Mboso Awaonya Wanaomfananisha na Aslay

Msanii Mboso kutoka katika kundi la WCB  amefunguka na kuwaonya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfananisha na msanii mwenzake Aslay ambae  amkuwa akifanya muziki kwa kujitegemea tangu kuondoka kwa kundi lao la ya moto.

Mboso anasema kuwa hawezi kufafanishwa na Aslay kwa sababu Aslay alianza muziki kabla yake na kabla hata ya kuundwa kwa kundi walikuwa wakifanya kazi hivyo hawawezi kulingana katika hilo.

download latest music    

hakuna kitu ninachokiona alafu nikajisikia vibaya kama ninapoona ninafananishwa na Aslay, yuke mimi ni kaka yangu na isitoshe mimi nimeanza music kama solo artist nikiwa na miezi 9 tu lakini yeye kaanza muziki tangu mwaka 2011.Ukinifananisha nae unakuwa unamvunjia heshima yake.

Mboso , Aslay na wasani wengine wawili walikuwa wakifanya kazi katika kundi moja lakini baada ya kundi hilo kuvunjika kila mmoja alianza kuimba kama msanii wa kujitegemea huku Mboso akisajiriwa na WCB kuwa chini yao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.