Jay Moe Asema Sababu ya Wasanii Kufeli ni Kiburi
Msanii mkongwe wa muziki Jay Moe anasema kuwa sababu kubwa ya wasanii kufeli ni kuwa na kiburi na kujiamini kupita kiasi na kufikia hatua ya kushindwa kuendelea kufanya kazi.jay moe anasema kuwa kwa upoande wake anaona kabisa mpaka sasa ameweza kudumu kwa sababu ya nidhamu na kuishi na watu vizuri na kuwa na usikivu pale anapokuwa akipewa ushauri.
katika kila kitu ili kidumu ni lazima kuwe na nidhamu,katika game yangu kulikuwa na wasanii wakubwa na maarufu waliokuwa zaidi yangu mimi,lakini labda nidhamu yao ndio iliwaangusha mpaka sasa.
ninachoshukuru mimi ni kwamba niko na mahusiano mazuri na watu ambao nafanya nao kazi kila siku kama media,mashabiki na watu mbalimbali katika industry,na nidhamu ndio kitu kikubwa kwa sababu unaweza kuwa na umaarufu sasa lakini baadae ukapata shindwa ukakosa wa kukupa msaada.
Lakini pia Jay Moe anasema kuwa wasanii wakongwe wamekuwa wakikataa mabadiliko kuwa muziki wa sasa na wazamani una utofauti mkubwa.