Nilipokuwa na Mimba Nilikuwa Mdogo, Ukinichamba Nakuangalia:-Gigy Money
Mwanadada Gigy Money amefanya mahojiano kwa mara ya kwanza tangu alipojifungua ambapo hata siku 40 hazijapita lakini alipata bahati ya kuelezea hali aliyokuwa nayo kipindi yupo mjamzito na baadhi ya magumu aliyokuwa ameyapitia kipindi mjamzito.
Gigy Money anasema kuwa alipojigundua kuwa yeye ni mjazmito ilikuwa na muda wa wiki tatu lakini ilimuia vigumu kukubali kwa sababu alikuwa akiwafikiri mashabiki zake watamwambia nini, lakini pia alikuwa anaona kama mimba ingemfanya kufifia katika muziki kwa sababu kipindi hicho alikuwa ametoa hit song ya nampa papa ambayo ilikuwa ikifanya vizuri.
Gigy Money anaendelea kusimulia na kusema kuwa kikubwa alichofanya ni kwenda kwa mama yake ambae alimwambia kuwa kikubwa anachotakiwa kukiangalia ni kama yupo tayari kupata mtoto bila kujali baba wa mtoto ana nini au hana nini na ndipo alipoona kuwa hana haja ya kuitoa mimba kwa sababu hata ba bawa mtoto pia alikuwa akionyesha kuwa ana hamu ya kupata mtoto.
Kadri miezi ilivyosogea Gigy Money alianza kuumwa sana na kushindwa kula muda mwingi alikuwa ni mtu wa kunywa pombe tu na ndipo alipopata mawazo ya kuitoa mimba lakini alikuwa akisita kutokana na ukweli kuwa mwanaume mwenye mimba alikuwa akionyesha asana kumjali na kuwa nae karibu.
Gigy Money anasema kuwa katika vitu alivyokuwa navyo kipindi yupo mjamizto ni kuwa mpole sana, alikuwa mdogo kiasi kwamba hakuwanauwezo wa kujibishana na mtu yoyote, wengine waliokuwa wakimchamba alikuwa akiwaangalia tu.
Gigy money anamalizia kwa kusema kuwa maumivu ya uchungu wa kuzaa hayawezi kuelezeka zaidi ni kuombeana sana unapoona mwanamke yupo katika hali hiyo.
