Harmonize Athibitisha Hana Bifu na Harmorapa wala Harmo Junior.
Msanii wa muziki anaefanya vizuri kwa sasa katika anga za muziki, Harmonize amethibitisha hana bifu na wasanii Harmorapa wala Harmo junior wasanii mabao wamekuwa wakitumia majina yake amabayo yeye ndi aliyetambulisha majina hayo katika anga za muziki wa bongo fleva.
Ingawa kitendo hicho kimeshtua wauwengi kutokana naukweli kwamba ingewezaka kabisa harmonize alitakiwa kuwa na chuki wa wasanii hawa kutokana na kutumia majina yake lakini hakuwa na kinyongo nao ingawa kwake ni mara ya kwanza kufanya hivyo lakini inaonyesha upendo fulani kwa wasanii hawa.
Harmonize anafunguka na kusema kuwa anafurahi kuona watu wana kuwa na tamaa ya jina lake kwa sababu hayo ni mafanikio kwake.
Katika ukurasa wake wa instagram , harmonize aliandika, mwiko kukata tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule, kwa sababu safari yako ya mafanikio ni ndefu sana.utakutana na changamoto nyingi sana kuna matusi , uonevu na kadhalika….. pale unapokata tamaa utakuwa pia umewavuna moyo watu wengi sana…mwenyezi mungu ni wa aabu sana na hajawahi kukosea katika hii Dunia, maisha ni kombolela…God bless you my twin brothers.