Safari ya Hawa Nitarejea Nchini India Imeiva.

Siku chache zilizopita msanii Diamond Platinumz alitangaza kuwa ameingilia kati matibabu ya mwanadada hawa ambae aliimba nae katika wimbo wake wa Nitareejea wimbo uliofanya vizuri sana kipindi cha nyuma lakini mwanadada huyo alikuja kupotea ghafla.

Akiongea na waandishi wa habari, Mlezi wa hawa  (PILI MISANAH ) ana sema kuwa meneja wa Diamond anaejulikana kama Babu Tale amekuwa mfatiliaji wa  kina kuhusu safari hiyo  hasa upande wa visa  na kwamba imekaribia kupatikana hivyo uhakia wa safari kupatikana kwa safari ambayo ilitangazwa na Diamond mwenyewe.

download latest music    

hapa tunasubiri visa na ndio itatupa mwanga wa lini tuakwenda kwa sababu huwezi kwenda nchi za watu kama unakwenda kariakoo,wao pia wanataratibu zao kwa sababu inabidi wajue kama pia tunauwezo wa kulipia hayo matibabu.

nashukuru kwa sababu kipindi hiki ninamuguza mwanangu lakini pia babu tale amekuwa akinisaidia kufatilia maswala ya visa , hivyo ninaamini kuanzia kesho tunaweza kuwa tumeshapata visa  na uhakika wa safari.

Hawa ambae amekuwa na tatizo la kujaa maji tumboni amekuwa akipelekwa hospitali kila mara na kutolewa  maji hayo, lakini imesemwa kuwa ugonjwa wake unaweza kukoma endapo atapatiwa matibabu nchini India ambapo kuna waatalamu zaidi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.