Wema Akanusha Kurudiana na Diamond.

Mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba wamekuwa karibu sana na Diamond kwa siku za hivi karibuni lakini haina maana kwamba wawili hao wamerudiana katika mahusiano ya kimapenzi kama zamani kama vile watu wanavyokaa na kusema katika mitandao ya kijamii.

Wema anayasema hayo alipokuwa akifanya interview na Times Fm akiwa na msanii mkubwa kutoka Nigeria Van Vicker ambae ametua Tanzania kwa ajili ya birthday gala ya Wema Sepetu pamoja nauzinduzi wa filamu yao liyoigizwa miaka ya hapo nyuma.

download latest music    

Wema anasema kuwa ukaribu wake na Diamond ni wa kikazi na urafiki tu na urafiki wao umekuwa zaidi ya urafiki kwa sababu ni watu waliowahi kuwa pamoja kwaio wanajuana lakini pia ukaribu huo unazidi kuunganishwa na urafiki alionao Wema na dada wa Diamond Esma pamoja na mama mzazi wa msanii huyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.