Ijue Siri ya Diamond Kuchaguliwa Kombe la Dunia
Mara nyingine labda watu wamekuwa wakijiuliza kwanini Diamond achaguliwe katika Kombe la Dunia kuiwakilisha Afrika na wala sio wasanii wengine waliopo Afrika, mbona kuna wasanii wengi tu wakubwa mbao wamekuwa wakifanya vizuri sana lakini hawajachaguliwa mpaka amechaguliwa Diamond.
Raia mmoja kutoka Afrika Kusini ambae ni mdau mkubwa wa muziki barani Afrika anafunguka na kusema kuwa yeye ndie alipwe jukumu la kutafuta wasanii watano kutoka afrika watakao shiriki kutengeneza wimbo wa kombe la dunia na kutokana na vigezo alivyokuwa navyo diamond haikuwa rais kuacha kumchagua.
Tim Horwood anasema kuwa diamond ni moja kati ya wasanii walijenga ngome kubwa sana barani A frika kupitiamuziki wake kiasi kwamba hata alipopewa kazi hiyo hakuweza kuacha kumfikilia Diamond Platinumz.