Mke wa Roma na Stamina Waingili Kazi za Waume Zao.

Haijawahi kutokea katika burudani ya muziki kuwaona wanawake wakiingilia kazi za wanaume zao hasa katika muziki wa hip-hop, hii inaweza kuonyesha ni jinsi gani wanawake hawa wamekuwa na upedo wa waume zao kiasi kwamba mpaka wameamua kujipanga kuwasapoti wale wa ubavu wao.

Mjengoni jana, wanawake wa Roma na Stamina waliibuka na kuamua kuja kuwasapoti waume zao kwa kuja kuwasaidia kutambulisha nyimbo yao mpya, ambapo katika kujitetea kwao walisema waliamua kufanya hivyo kwa sababu wasanii hao wameenda kufanya shooting ya wimbo huo.

download latest music    

Roma na Stamina wanaunda kundi moja la muziki na wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu, hivyo wameamua kuwaunganisha pia hata watu wa karibu wa familia zao ili kufanya sapoti katika muziki wao.

kwa upande wa Roma, mke wake tumekuwa tukimuona mara nyingi sana akiwa bega kwa bega nae katika matatizo na raha zote za muziki anazokuwa anapitia mke  wake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.