Godzilla Athibitisha Kutokuwepo na Bifu Kati Yake na Bilnass.
Kwa muda mrefu kuliwahi kuwa na tetesi kuwa wasanii wawili Billnass na Godzilla wamekuwa na bifu na hiyo ni kutokana na kwambaBilnass amekuwa akifuata nyayo za Godzilla na kuiga sana muziki wake.
Hata hivyo baada ya kusambaa sana kwa tetesi hizo Billnass aliwahi kukanusha hilo lakii hivi karibuni pia mwanamuziki huyo aliamua kusema kuwa ana album mpya inakuja na katika album hiyo kutakuwa na kolabo yake na Billnass.
Kwenye album yangu mpya inayoitwa 5555 kuna ngoma yangu moja niko na billnsa na wala sina tatizo nae na ndio maana tumefanya kzi pamoja.:- aliongea Godzilla alipokuwa akiongea na Lilommy wa Times Fm.
