Kocha wa Yanga Amtolea Uvivu Diamond
Kocha mkuu wa timu ya yanga ameamua kumponda Diamond na kusema kuwa amekuwa akipenda sana kusikiliza muziki lakini hapendi sana kusikiliza nyimbo za mwanamuziki Diamond Platinumz kwa sababu amekuwa akifanya muziki kiujanja ujanja.
Kocha huyo wa Yanga ambae ni mwenyeji wa DRC, sehemu ambayo kwa kawaida imekuwa ikisika kuwa ndio sehemu muziki ulipozaliwa anasema kuwa amekuwa akivutiwa sana na msanii Alikiba na wala sio Diamond platinumz.
muziki wa hapa nimekuwa nikiufatilia na sio kwa kiasi kikubwa sana, namjua kuna diamond lakini simpendi sana kwa sababu ni mjanja mjanja sana kwenye mambo yake lakini nimekuwa nikivutiwa sana na Alikiba.
