Diamond Athibitisha Nafasi ya Mavoko Kupata Mrithi.
Ikiwa ni baada ya kupelekana BASATA, ndipo mkataba wa msanii Rich mavoko ulipofutwa katika lebel ya wasafi, msanii wa lebel hiyo ambae pia ni bosi katika kundi hilo Diamond Platinumz amethibitisha kuwa kuna mpnago wa kusajiri msanii mwingine katika lebo hiyo ili kuziba pengo aliloliacha Rich mavoko.
Rich mavoko ambae alikuwa msanii katika kundi hilo ameondoka katika kundi hilo huku akitoa tuhuma nzito kuhusu lebo hiyo kuwa wamekuwa wakinyonya wasanii na kwamba hakuna haki katika lebo hiyo na hata mikataba yao imkuwa ya unyonyaji.
Mbali na maneno ya Rich wasanii wnegine kutoka katika lebo hiyo walikataa skendo hiyo na hata ukiangalia wasanii wengi nje ya wasafi wamekuwa waktamani kuingia katikalebo hiyo kutokana na masiha wanayoishi wasanii hao katika umoja huo.