Chaz Baba Adaiwa Kubadili Dini Ili Aoe Mke Mwingine

Msanii wa muziki wa Dansi nchini kutokea bendi ya The African Stars band ‘Twanga Pepeta’ Charles Gabriel maarufu kama Chaz Baba amedaiwa kuabadilisha dini ili apate kuoa mke mwingine.

Global Publishers wanaripoti kuwa Chaz Baba anadaiwa kubadilisha dini kutoka Ukristo kwenda Uislam ili aweze kuoa mke mwingine huku ndoa yake ya kwanza na mwanamama Rehema Sospeter ambaye alifunga naye kanisani ikidaiwa kuvunjika.

Inaripotiwa kuwa kulikuwa na mgogoro wa mda mrefu kati ya Chaz Baba na mkewe huyo kiasi ambacho kuna kipindi mkewe huyo alikuwa akiondoka na kurudi kwao kisha kurejea tena kwa mumewe. Ilisemekana kwamba ilikuwa ni kawaida yao kutofautiana na kuyamaliza, lakini safari mkewe aliondoka na hakurudi tena.

Baada ya mkewe kugoma kurudi ndipo Chalz Baba alianza harakati za kutaka kuoa Mke mwingine kwa kubadilisha dini.

Baada ya Tetesi hizo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Chalz Baba ili kupata ukweli wake ambapo alikiri kubadilisha dini na kusisitiza anaoa mwanamke ambaye sio maarufu baada ya Tetesi kuwa anataka kumuoa muigizaji wa Bongo movie Husna Sajent.

Ni kweli kabisa na sasa hivi ninaitwa Adulkarim na ndoa yangu ni mwezi ujao (mwezi wa kumi na moja).

Sajenti? (kicheko) hapana, mke wangu mtarajiwa siyo maarufu hata kidogo. Yeye yupo bize na kazi zake tu maana ni mfanyabiashara“.

 

Wema Sepetu Adaiwa Kumpiga Vibao Chalz Baba Hadharani Kabisa

Muigizaji wa Bongo movie Madam Wema Sepetu amerudi Kwenye headlines Tena huku safari hii akidaiwa kumtandika vibao hadharani aliyekuwa mpenzi wake Chalz Baba.

Global Publishers wanaripoti kuwa tukio hilo lilitokea ukumbi wa burudani wa The Club Legend (zamani Nyumbani Lounge), ambapo Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ilikuwa inafanya shoo ambapo inadaiwa Wema alimpiga vibao Chalz Baba huku kisa kikiwa ni Husna Sajent.

Inadaiwa kuwa Baada ya Chaz Baba kuburudisha jukwaani na wanamuziki wenzake, alishuka na kwenda maliwatoni, wakati akitoka huko alikutana na Wema njiani na baada ya mazungumzo machache watu walishuhudia Wema akimzaba makofi kadhaa Chaz Baba.

Global Publishers lilipojaribu kumsaka Wema na kumuuliza juu ya tukio hilo na kutaka kujua sababu ya kumpiga aliyewahi kuwania mpenzi wake Wena alichomoa na kusema “No Comments”.

Baada ya sakata hilo Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Chalz Baba ambaye alifunguka:

Tulikuwa vizuri tu maana jioni tulikuwa naye pamoja kwenye kikao cha kamati ya Miaka Ishirini ya Twanga maana na yeye ni mjumbe, tunategemea kusherekea naye siku hiyo kwa sababu itakuwa ni siku yake ya kuzaliwa pia usiku huo.

Hakukuwa na shida yoyote. Sasa nimeshuka jukwaani naenda maliwatoni mara nikakutana naye akaanza kuniuliza kwa nini Sajenti ananiposti kwenye mitandao ya kijamii na kwa nini tupo karibu.

Mimi nilimjibu kuna shida gani kwa sababu nina uhuru wa kuwa karibu na mtu yeyote yule na yeye hawezi kunipangia masharti kwa sababu si mpenzi wangu.

Nilipomjibu tu hivyo nilishitukia nazabwa makofi kadhaa usoni. Kalala alikuwa karibu ikabidi amtoe. Kiukweli ni kwa sababu ni mwanamke lakini angekuwa mwanaume mwenzangu pangechimbika”.

Ndoa Ya Chalz Baba Yadaiwa Kuingia Mdudu

Msanii wa muziki wa Bendi Charles Gabriel maarufu kama Chalz Baba aliyejizolea umaarufu Kwenye bendi ya Mashujaa amedaiwa kuwa Kwenye utata kuhusu ndoa yake.

Global Publishers wanaripoti kuwa Chalz Baba na mke wake Rehema Sospeter wamemwagana kisa ni maugomvi ya kila siku ambayo hyaishi ndani ya nyumba.

Lakini pia inadaiwa baada ya wanandoa hao kuachana Chalz Baba Kurudisha mapenzi kwa mzazi mwenzake ambaye pia ni msanii wa Bongo movie Husna Sajent.

Unajua Chaz na mkewe huyo mara nyingi wamekuwa wakigombana mara kwa mara kisha wanawekwa sawa wanarudiana tena. Lakini safari hii inaonekana wazi kuwa ndoa yao haipo tena, kwani mwanamke huyo kabeba kila kitu ndani kaondoka na ni muda mrefu sasa hawaishi pamoja na mwanamuziki huyo amerudisha mapenzi kwa Sajenti”.

Baada ya tetesi hizo kusambaa gazeti hilo lilimsaka Husna Sajent ili kujua kama jambo hilo Kiba ukweli ambapo alikataa tetesi hizo na alipoulizwa zaidi alikata simu.

Lakini pia Chalz Baba aliweka wazi kuwa yeye mke wake wamegombana Lakini anaamini watayaweka mambo sawa na Kurudisha mapenzi yao kama mke na mume.