Muonekano wa Msanii Ndio Unaouza Kazi zake.:-Tammy the Baddest
Msaii wa rap wa kike nchini Tanzania , Tammy the Baddest amefunguka na kusema kuwa kwa kawaida kitu kikubwa kinachoweza kuuza kazi ya msanii ni muonekano wake kwanza kabla ya kazi yake yenyewe.Na hii inakufanya watu wakuone kuwa wa thamani hata kutamani kufanya kazi na wewe.
Msanii kama msanii hasa mtoto wa kike ni lazima uwe full package,sio uonekane tu unafanya muziki basi, no! u have to sale.ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri , ili hata kama unashida mtu aone mmmh yani kumpa show tammy kwa kiasi fulani , hapana.
Tammy pia amesema kuwa hata yeye amekuwa akijari sana muonekano wake ingawa kuna muda inampa changamoto kwa sababu mashabiki na watu wanaomuona wanahisi kama ana ela sana.
