Amber Lulu Asema Hataki Tena Kupoteza Muda kwa Sababu ya Mwanaume.
Tangu mwanadada Amber Lulu atangaze kuwa single hajataka kubadilisha msimamo wake kuwa hataki tena na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote kwa sababu anachoamini kuwa kwa muda wote aliwahi kuwa katika mahusiano kulikuwa kuna kupotezeana kwa wakati kati yake na wanaume wake.
Amber Lulu ambae alikuwa katika penzi zito na msani kutoka kenya prezoo walikua kuachana ghafla baada ya kusambaa kwa picha za mwanaume huyo akiwa na mwanamke mwingine, kitu kilichomuuma sana Amber Lulu, na kuamua kutangaza kuwa yuko single.
Amber Lulu ameuambia mtandao wa Pro24Djs kwamba amepotezewa sana muda na wanaume ambao hawana msimamo katika mapenzi.
“Kama kutoka kimapenzi na mtu ambaye hajui thamani yako, ndio kitu ambacho huwa nakifikiria kwasababu nimepoteza sana muda,” alisema Amber Lulu. “Huwaga hicho kitu kinaniumiza sana, muda ambao nilikuwa naupoteza na nguvu ambazo ningeziweka kwenye muziki wangu ningefika mbali sana,”
Aliongeza, “Ndio maana watu wanasema ni bora mtu akupende kuliko umpende, kwa sababu ukimpenda inakuwa ni shida. Vitu kama hivyo vimenipelekea kufanya vitu vya ajabu, unakuwa na watu ambae haujawataka, inakuwa kama ni hasira kwahiyo imenifanya nisitamani kumuona mwanaume yeyote katika macho yangu,”
