Diamond Kumpeleka Hawa wa Ntarejea Nchini India

Mwanadada Hawa ambae jina lake lilikuwa  maarufu kipindi ulipotoka wimbo wa nitarejea ambao alishirikishwa na msanii mkubwa Diamond Platinumz,  alikuwa akiomba msaada kwa muda mrefu  hapo nyuma na kutangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa hali yake sio nzuri kutokana na afya yake kudhoofu sana kutokana na ugonjwa unaosumbua.

Baada ya kipindi cha silawadu kumtoa msanii huyo , watu walianza kumuonea huruma huku wengine wakijitahidi kutuma salamu kwa Diamond ili aweze kumuonea huruma mwanadada huyo kwa sababu alikuwa mtu wake wa karbu sana kipindi walipokuwa wakifanya kazi.

download latest music    

Hata hivyo , baada ya kimya cha muda mrefu cha msanii huyo  sasa ameamua kuwajibu na kuthibitisha kuwa  sasa amaemua kumsaidia mwanadada huyo na kwamba hivi karibuni ataanza kupatiwa matibabu nchini India.

Diamond anasema kuwa amesikia kilio cha hawa muda mrefu na yupo katika mchakato wa kumpeleka nchini India ila hakutaka kutangaza swala hilo kwa sababu hakutaka msaada wake uonekane kama kiki kwa watu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.