Tunda Kanizidi Umri tu Sio Kazi:-Bob Junior
Msanii wa bongo fleva wa muda mrefu Bob Junior amefunguka na kumjibu tunda man kuwa aache kumdharau kwa sababu kati yake na yeye wanazidiana kwa umri tu na sio kazi kama ambavyo yeye amekuwa akimuita mdogo.
Bob Junior ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika kipindi cha EATV, cha eNews na kusema kuwa yeye ameanza musiki kwa muda mrefu sana ila wazazi wake walikuwa wakimkata kufanya muziki na kuwa ekuwa akmheshimu sana tunda man kwa sababu ni mkubwa kwake kiumri na wala sio kazi.
Tunda ni kaka yangu na ninamheshimu sana kwa sababu amenizidi umru sana tu, lakini katika kazi naomba tuheshimiana sana mimi so mtoto kama yeye anavyosema kuwa mimi ni mtoto ,mbona nimemfanyia baadhi ya nyimbo zake wakati anaanza na sijasema kitu sasa nani mdogo hapo kati yake na yangu.
