Queen Darleen asema Diamond Atasubiri Yeye Aolewe Ndio na Yeye Aoe
Mwanadada pekee kutoka kundi la wcb Queen Darleen,amefunguka na kusema kuwa wakati wake wa kuolewa ukifika lazima na yeye ataaolewa tu kwa sababu hata yeye ni binadamu na pia ni mwanamke kwaio hawezi kuacha kuolewa.
Watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka sana mahusiano ya kimapenzi ya Queen Darleen kutokana na ukweli kwamba mwanadada huyo hajawahi kuonekana sana akiwa na mwanaume yoyote na pia ni kutokana na muonekano wake ambao mara nyingi anaonekana ni wa kiume.
Mimi sina shida , ndoa ni majariwa na kama mungu atanijalia basi na mimi nitaolewa na mimi ni binadamu na nina hisia vile vile kwaio nikipata mwanaume na mungu akinijalia basi nitaolewa tu.
Hata hivyo queen darleen anasema kuwa pamoja na kwamba yeye bado hajajua muda wa kuolewa lakini yeye ni mkubwa sana kwa diamond kwaio lazima diamond atasubiri sana kuoa mpaka yeye aolewe kwanza.
