‘Najiamini’, Alikiba akanusha kuiba wimbo wa seduce me

kwa mara ya kwanza kwa mwaka huu tamasha kubwa nchi  la Fiesta limefunguliwa huko mkoani Arusha  na kujumuisha wasanii wengi wakubwa , lakini katika wasanii hao msanii mkubwa Alikiba anaetamba na kibao kipya cha “seduce me” alikuwa ni mmoja wa msanii aliepata bahati ya kuwepo katika ufumbuzi huo.

Akiongea na Ayo TV  usiku wa tamasha ilo lililofanyika tarehe 9 septemba msanii alikiba alikata katukatu kwa tuhuma izo zinazomuandama kuwa kibao icho kipya cha seduce me sio chake bali ameiba, king kiba anasema kuwa ‘Izo ni stori tu,siku zote unapofanya kitu kizuri lazima watatokea watu waige kidogo….najiamini sana na wimbo wangu ni mzuri

download latest music    

katika tamasaha hilo alikiba alijikuta akiperfome wimbo huo zaidi ya mara tatu kutokana na uhitaji wa mashabiki, lakini kwake ni furaha na anasema hata yeye amekuwa akienjoy sana anapoona mashabiki wakiomba wimbo kurudiwa kwa sababu hata yeye anaamini kuwa wimbo huo ni mzuri sana na perfomance ya arusha imekuwa ni moja kati ya show zake zilizoongezeka katika historia ya muziki wake.

Tamasha la fiesta ndio kwanza limeanza na linalengo la kuzunguka mikoa zaidi ya 15 tanzania nzima hivyo basi tunategemea show zingine nzuri zaidi kutoka kwa wasanii wetu kwa kipindi chote cha Fiesta huku ikionekana ndio kipindi ambacho wasanii wengi hupata kukutana na mashabiki wao

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.