawahi kuwa katika mahusiano na msanii mwenzake Nandy.