Diamond Kuja na Wasafi Festival
Msanii diamond platinumz ametangaza rasmi kuhusu kufanya festival kubwa mwaka huu itakayojulikana kama Wasafi Festival ikiwa ni moja ya ubunifu wake mkubwa katika biashara na kuwafurahisa mashabiki wake.
Hii ni moja ya jambo kubwa sana ambalo mashabiki wengi wa team hiyo walikuwa wakirisubiria kwa hamu kubwa givyo ujio huo umewaweka watu wengi katika hamsa ya kujua lini litafanyika swala hilo.
Katika ukurasa wake wa instagram, diamond aliandika “kama naiona wasafi festival mwaka huu itakavyokuwa , sijui hata tuanze mkoa gani “
Wasafi wamekuwa wakifanya baadhi ya matamasha ya pamoja na mshabiki ikiwa ni moja ya njia nzuri yakuwa na mshabiki wao , kama ilivyofanyika mwaka uliopita Wasafi beach party.
