Otile Brown na Sabby Angel Wasemekana Kuwa Wapenzi.
Mwanadada Sabby Angel kutoka tanzania anasemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii kutoka kenya Otile Brown ambae hivi karibuni alisikika kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi Vera Sidika wa nchini humo.
Wakati wawili hao wakihaha kujinasua katika mapenzi hayo na kila mmoja akitaka kujiona kuwa hana makosa kwa mwenzake, Sabby angel pia alitafutwa ili kuelezea ukweli wa swala hilo ambapo hakupatikana kusema ukweli wa mambo.
Watu wake wa karibu walisema kuwa mwanadada huyo kwa sasa yuko nje ya nchi ingawa haijajulikana yupo nchi gani , lakini hawakusema kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa.
