Riyama Amsifia Mume Wake kwa Kuwa Mwaminifu.
Mwanadada Riyama Ally amezidi kumsifia mume wake mpenzi kwa kusema kuwa mwanaume huyo ni mwaminifu sana kiasi cha kwamba amekuwa katika ndoa yao kwa miaka minne sasa lakini hajawahi kuona wala kuhisi mwanaume wake akiwa na mchepuko wala kukutana na meseji za ajabu katika simu yake.
Riyama na Rey walifunga ndoa miaka kama minne iliyopita na ni moja ya ndoa za wasanii zilizodumu na kutokuwa na skendo katika mitandao ya kijamii kila siku kutokana na kuweka sana mambo yao chini ya kapeti.
niko na mume wangu mwaka wa nne sasa na wala hata siku moja sijawahi kuona meseji ya mwanamke katika siku yake hata ya kusingiziwa tu– Anasema Riyama.
