Nilipotangaza Kuwa Bikra Nilitongozwa Sana;-Chemical
Msanii wa muziki wa hip -hop nchini, Chemical amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwashangaa sana wanaoshangaa wasichana wenye bikra hasa wanaoamua kusema ukweli kuhusu swala hilo wakati kwake ni jambo la kawaida kama ilivyo vitu vingine.
Chemical amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo katika kipindi cha kikaangono live cha EATV.
Kuna wasichana mpaka leo wanemda kuolewa wakiwa na bikra zao na wanafanya vizuri kabisa na ni wazuri tu,kwaio kuwa na bikra sio ushamba na kutokuwa na bikra ukubwani pia sio ushamba, inategemea tu umekulia wapi na mazingira uliyopitia hapo awali.
Hata hivyo chemical anasema kuwa alipotangaza katika vyombo vya habari kuwa yeye ni bikra alitongozwa sana na watu wa rika tofauti tofauti ingawa pia wapo waliomshangaa na kumuona mshamba.
mimi nilitongozwa sana niliposema mimi ni bikra , tena na wengi wakiwa watu wazima kabisa,na nikaona kumbe kuwa bikra ni dili sana.
