Jinsi Waaandishi wa Habari Walivyomtolea Povu Diamond Platinumz.

Hivi karibuni msanii diamond platinumz amefungua rasmi kituo chake cha habari ambacho kitakuwa na radio na tv, lakini waandishi wa habari kutoka tanzaia wamemjia juu msanii huyo kwa kitendo chake  cha kwenda kutafuta waandishi wa habari na wafanyakazi wa radio hiyo mtaani bila kujali kuwa kuna vigezo na masharti ya habari.

Waandishi hao wanasema kuwa kazi ya uandishi wa habari inatakiwa kuwa na proffesional yake kwaio alichokifanya Diamond sio kitu sawa kabisa na hajafanya vizuri.

Akiongea na online tv, mmoja wa waandishi wa habari wa gazeti penda hapa nchini  Chritopher Lisa ambae ni mwandishi wa habari anasema kuwa

swala la dimaond kwenda kuatafuta wafanyakazi mitaani kwa ajili ya radio na tv yake mi naona ni kama vile amekos watu wa kumshauri kwa sababu uandishi wa habari ni taaluma kama zingine,taaluma hiyo inahitaji watu waliosoma na ambao wamekidhi vigezo vya habari kwa mfano sasa hivi tuna sheria kuwa watu wa habari ni lazima wawe hata na diploma tu,ambapo serikali ilitoa miaka mitano kwa waandishi kwenda kusoma.

kitendo cha diamond kwenda kutafuta waandishi nje ya taaluma ya habari sidhani kama kitamsaidia sana kwa sababu kutangaza sio kwamba ni sanaa au muziki ule kusema kuwa utatumia kipaji chao. kuna taratibu , sheria na kanuni za kuzungumza na hata kuongea pia sio unaongea tu blaah blaah

Mwandishi mwingine ambae pia aliguswa na jambo hilo alisema;

Kutafuta watangazji kwa kutumia njia ya viapaji ni kosa kubwa sana kwa sababu kwa jinsi a ambavyo sasa hivi tanzania tunaelekea katika mfumo wa kuatambua taaluma ya mwandishi wa habari sasa unapochukua watu bila taaluma madhara yake ndo haya sasa unashangaa kwanini kuna habari fulani imetokea ni kwa sababu watu hawana taaluma na hawajafata mchakato wa upatikanaji habari.Namshauri diamond afany matangazo ya kazi na watu wafanye interviews.

Moja ya mwanafunzi na shabiki wa diamond alisema

kwa mfano kama mimi ninavyosomea IT, Nikisema kuwa nataka kufungua mgahawa wa kuhusu maswala ya kumputa basi ni lazima nitaajiri watu waliosomea kitu ninachotaka kukifanya.

 

Mjini Sio Kujua, Its All About Techniques-Diamond platinumz.

Msanii wa  mkubwa wa muziki bongo Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wameshindwa kufanikiwa katika maisha kwa sababu wanashindwa kusihi vizuri na watu na wanatumia nguvu nyingi katika maisha wakati ili uweze kufanikiwa ni kuangalia jinsi gani uanishi na watu vizuri na njia gani unatumia kufanua maisha yasowe magumu.

Diamond ameongea hayo alipokuwa akipiga stori na bagh_dad wa Efm na kumwambia kuwa lazima kuwe na techniques nzuri za kuishi mjini , lakini pia kama unaishi na watu vizuri hata unapopata shida watu wanaokujua na kujua tabia zako lazima watakusaidia hawatakuacha.

unajua mjini sio kuishi kwa kujua, ni namna unavyoishi na watu tu , inawezekana mimi ninajua kitu kuishia hapa lakini kumbe wewe unajua kuanzia nilipoishia mimi na kwenda mbele.na kama nina mazungumzo mazuri na wewe uwezi kuniacha mimi niangaike nisiendelee utanisaidia ili nisogee, kwaio sio kujua ni kuang.alia njia gani unazitumia na unaishije na watu, its all about techniques–Alifunguka Diamond.

Maneno ya diamond yanadhihirika kutokana na jinsi yeye alivyo na moyo wa kujitoa kusaidia wengine katika tasnia ya muziki ambapo kila siku anasema kuwa ndoto yake kubwa ni kuona wasanii wachanga wanafika mbali.

Hata hivyo Diamond alishawahi kusema kuwa hata wasanii anaowatoa yeye ikiwemo rayvanny na harmonize wamekuwa wakifanikiwa ni kwa sababu na nidhamu walioyonayo katika kazi na moyo wa kujituma.

Diamond Atuma Salamu za Pole Kwa Rick Ross

Imeripotiwa wikiend hi kuwa msanii mkubwa wa muziki dunianai rick ross ni mgonjwa na kwa muda amekuwa akitumia mashine ili kuweza kumsaidia kupumua.msanii huyo william leornard  roberts ameripotiwa kulazwa katika hospitali moja nchini marekani baada ya kuchukuliwa kwa dharura nyumbai kwake miami alipokuwepo kwa wakati huo.

kwa mujibu wa ripoti ya TMZ, inasemekana kuwa mtu mmoja wapo aliekuwepo nyumbani kwake alipiga simu ya dharura na kuombamsaada baada ya kuona kuwa hali ya msanii huyo imekuwa mbaya na hawezi kupumua hali iliyosababisha pia kushindwa kuongea.

Baada ya kupelekwa hospiatali na magari ya msaada wa haraka, iligungulika kuwa msanii huo anasumbuliwa na Pneumonia hivyo kuanza kupatiwa matibabu mara moja.

Akiwa kama mmoja wa ambassador wa kinywaji cha Belaire nchini  na mwanamuziki aliefanya nae kolabo , Diamond Platinumz ametuma salamu zake za pole kwa msanii huyo mkubwa ulimwenguni.kupitia ukurasa wake wa instagram , Diamond Platinumz aliweka picha ya rapa huyo na kuandika “get well soon” ikiwa ni ishara ya kumtakia apone haraka na matatizo yanayomsumbua.

 

Diamond Atoa Fursa ya Vipaji vya Utangazaji Bongo

Wakati bado wanasubiri kuwasha mitando ya radio na televishei zao kwa ajili ya kazi zao na kazi za wasanii wengine ili kukuza soko la muziki Tanzania, meneja wa lebo ya wcb Diamond Platinumz anaonekana bado ana nia ya kutoa fursa na ajira kwa watu wengine ambao sio wasanii katika vituo hivyo vya habari.

Diamond na lebo yake ambao wamepanga kufanya mapinduzi ya muziki kwa kutaka kufungua radio na televisheni kwa ajili ya kazi za wasanii, ameamua kutoa fursa ya utangazaji kwa vijana wa Tanzania katika stations hizo.

Katika ukurasa wake wa instagram, Diamond Platinumz aliandika “please tell me from you perspectives,which cuty has the best radio and tv presenter,….eti nina swali ni mkoa gani ambao una vipaji vya utangazaji.-Aliandika Diamond.

Diamond anaweza kuwa ni moja ya wasaniiwachache afrika ambao wanataka kukuza muziki tanzania lakini ni mtu mwenye moyo wa kusaidia vijana wenguen wa nyanja tofauti tofauti.ukiachana na kutaka kufungua radio na televisheni, Diamond alishafanikiwa katika kufungua lebo hiyo ya wcb na kutafuta wasanii chipukizi kwa ajili ya kuwasaidia kuinua viapji vyao.

Wasanii ambao mpaka sasa wamekuwa chachu ya mafanikio ya muziki kwa wasanii wengien kutokana na kazi nyingi na nzuri wanazofanya za kukuza na kuutangaza muziki nje ya Tanzania.

Baadhi ya wasanii wanaopatikana katika lebo ya diamond ni pamoja na Rayvanny, Harmonize na Lavalava.

Siri Nzito Yafichuka Kuhusu Biashara ya Diamond Platinumz

Kwa muda mrefu kidogo diamond amekuwa akisifika kwa kuwa ni moja ya wasanii wachache walioamua kuwekeza  katik biashara ukiachana na kazi ya muziki anayoifanya.diamond alizindua karanga za Diamond zinazotengenezwa na kampuni ya Smart na kuwa na manukato yake mwenyewe yanayojulikana kama chibu.

Lakini hivi karibuni kuna habari na tetesi zilizokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amekuwa akiwadanganya mashabiki wake kuwa karanga hizo ni za kwake kumbe karanga hizo zna ubia na watu wengine kutoka nje ya nchi lakini pia bosi wa clouds media pia amekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha biashara hiyo.

Hivi karibuni msanii  Diamond Platinumz ambae  alihusishwa katika ugomvi wa shilawadu , meneja wa clouds media group na mcheza dance wa WCB (Mose Iyobo), na kusemekana kuwa media hiyo inataka kumpoteza msanii huyo kwa kumfanyia figisu za kutaka kuua muziki wake hali iliyopelekea mpaka meneja wa msanii huyo kutaka kuweka siri za bosi wa Clouds Media.

Hata hivyo habari zilizopo mjini ni kwamba boss ya kampuni na bidhaa hiyo ya diamond karanga alikuwepo nchini siku za hivi karibuni na kupokelewa na  Mmoja wa viongozi wa Clouds Media ambapo alikuwa kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya biashara hiyo iliyopewa jina la msanii huyo mkubwa.

Mwekezaji huyo alijulikana kwa jina la Mr. Radima aliweza pia kufanya  ziara   yake katika ofisi za Clouds Media hivi karibuni na kupokelewa na joseph kusaga  hapo mikocheni, ambapo Mr Radima ni mmiliki wa kiwanda kinachozalisha diamond karanga ambapo  msanii diamnd ni balozi wa karanga hizo .

Baada ya kusambba kwa tetesi za ziara ya bosi huyo ndipo mashabiki wengi waliazna kufumbuka na kusema kuwa wengi wao walikuwa wakijua kuwa Diamond karanga ni baishara yake kumbe yeye ni balozi tu.

 

Mama Mobeto Achoshwa na Skendo za Diamond.

Mama wa video queen maarufu nchini Mama Mobeto amefunguka na kusema kuwa amechoshwa na tabia ya waandishi kuwa wanamuliza maswaka yanayomuhusu diamond wakati wao sasa hivi wako busy na kufanya kazi na sio kuzungumziwa katika mitandao ya kijamii.

Mama Mobeto amsema hataki kabisa kusikia habari zinazomuhusu Diamond kwa sababu kila mtu sasa hivi ana maisha yake hivyo waache kumfatilia.

jamani sisi mambo hayo ya kwenye mitandao hatuna kabisa,hata mtoto wangu ameshayasahu hayo mambo kabisa sas hivi, badala yake yupo kabisa na mambo yake mengine sasa hivi.michakato  yetu sasa hivi ni kutafuta pesa na wala sio kitu kingne kabisa.muda wa kuchokoana katika mitandao hatuna tena sasa hivi michakato yetu ni kutafuta pesa tu sasa hivi .tukiwa tunaongelea hivyo hatuwezi kupiga hatua kabisa kwaio kama kuna watu wana weza kufanya hivy acha wao wafanye tulishajivua kabisa na hayo mambo na hata huyo Diamond hatutaki kusikia mamneno yake tena.

Wakati Mama Mobeto akisema hayo kuhusu diamond na maisha yao mpaya huku  mtoto wake Hamisa alipost maneno katika mtandao wa snapchat kuwa amemmsi mwanaume wake ambao inasemekana kuwa mwanaume huyo ni diamond platinumz.

Diamond Atoa Siri, Aelezea Sababu ya Wasanii wa WCB Kufanikiwa.

Msanii mkubwa bongo Diamond Platinumz aefunguka na kutoa siri ya kinachowafanya wasanii wote katika lebel yao ya Wcb kuwa wanafanikiwa kila wanapotoa wimbo unapendwa na hata kama imechukua muda mchache kuja katika game la muziki.

Diamond amefunguka hayo siku ya Jumamosi alipokuwa akimkaribisha na kumtambulisha msanii mpya wa wcb , maromboso ambae mara ya kwanza laikuwa ktaika kundi la Ya Moto Band kabla kundi hilo halijavunjika na kusambaratika.

Diamond anasema kuwa katika kuwatoa wasanii wake katika lebel hiyo hajawahi kufanya hivyo kama biashara kama wanavyofanya wengine bali yeye anawato wasanii wengine kwa sababu anataka watoke na waweze kusaidiana kwa sababu wapo wengi wana vipaji lakini wanashindwa kutoka.

Diamond anaongezea na kusema kuwa kinachomtia moyo kutoka kwa wasanii hao ni kwa sababu wamekuwa wakijituma sana na hata kuacha  kulala usiku ili kuhakiisha kuwa kazi zao zianakwenda vizuri kwa sababu hawafanyi kwa ajili yake bali ni kwa ajili yao na familia zao.

nafikiri kwa sababu mimi sifanya hivyo kibiashara, watu wengi wamekuwa wakiifanya kibiashara lakini mimi ninafanya kwa ajili ya kujikomboa,na kila mtu apate kulingana na kazi ile anayoifanya.na ndio maana kila mtu anaefanya kazi wcb anafanya kazi kwa kujituma na kwa moyo mmoja kwa sababu anajua kabisa kile anachokitengeneza hamtengenezei Diamond au Wcb, bali anafanya kwa ajili ya yake na familia yake.

Diamond ni msanii aliyejitolea kwa muda mrefu sasa kutoa wasanii wadogo na kuwaingiza katika game la muziki, na kwa bahati nzuir wasanii wote kutoka katika lebel hiyo wamekuwa wasanii wakubwa na kufanikiwa sana hata kuanza kutambulika kimataifa,wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Lavalava na Queen Darlen ni wasanii zao kutoka Wcb na wamekuwa wakifanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.

Diamond Ahudhuria Mazishi ya Shabiki yake.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinumz jana alihudhuria mazishi ya moja ya shabiki zake wakubwa mtandaoni na nje alifariki kwa ajali ya gari siku tatu zilizopita.kijana huyo aliekuwa akijulikana kuwa ni moja ya mwanamchama mkubwa wa Team Wcb aliejulikana kama Philly Nevvo  alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar- Es- Salaam.

Siku chache zilizopita mashabiki hao wa Wcb, walipata ajali mbaya ya gari walipokuwa maeneo ya Chalinze wakitokea Morogoro kurudi Dar-Es-Salaam.

Mashabiki na watu mbalimbali waliohudhuria msiba huo

Diamond akiwa na baadhi ya mashabiki katika msiba huo.

Akiongea katika mazishi hayo diamond anasema kuwa kuondoka kwa philly ni pigo kubwa sana kwa sababu alikuwa ni zaidi ya ndugu aliejitolea kumsapoti na kutumia muda mwingi kuangaika nae.

nikisema nimzungumzie mazuri yake ni vigumu sana, unaweza kuwa na ndug yako na bado asikusapoti lakini yeye alikuwa natumia muda wake na ela yke kununua bando kukusapoti na unaona kabisa ana mapenzi na wewe..kuondoka kwake ni pigo kubwa sana,tumeondokewa na mmoja wa watu muhimu sana na ni mtu ninamheshimu sana , hata kama ninashughuki gani katika mambo kama haya lazima nije kuzika. -Alifunguka Diamond.

Mr.blue Hana Beef na Diamond Platinumz.

Msanii wa  muziki nguli Bongo Mr.Blue amefunguka na kukanusha maneno yanayosambaa katika mitandoa kwa muda mrefu  ya kusema kuwa yeye na msanii mwenzie wa muziki Diamond Platinumz wako katika beef zito linalowafanya washindwe kufanya kazi za muziki kwa pamoja.

Mr.Blue amesema kuwa yeye na Diamond walishawahi kufanya kazi mbili  hapo nyuma labda kwa sasa wafanye tena lakini sio kweli kuwa  yeye na Diamond wana beef linalowafanya washindwe kushirikiana.mMr blue anasema kuwa kwa sababu watu wamekuwa wakizusha kuhusu beef lao basi kama kuna uwezekano watafanya kolabo tena ili kuthibitisha kuwa hakuna beef kati yao.hata hivyo anasem akuwa kitu kikubwa kinachowafanya washindwe kufanya kolabo ni kwa sababu wote ni wasani wakubwa na kunakuwa na u-busy kati yao wa kushindwa kukutana.

ni mtu nilishashirikiana nae  sio kitu cha kushangaza kwamba  labda kusema haitawezekana kufanya nae kazi pamoja,lakini unajua shida mnapokuwa wasanii wakubwa kila mtu anakuwa busy  kwa upande wake lakini ikija kufanyika kolabo kati yangu na yake basi inakuwa kitu kizuri sana kwa sababu tutawaonyesha raia kuwa hatuna beef lolote.

kwa kwelie sina tatizo lolote na diamond , ni mdogo wangu ninamuheshimu na ninaheshimu hustle zake, na amekuwa mfano wa kuigwa kwa watu.hayo mambo mengine tusiyachukulie sana serious.

Diamond na Mr blue walishawahi kufanya kazi kwa pamoja kama katika  nyimbo ya BBM  ambao waliimba wakiwa na msanii mwenzao ambae sasa hivi ni marehemu , Ngwea.na pia wimbo wa Dimaond  ambao unajulikana kama kiss to the lady .

Wasanii wengi wanakuwa na beef na migogoro isiyokuwa na maana inayowafanya washindwe kufanya kazi pamoja na kukuza soko la muziki, Mr.Blue anasisitiza kuondoa tofauti zinazotokea kati ya wasanii ili kukuza muziki wa Tanzania.

kwa upande wa diamond kumekuwa na tetesi nyingi za yeye na wasanii wengi kutokuwa na maelewano mazuri ambapo wasanii kama bob junior, alikiba ambao wamekuwa wakishindwa kukaa meza moja na kuzungumza yakaisha na kurudi kufanya kazi pamoja.

Madalali Nyumba ya Diamond Waendelea Kuleta Utata.

Baada ya Diamond Platinumz kutangaza kuwa amenunua nyumba yenye gharama kubwa kwa ajili ya kufanya ofisi ya lebel yake nzima na wafanyakazi na wasanii wake , zilizuka tetesi na kusambaa kuwa msanii huyo amedanganya  umma kwa kusema kuwa nyumba amenunua ilhali sio kweli bali nyumba hiyo ilikuwa ni ya kupangisha .

Hata hivyo Mange Kimambi , mwanamama anayevumbua mambo mengi yanayofichika kwa jamii na kwa wasanii alisema kuwa nyumba inayotangazwa kununuliwa na Diamond sio kweli kuwa imenu nuliwa bali nyumba hiyo ni ya familia moja ambayo inahitaji ela kwa ajili ya kusomesha watoto hivyo nyumba hiyo ambayo ni ya urithi haiwezi kuuzwa kwa sababu  ipo kwa ajili ya kusomesha watoto.

Daada ya maneno mengi kutokea, aiyedaiwa kuwa ndie dalali aliyemsaidia diamond kupata nyumba hiyo alifunguka na kusema kuwa ni kweli kuwa nyumba hiyo ilinunuliwa na diamond kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

Lakini bado haikuishia hapo, dalali wa familia wa nyumba hiyo aliamua kutoa ukweli wa tamko ilo na kusema kuwa sio kweli kuwa nyumba hiyo ilikuwa inauzwa bali nyumba hiyo ilikuwa katika mtandao kwa muda mrefu kwa ajili ya kupangishwa.

Dalali huyo alijulikana kama dalali kiongozi alisema kuwa ukweli ni kwamba anampongeza Diamond kwa juhudi anazokuwa anafanya kwa sababu hata kukodisha nyumba kubwa na yenye thamani kama hiyo ni swala la kujivunia lakini nyumba hiyo haijanunuliwa.

kiukweli nataka kusema tu kuwa niamini mimi ninachokwambia amepanga,na swala la kwamba yeye ni dalali ni kweli lakini yeye aliipata hiyo nyumba kupitia mimi kwa sababu alipiga simu kuniambia kuna mtu anatafuta nyumba kwa ajili ya ofisi na tukasema ile itamfaa.

Hata hivyo dalali huyo anasema kuwa nyumba hiyo ilikuwa ina matangazo yake mengi katika kurasa zake za instagram kwamba inapangishwa  na hata ukiangalia matangazo ya kupangishwa kwa nyumba na ya nyumba kuchukuliwa yapo.

Dalali huyo anasema kuwa nyumba hiyo ilikuwa inapangishwa kwa muda mrefu na ilikosa wapangaji kwa sababu ilikuwa ikipangishwa kwa gharama sana hiyo wapangaji walikuw wakishindwa bei hiyo.

Holiday Season Ya Familia Ya Daimond Huko S.A

Imekuwa ni moja ya furaha kwa familia ya diamond pamoja na wafanyakazi wake na marafiki  w karibu hasa walipoamua kufanya birthdau party ya mtoto wake wa pili wa kiume nillan na kuamua kuwa na siku za mapumziko juko south afrika.Nakuletea kwa picha baadhi ya matukio ya familia hiyo.

Diamond akiwa na mkwe Zari

Diamond akiwa na mama yake mzazi

team nzima ya wasafi  pamoja na wake zao.

Aunty ezekiel akiwa na Zari the Bossy

Diamond akiwa na mkewe na mama yake mzazi

Matukio Kwa Picha:Birthday Party Ya Mtoto Wa Diamond Platinumz

Weekend iliyopita ilifanyika party ya mtoto wa msanii mkubwa Tanzania Diamond Platinumz iliofanyka nchi Afrika Kusini  na kuhudhuriwa na familia nzima ya Diamond Platinumz pamoja na wasanii wote kutoka WCB na watu wa karibu wa familia hiyo.Nillan  ni mtoto wa pili kuzaliwa baada ya Princess Tiffah ambao wanakamilisha idadi ya watoto wawili kutoka kwa mwanamama kutoka Uganda Zari The Bossy.

Familia ya wasafi ikiwasili kutoka Tanzania wakiingia Afrika ya Kusini.

Muonekano wa ukumbi kwa nje, wakati wa maandalizi.

.

Diamond akiwa na meneja wake Babu Tale

Diamond akiwa rafiki zake wa karibu na familia yake pia , pichani kushoto ni mama wa Diamond, Zari The Bossy na watoto wake.

Tiffah akiwa na mdogo wake Nillan ambae ndie ilikuwa siku yake rasmi.

Zari The Bossy akiwa na wakwe zake, mama yake mzazi na Diamond pamoja na mumewe.

Diamond akiwa na mkew Zari.

wakati wa chakula cha pamoja katika sherehe iyo.

Diamond na kundi zima la Wasafi wakiwa wanatumbuiza katika party hiyo.

Moja ya wasanii kutoka kundi la mafikizolo nae alipata nafasi ya kushiriki katika party hiyo.

 

 

 

H.Kaba kumaliza Beef Lake Na Diamond.

Msanii mkongwe alikuwa katika miondoka ya dansi H.Baba, ameamua kumaliza beef alilokuwa nalo na msanii mkubwa na anayefanya vizuri   kwa sasa bongo Diamond Platinumz kwa kuweka picha ya msanii huyo mkubwa akiwa na mzazi mwenzie Zari The Bossy hivi karibuni na kuandika maneno yenye kuonyesha kuwa hana chuki na wawili hao.

H.baba amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na mahusiano ya Diamond na Zari kwa muda mrefu na kwa sasa anawashauri waweze kuoana kwa kufunga ndoa na kama msanii mwenzie atatoa ngombe watano kwa ajili ya harusi hiyo.

H.baba ameongezea na kusema kuwa hawezi kuficha hisia zake kwa couple hiyo kwa sababu amekuwa akivutiwa nayo kila anapoiona ana amekataa kuwa kaa kwa kutaka kurudisha nyuma mahusiano hayo kwa sababu watu hao wanapendana na wamekuwa wakiendana sana.

Kinyama mnapendezana sana na mnaendnana sana , Mungu awasimamaie na kuwaongoza mfunge ndoa awe wako katika hesabu ya mwenyezo mungu,natoa ngombe watono kabisa wakubwa wa kisukuma waletwe Dar, huo nduo uwezo wangu  na hicho ndicho ntaajaliwa na Mwenyezi mungu.nakutakia maandalizi mema ya ndoa yako na hongera kwa kupendana……ninaheshimu mahusino yamtanzania mwenzangu#MIMINIMZALENDONANIMEKATAAKUWAKAA #Usinilazimishekwamanenoyakokuwakaa #Natudiatenanimekataakuwakaa.

Hii inakuja baada ya muda mrefu msanii h.baba kuwa katika beef zito na msanii diamond kutokana na kile kuwa msanii huyo alikuwa ni team alikiba kwa kuwa alikuwa akipost na kumsapoti alikiba huku akiweka vijembe vya kumkandia Diamond Platinumz.Hii inaongeza na kuwafariji mashabiki pale wasanii wanapokuwa wanapendana na kuungana ili kufanya kazi pamoja kwa sababu hii inaleta hamasa ya mashabiki kuzidi kuwapenda ,ashabiki.

Nay Wa Mitego Kumlipisha Diamond Fidia

Ikiwa bado anaendelea na kesi yake ya kutakiwa kulipa fidia kwa wasanii wakongwe nchini  wa band ya Msondo Ngoma baada ya kutumia ala yao ya sauti  Saxophone na kuweka katika wimbo wao wa Zilipendwa, hivi karibuni tena Diamond ametoa wimbo mpya ambao pia umekuwa na vionjo vya wimbo wa Ney wa Mitego unaojulikana kama makuzi ambao Diamond ametoa akimshirikisha msanii mkubwa Dunianai Rick Ross.

anaemiliki muziki huo wa makuzi ney wa mitego   anaweza kuwashitaki wasafi kwa kutumia kionjo hicho cha muziki wake bila kuwa na ruhusa yake.uongozi wa free nation ambapo ndio anapofanyia kazi ney wa mitego wana haki ya kudai fidia baada ya msanii huyo kutumia baadhi ya sehemu za wimbo wao katika wimbo mpya wa diamond.

Hata hivyo uongozi wa Free Nation chini ya Ney wa Mitego amesema kuwa wameamua kuwapa muda Wasafi na kujifikiria nini kufanya kabla  hawajaamua kuwapeleka mahakamani.

Hata hivyo meneja wa Diamond ,Babutale amejibu tuhuma hizo na  kusema kuwa wako tayari kukaa mezani na viongozi wa Free Nation ili kulizungumzia swala hilo hata hivyo meneja huyo alionekana kujiamini na kusema kuwa siku zote anaedaiwa huwa ni tajiri huwezi ukakuta maskini anadaiwa hata siku moja.

kumekuwa na malalamiko mengi kwa wasanii wa Tanzania kuibiwa baadhi ya maneno, mashairi au vionjo vya nyimbo zao bila kunufaika na nyiimbo hizo, Free nation hawatakuwa watu wa kwanza kutoa malalamiko , wapo wasanii wengi amabo wamekuwa na malalamiko ya aina hii.

Hamisa Atupilia Mbali Kesi Ya Madai Kwa Diamond.

Baada ya kesi ya mwanadada mrembo aliyefanya vizuri katika video mbalimbali nchini za wasanii  wengi Hamisa Mobeto kuhusu madai ya malezi ya mtoto wake kwa kiume kwa baba wa mtoto huyo Diamond Platinumz kuonekana kuwa ilikosewa kufunguliwa na kutakiwa kurudiwa kufunguliwa upya, inasemekana kuwa kesi hiyo imefutwa kabisa baada ya mwanadada huyo kusema kuwa ameona ni bora atupilie mbali kesi hiyo na kuamua kupatana na baba wa mtoto.

Wawili hao ambao wamebahatika kupata mtoto mmoja kwa muda mrefu walikuwa wakionekana hawako vizuri katika mitandao ya kijamii na kuwa wanajibizana lakini hivi karibuni mwanadada huyo amesema kuwa haikuwa na maana ya kuendelea kupigana na kesi hiyo mahakamani kwa sababu wameshakubaliana na mzazi mwenzie.

Kampuni ya GPL walipomtafuta hamisa kuthibitisha kauli hiyo alisema kuwa ni kweli kesi hiyo imefutwa na wapo vizuri na baba wa mtoto wake.

Kwanza sitaki kuzungumzia hizo habari kabisa,lakini ujue tu kuwa hakuna kesi yoyote inayoendelea na tuko vizuri na baba wa mtoto.

Hamisa alifungua kesi hiyo kumshitaki Diamond ambae alikuwa akisema katika media kuwa alikuwa akimpa Hamisa ela ya matunzo ya mtoto ilhali kwa anavyosema yeye kuwa sio kweli, hivyo Hamisa alifungua kesi hiyo ili kuwa anapewa haki ya mtoto wake kupitia sheria za mahakama.hata hivyo watu wengi waliamua kuwashauri wawili hao kuweza kukaa na kutafakari swala la kwenda mahakani ni kubwa kuliko wakikaa pamoja na kuongea kama familia.

Swali kubwa kwa mashabiki linakuwa je kama wawili hao wamepata au kukubaliana kuhusu malezi ya mtoto , inakuwaje kwa mzazi mwenzie na Diamond, yaani Zari ambae alikuwa katika vita kubwa na Hamisa katika kumtetea mumewe.

Alichokisema Meneja wa Harmonize Kuhusu Kolabo Ya Diamond na Omarion

Kwa muda mfupi sana kumekuwa na mafanikio yanayoendelea kupishana na kuongezeka kwa msanii Diamond Platinumz ambae anafanya vizuri sana katika kazi zake, Diamond ambae hivi karibuni amefululiza kutoa nyimbo nyingi na  zote zimekuwa zikifanya vizuri sana.Hivi karibuni Diamond alipokea tuzo kutoka Universal  Afrika baada ya wimbo wake wa Marry You  kufikisha views millioni 17 kwenye Vevo akaunti yake, na kupewa tuzo ya heshima iliyojulikana 6x Platnumz Award.

Katika mtandao wa instagram kumesamba picha zilizomuonyesha Diamond akiwa na msanii mwingine mkubwa kutokea bara la Ulaya, Omarion, msanii ambae alishawahi kufanya kazi zake na wasanii wengine wakubwa duniani kama kina Chris Brown. Picha hizo zinaonyesha jwasanii hao wapo katika moja ya location kwa ajili ya nyimbo mpya.

Ricardo Momo ambae ni meneja wa msanii Harmonize ambae pia ni msanii kutoka lebel ya Wasafi ameandika maneno mazuri ya kumpongeza lakini pia kumtia moyo ‘Piga ndinga Simba Tanzania yote inakubali na inatambua mchango wako kwenye muziki usione wanaokutukana kama hawakupendi vile..hapana sasa  jua kuanzia leo hawa watu wanakupenda  kuliko hata tulio karibu yako ila kutokana na hali ngumu ya mjomba Magu wanaona bora watumie njia ya kukupinga japo inauma kumpinga unaempenda ilimradi waongeze followers ili wapige matangazi kwa maana wewe ndie msanii unaeongoza kwa like na comments nyingi kwa yoyote atakaepost .sasa ulitaka wamtusi nani kama sio wewe mtoa ajira mitandaoni..#ABoyFromTandale ” Aliandika Ricardo katika akaunti yake ya instagram

Diamond amekuwa msanii mkubwa na anaeongoza sasa Tanzania kwa kufanya nyimbo na wasanii wengi wa nje, lengo lake ni kutangaza muziki wake na muziki wa Tanzania nje na mipaka ya Afrika.Diamond ni moja ya wasanii waloingia katika game kwa muda  mfupi lakini ameonyesha juhudi na jitihada kubwa ya kitu anachokifanya, anachokifanya Diamond ni zaidi ya kazi lakini pia anapenda kile anachokifanya kwa faidia yake na faida ya Taifa pia.

Kolabo anayoifanya sasa na omarion itakuwa ni moja ya kolabo nyingi anazoendelea kufanya ambapo hivi karibuni tena ilioonekana akifanya na Rick Ross.