Baada ya Kupewa Tuzo,Shiloleh Atoa Shukuran kwa Aunty Ezekiel

Siku ya May 13 ilikuwa pia siku aalumu na muhimu kwa Shiloleh hasa baada ya kupokea tuzo kubwa ya kutambulika kwa machnago wake katika tasnia ya muziki na pia kama mwanamke mpambananji katika tasnia ya muziki na filamu pia lakini akiwa kama wanamke anaepambana kuhudumia jamii.

Aunty Ezekiel alimpa shiloleh tuzo ya kutambua mchango wake mkubwa wa kuhamasisha jamii kwa kile aanacho kifanya katika jamii na pia kuhamamsisha watu wengi waliokata tamaa.

download latest music    

Katika uzinduzi wa filamu yake ya mama, Aunty Ezekiel alitoa tuzo hiyo kwa shiloleh na kupokealwa na snura na kisha kumfikishia mwenye nayo.baada ya kupokea tuzo hiyo Shiloleh kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika

Naamini kuna wengi wanaostahili tuzo hiilakini siwezi kuwa na maneno mengi ya kutosha kushukuru  kwa heshima kubwa ulionipatia mama cookie, nashukuru sana  kwa zawadi nzuri.tuzo ya mama bora mpambanaji  bora kwa bongo fleva na movies katika uzinduzi wako wa filamu ya mama.lakini pia nakupongeza sana kwa kazi nzuri na product ya spray ulioizindua, wewe ni mwanamke shupavu.

Mama yangu aliniacha nikiwa mdogo sana kwaio nikaelewa mazingira magumu ya kuishi bila mama,na ndio maana siku zote nitapambana sana kwa ajili ya wanangu, ukiwagusa wanangu  umenigusa mimi.Hawa ndio watu pekee ninaoweza kusema nitakufa kwa ajili yao.

Shiloleh amekuwa akitambulika kama msanii na mwanamke mwenye moyo wa uthubutu na kujiamini sana ktikakufanya vitu na amekuwa moja ya wanawake wenye kuleta hamasa sana ukiangalia jinsi alivyoanza na mpaka sasa hivi alipofikia , watu wengi wanapata moyo kupitia yeye,.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.