Stamina Atamani Kuwa na Media House Kama Diamond
Msanii wa hip-hop Stamina amefunguka na kuongelea juhudi za diamond baada ya kufungua media house yake ambayo itakuwa ni kama chachu kwa wasanii wengine kutamani kufanya kama alivyofanya yeye.
Stamina ansema kuwa anamuona diamond amepiga atua kubwa kwa sababu kitu alichokifanya hakuna aliyewahi kukifanya na kama kuna mtu atakuwa kimya bila kumpa sifa diamond basi ni mtu mwenye roho mbaya .
ni steji nzuri alichokifanya kama una roho mbaya utakiona kitu cha kijinga ila kama una roho nzuri unaachaje kumsifia mtu ambae kajitahidi na kuweka efforts zake, namsifia mimi siwezi kuacha kumsifia , siwezi kuwa na negative though ukiona mtu anafanya vile ujue ana step anatoka hapa na anafanya vile.
Stamina ansema kuwa alichokifanya diamond ni chachu kwa wasanii wengine na hata yeye ametamani sana kuwa na media house kama Diamond.
lazima iwe chachu msanii gani ambae hatamani, hata mimi natamani kuwa na media house yangu kwa sababu kutoka kupigwa nyimbo yako kwenye media hadi kuwa na media yake kuamua anapiga mud wowote anaotaka.