Gigy Money Atoa Ushauri kwa Wanaotembea na Waume za Watu.
mwanadada Gigy money amefunguka nakuongelea swala la wanawake wenzake kuwa uru kwa kutembea na wanaume wa watu bila kujali maumivu wanayoyapata wanawake wenzao na huku wao wakiwa wanajua kabisa kuwa mwanaume anayetembea nae ni mume wa mtu.
Gigy money anasema kuwa ukiwa na mwanaume anayelala kwako na kukujali wewe kila muda huku akiwa amacha mwanamke wake nyumbani basi huyo ujue ni shetani tena mnyama kabisa wala hana huruma.
Gigy money anasema kuwa usione mwanamke anakaa kwa mwanaume wake huku mwanaume huyo akiwa na wanwake wengine nje, swala ni kwamba unakuwa hujui ni kitu gani kimemfanya aendelee kukaa mule ndani bila kuondoka yeye au na watoto wake hivyo wanawake wanapaswa kuwa na huruma na wanawake wenzao.
Katika ukurasa wake wa instagram, Gigy money ameandika kwa kuonyesha uchungu wanaoupata wanawake wengine waliopo katika ndoa huku michepuko ikiona kutembea na wanaume za watu ni swala la kawaida tena lenye furaha kabisa.

