Mange Ameanika Ukweli Wote Kuhusu Bifu la Diamond, Ruge na Kusaga

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni mwanadada Mange Kimambi ameibuka na bomu jipya was huku safari hii akifunguka kuhusiana na mambo ambayo yanaendelea kati ya supastaa wa bongo fleva Diamond Platnumz na Wakurugenzi wa Clouds Fm Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.

Wiki iliyopita Diamond na Clouds Fm waliingia katika vita kali ya maneno ambapo meneja wa Diamond, Salaam SK alimtolea maneno mazito Ruge kwa kudai ana njama za kutaka kumuangusha Diamond na kumshusha kimuziki.

Leo Mange amefunguka na kudai kuwa ukweli kuhusu bifu hili unaanzia kuwa msanii Diamond yuko chini ya Ruge akimaanisha kwamba meneja halisi wa Diamond ni Ruge na Babu Tale na Salaam SK ni watu waliowekwa ili kuzuga watu wasijue kuwa Diamond yuko chini ya Clouds Fm.

Lakini pia Mange amefunguka na kudai kuwa sasahivi Clouds kuna matatizo makubwa kwani Joseph Kusaga anataka kuiuza Clouds kwa kuwa anafungua redio yake nyingine:

Joseph Kusaga anataka kuwekeza pesa yake sehemu nyingine na hiyo sehemu ni kwa Diamond kwa sababu basilica Clouds kuna matatizo makubwa, na Ruge amekuwa dizaini anamsumbua Kusaga kuhusu umiliki ukweli ni kwamba hakuna Clouds Fm bila Ruge”.

Lakini pia Mange amefunguka kuhusu umiliki wa mali za Diamond ambazo amedai zinamilikiwa na Joseph Kusaga:

Jamani ni hivi hiyo Wasafi Radio na Wasafi Tv, Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80% na Diamond anamiliki 20%  All the investment ya Wasafi Radio na Wasafi Tv amefanya Joseph Kusaga na pia hiyo Wasafi online 95% inamilikiwa na Kusaga lakini pia Chibu perfume 100% inamilikiwa na Joseph Kusaga na Diamond Karanga 100% inamilikiwa na Johanna Kusaga mke wa Joseph Kusaga”.

Mange amesisitiza kuwa hili bifu linaloendelea hivi sasa kati ya Diamond na Ruge ni kwasababu wanajua kuwa boss mkuu Kusaga yupo upande wa Wasafi na hivyo wakiwchana na Ruge Babu Tale na Salaam watakuwa mameneja wa Diamond full time.

Diamond Amefunguka Kuhusu Mahusiano Yake na Baba Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz ‘ Amefunguka kuhusu uhusiano aliokuwa nao na baba yake mzazi.

Sio siri kuwa Diamond na Baba yake mzazi anayejulikana kwa jina la Mzee Abdul Juma hawa na uhusiano mzuri sana. Mara kwa mara Baba Diamond amekuwa akilalamika kwenye vyombo vya habari kuwa hayupo kwenye maisha ya mwanaye kumaanisha hata wajukuu zake hajawahi kuwaona.

Diamond aliwahi kuwa muwazi na kusema kuwa hajalelewa na Baba yake na kusema Baba yake aliokuwa cha wakati mdogo sana na yeye alilelewa na mama yake. Lakini siyo hayo tu pamoja na Diamond kuonekana supastaa na kuishi maisha fulani ya kifahari ni tofauti na maisha anayoishi baba yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya jana akiwa anatoka mahakamani kufuatia kesi yake na mzazi mwenzake Hamisa, Diamond alisema mambo kama hayo yanaweza kuharibu mahusiano yaliyopo kati ya Baba na mtoto kwani huwezi kujua akikua ataambiwa nini kuhusu Baba yake.

Diamond alifunguka haya kuhusu uhusiano alionao na baba yake kwa hivi sasa:

Nimejifunza kwamba sio kila mtoto ambaye haishi na mama yake au na baba yake basi ana tatizo naye hili suala langu na mwanangu limenifunza kitu kuhusu uhusiano wangu na baba yangu ingawa sasahivi tupo sehemu nzuri nawasiliana naye vizuri na kwenye kusaidia basi namsaidia na nikiwa Sina uwezo basi namwambia sina uwezo lakini kwa bahati mbaya hatukubahatika kuwa na mahusiano ya karibu kama nilivyo na mama yangu na hiyo inaniwia ugumu kwa sababu sijamzoea kihivyo ndio maana hunioni naye kila sehemu kama mama yangu”.

Lakini pia Diamond amewaomba waandishi wa habari waache tabia ya kuchonganisha familia yake na kuongelea kitendo cha mwandishi kumpeleka baba yake nje ya geti la nyumba yake na kuandika kuwa Diamond kakataa kumfungulia mlango baba yake kitendo alichosema hakipendezi hata kidogo.

Ray C Amkingia Kifua Diamond Platinumz.

Msanii wa muziki wa bongo fleva alikuwa amepotea kwa muda mrefu lakini sasa amerudi katika game Rehema Chalamila maarufu kama Ray c, amefunguka na kusema amekuwa akisikitishwa sana na watu wanaokuwa wanamuandama sana msanii mwenzake Diamond Platinumz.

Ray C anasema kuwa watu bwanamuongelea diamond vibaya na kuacha kuangalia mazuri na makubwa aliyoyafanya katika muziki wa tanzania kwa kuwakomboa na kuukomboa muziki huo.ray c anasema kuwa kama mtu ana macho hana haja ya kuambiwa ni  kiyu gani daimond  amefanya kukuza na kuuboresha muziki wa tanzania zaidi ya kumpongeza na kumfanya apate moyo wa kuendelea kufanya.

Ray c anawaomba  wanaomsema Diamond vibaya kuiga mfano kutoka Nigeria jinsi watu wa huko wanavyofanya kusapotiana kimuziki ili ukue.

ninaumiaga sana ninapoona  watu wanamuongelea vibaya huyu mtoto,amfanya mapinduzi makubwa sana huyo mtoto.kama una macho unaona kabisa .muziki wa tanzania sas ahivi  unafika mbali sana sababu ya watu kama hawa.Nigeria  wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana  lakini sijui kwa nini tanzania tunapenda kuzodoana,kushushana,kuchukiana, dah yaaani huyo alieanzisha social media mungu na amlaani.

Kwa kipindi hiki kifupi Diamond amekumbwa na mambo mengi na maneno mengi katika mitandao yanayomsema vibaya ambapo baadhi ya wachambuzi wakuwa wa habari na muziki pia wamekuwa wakisema kuwa mambo hayo yanaweza kumshusha au kumuangusha kabisa Diamond kimuziki, ukianza familia, mapenzi na hata mashabiki wamekuwa mstari wa mbele kumshambulia Diamond kimuziki.

 

Eric Shigongo: Diamond Asipoangalia Atapotezwa na Mameneja Wake

Mkurugenzi mtendaji wa Global Publishers na Mjasiriamali Eric James Shigongo amefunguka kuhusu supastaa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai kuwa pamoja na kipaji chake lakini anaweza akaja kupotezwa na uongozi wake.

Shigongo aliyejipatia umaarufu kwa kichapisha vitabu na magazeti amekiri kuwa anavutiwa na Diamond kwa sababu anaona kama wote wana historia sawa ambapo wote wametokea kwenye familia au maisha ya hali duni ambapo amekiri amekua katika maisha magumu maana mama yake alikuwa anauza vitumbua lakini amekuja kujikwamua na kujitengenezea maisha mazuri kama Diamond.

Shigongo alifunguka hayo kwenye barua ya wazi aliyomuandikia kwenye mtandao wa Instagram siku za nyuma kidogo, ambapo aliandika:

Nampenda Diamond sana tena sana (sina uhakika kama analijua hili)  I am too proud of him ni fighter (mpiganaji) kutoka Tandale mpaka Beverly Hills with Neyo kwenye video ya wimbo wa Marry you ambao nimetoka kuuangalia    Kwenye YouTube hakika sio kitu kidogo.

Nafahamu kwa sababu niameanzia chini sana kimaisha, Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania.  Bila elimu kubwa bila connection bila fedha, ameweza kuvuta vizingiti vyote hadi kufika hapo alipo leo hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. Bravo!

Lakini nina machache ya kusema naomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi kama kaka na Mtanzania mwenzake niseme huko anakoelekea kuna shimo asiporuka atatumbukia na huo utakuwa mwisho wake. 

Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu nao ni Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam Sk. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti”.

 

 

Meneja Wa Diamond Ahaidi ‘Kumuanika’ Ruge Endapo Atamuandama Tena Diamond

Sakata linaendelea kupamba mtoto kati ya meneja wa Diamond Platnumz Salaam SK na timu nzima ya WCB dhidi ya Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media.

Kizazaa hiki kilianza wiki iliyopita kutoka kwa vijana watangazaji wa kipindi cha Shilawadu Qwisa na Soudy Brown ambao walidai kuwa wamepewa kichapo cha hali ya juu na mcheza shoo wa WCB Mose Iyobo.

Ambapo inasemekana kuwa walimfata Aunty Ezekiel ofisini kwa kwake kwenda kumfanyia mahojiano kuhusiana na suala la ugomvi wao na Tunda lakini kwa bahati mbaya hawakumkuta lakini badala yake walimkuta Mose Iyobo ambapo walidai baada ya kumuuliza maswali mawili matatu aliwageuzia kichapo na kuuanza kuwapiga na kutaka kuwagonga na gari hali iliyowasababishia majeraha.

Tangu siku hiyo kumekuwa na maneno mengi yanayoongelewa mtandaoni lakini hali ilikuwa inaonekana kama si shwari kati ya WCB na Clouds ambapo jana walitoleana povu zito ambapo Meneja wa Diamond anayejulikana kama Salaam Sk amedai kuwa kuna njama zinapangwa ili kumshusha Diamond kimuziki.

Diamond Platnumz na Uongozi Wake

Sallam Sk alifunguka na kudai kuwa Shilawadu hawakupigwa na Mose Iyobo kama walivyodai bali walimtumia Mose ili kumharibia Diamond kwenye jamii na timu nzima ya WCB hivyo akadai kuwa atamuanika Ruge na maovu yake yote ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Kwa heshima ya bwana Joe Kusaga kukuombea msamaha leo Bwana Ruge Mutahaba naamua kukusitiri ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi ntayaanika maovu yako yote unayofanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds media group ila huyu Ruge ndio mwenye matatizo #tumekataakuwakaa”.

Mpaka sasa sio Ruge wala Clouds waliotoa tamko lao rasmi kuhusu sakata hilo lakini kuna habari za chini chini zinazodai kuwa hii yote ni kiki tu iliyopangwa.

Mama Diamond: Mtoto Wa Hamisa ni Mjukuu Wangu Pia

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mama Diamond au Bi. Sandra amefunguka kwa mara ya kwanza na kukiri kuwa mtoto wa Hamisa aliyezaa na Diamond pia ni mjukuu wake.

Mwaka jana mwishoni Diamond alizua kizaazaa cha mwaka baada ya kuenda redioni na kukiri kuwa amezaa na Hamisa ambaye pia alikiri kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi kwa miaka zaidi ya tisa huku siku zote akiwa msichana wake wa pembeni wakati yupo kwenye mahusiano na mpenzi wake Zari pia aliendelea kuchepuka naye.

Lakini hata baada ya sakata hilo Zari alimsamehe baba watoto wake na wakaendelea na mahusiano yao na hapo ndipo familia ya Diamond ilipoongeza ukaribu na Zari na kumtupia mbali Hamisa na mtoto wake.

Kwa muda mrefu kumekuwa na maswali mengi juu ya sababu inayopelekea mpaka familia ya Diamond kutoweka ukaribu na mtoto wa Hamisa anayeitwa Prince Dully au Dylan kama ilivyokuwa kwa watoto wengine wa Diamond Princess Tiffah na Prince Nillan aliozaa na mpenzi wake Zari.

Lakini hivi karibuni Diamond karudi tena kwenye headlines za mitandaoni huku akiwa na skendo mpya tofauti tofauti huku safari hii ikionekana Zari ameshindwa kuzivumilia kwani aliwaunfollow familia nzima ya Diamond akiwemo shoga yake namba moja Mama Diamond.

Baada ya sakata hilo na Zari hatimaye Mama Diamond amekiri kuwa Dylan mtoto wa Hamisa naye ni mjukuu wake hii ilitokea kwenye Instagram aliporusha picha ya mjukuu wake Nillan kuna shabiki akamuuliza “Uwe unamposti hata Dylan kwani naye si mjukuu wake?”. Baada ya kubandikwa swali hilo Mama Diamond akamjibu “Usijali ntamposti yule ni mjukuu wangu hivyo lazima nyamposti tu”.

 

“Nililala na Diamond Lakini Alinisakizia Kwa Dancer Wake”- Mia

Mwanamuziki mkali wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta ndani ya skendo nyingine baada ya msichana mrembo anayeitwa Mia kukiri kuwa alilala na Diamond Nyumbani kwake Madale.

Wiki chache zilizopita Diamond alikamata headlines zote kwenye mitandao ya kijamii baada ya msichana aliyetambulika kwa jina la Mia kuonekana amejirekodi ndani ya nyumba ya Diamond huko kwake Madale.

Baada ya kusambaa kwa ile video mara moja taarifa zilienea kuwa msichana huyo alikuwa ni mchepuko wa Diamond na alikuwa ameenda Madale kwa Diamond jambo lililozua tafrani hata Zari kumrushia dongo na kusema madale pamekuwa Guest house.

Lakini tetesi hizo zilizimwa siku inayofuata baada ya timu ya Diamond kusambaza picha na video zilizokuwa zinamuonyesha msichana yule akiwa Madale Nyumbani kwa Diamond lakini safari hii alionekana akiwa amekumbatiana na Bajuni ambaye ni mmoja Kati ya mcheza shoo wa Diamond hivyo ilidaiwa kuwa Mia alikuwa ana uhusiano na Bajuni na sio Diamond kama ilivyodaiwa awali.

Wiki chache kupita baada ya sakata hilo kutokea mrembo Mia amefunguka na kueleza ukweli wote ambapo amedai kuwa habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli kwani yeye alienda Madale kumfuta Diamond.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Shilawadu ya Clouds TV, Mia amefunguka na kusema alipigiwa Simu na Diamond aende Madame ilikuwa mida ya saa nne usiku alifika akalala naye mpaka asubuhi kesho yake asubuhi alichukua Simu yake akajirekodi video akiwa anatembea tembea nyumbani kwa Diamond.

Kupitia kamera zilizokuwa mule ndani Diamond alimuona akijirekodi akaichukua Simu yake kwa lazima akaanza kuisachi akaifuta kila kitu kilichokuwepo picha zote mpaka video.

Baada ya hapo Diamond akawaita Bajuni na Harmonize wakamlazimisha aanze kupiga picha na Bajuni ili ionekane kama ni wapenzi ili baadaye Diamond aje aseme alienda Madale kwa Bajuni sio kwake.

Mia aliongea kwa uchungu akidai amezalilishwa na Diamond na watu wote wamejua kuwa yeye anatembea na Bajuni wakati alikuwa hajawahi hata kumuona hapo kabla wakati aliyeenda kumfuata Madale ni mwenyewe Diamond.

“Nikifa Leo Mwanangu Asinizike Wala Asiguse Jeneza Langu”- Baba Diamond

Baba mzazi wa msanii wa Bongo fleva, Diamond Platnumz pamoja na dada yake staa mkongwe wa Bongo fleva anayejulikana kama Mzee Abdul Juma, ameibuka na kudai kuwa endapo akifa hata leo kesho basi mtoto wake asimzike wala asiguse jeneza lake.

Baba Diamond amekuwa hana uhusiano mzuri na watoto wake wote wawili yaani Diamond na Queen Darlene mara kwa mara amekuwa akuongea na vyombo vya habari kuhusuatatizo aliyonayo kwenye familia yake.

Hivi karibuni Queen Darlene alifanya mahojiano na kituo kimoja na katika maongezi yake kuhusu wifi yake Zari, alimuingiza baba yake mzazi Mzee Abdul ambapo alisema:

Zari ni wifi mzuri kwangu ana roho nzuri na ndiye mtu pekee aliyekuwa ananishauri kumjali baba yangu, japo baba mwenyewe kuumwa kwake kumekuwa kama mtoto kwa kweli kwa sasa siwezi kusema baba yangu ni Abdul baba yangu ni Naseeb”.

Baada ya mzee Abdul kusikia kuhusiana na maneno aliyoongea binti yake alikasirishwa na kumwambia kuwa endapo akifa basi Queen Darlene asiguse jeneza lake wala hata asithubutu kumzika kwenye mahojiano na Global TV alifunguka yafuatayo:

Nimeumia sana kwani Queen Darlene yeye ni nani hata kunyanyuka na kusema maneno kama hayo kanichukulia mimi kama mtoto hata kama ni dharau sio hivyo kaka yake mwenyewe ambaye ametoka kimuziki na anafanya vizuri hata kama ananidharau hajawahi kunitamkia maneno kama hayo iweje leo hii Queen Darlene anitamkie maneno kama haya Queen Darlene ni binti yangu ambaye nimekaa naye kwa muda mrefu sana na mara nyingi amekuwa akija hapa nyumbani tunapika tunakula lakini leo hii inakuaje baada ya kutoka kimuziki anaanza kutoka kimuziki anaanza kunidharau mimi nimeumia sana sasa na mimi niseme nikifa hata leo na yeye asije kabisa assogelee jeneza langu wala asinizike yeye si kasema baba yake Naseeb basi na mimi sio baba yake “.

 

Babu Tale Ametoa Sababu Iliyopelekea Diamond Kuzomewa Kwenye Tuzo

Meneja wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuelezea sababu iliyopelekea mpaka Diamond kuzomewa kwenye tuzo.

Mwishoni mwa mwaka 2017 Diamond Platnumz alichaguliwa kushiriki tuzo za Soundcity Music Awards ambapo alikuwa anashindana kwenye kipengele cha The best Male MVP of the year 2017 ambayo alishinda na kuwabwaga wasanii wakubwa wa Nigeria kama Davido na Wizkid pamoja na wengineo.

Lakini cha ajabu baada ya Diamond kutangazwa mshindi watu waliokuwa ukumbini hapo waliishia kumzomea vibaya mno na jambo lililoashiria kuwa hawakufurahishwa na  ushindi huo lakibi pia Wanigeria walipiga sana vita ushindi huo wa Diamond mtandaoni.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online Babu Tale ameeleza sababu kubwa zilizopelekea Diamond kuzomewa:

Unajua zile ni tuzo za Nigeria na walikuwa sio tu wanazomea bali walikuwa wanamzungumzia mtu wao ambaye walitaka ashinde lakini aliyefanya vizuri ni Diamond kwa sababu mashabiki zake walimpigia kura name unajua kwanini Wanigeria wao walipiga kelele? Kwanza wenyewe wako wengi Alafu wanakuwa wanajiona wao kama ndio wanaendesha mziki Wa Africa alafu huyu anatokea Tanzania sehemu ambayo ina watu wachache Lakini mwisho wa siku ni wivu kwao kuona kwanini tuzo haikai kwao imeondoka imekuja kwetu”.

 

Hakuna Msanii Wa Kumshusha Diamond Labda Afe- Baba Levo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mwanasiasa, Baba Levo amefunguka na kumrusha msanii mwenzie wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai kuwa hakuna msanii yoyote anayeweza kumshusha labda afe.

Baba Levo ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwanga mkoani Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo amemtukuza mkali huyo baada ya kuhaidi na kumpa zawadi Shilole ya kumtangazia bidhaa yake ya shishi chilli.

Siku chache zilizopita kwenye harusi ya Shilole na Uchebe iliyofanyika maeneo ya Mikocheni, Baba Levo ndiye alikuwa Mshehereshaji / Mc. Baada ya Diamond kumtaka Shilole kuchagua zawadi Baba Levo alivutiwa nakumwagia sifa kibao msanii huyo.

Kwenye maneno hayo na sofa hizo alizomwagia Diamond haya ni baadhi ya maneno aliyoyaongea:

Diamond Platnumz amehaidi kusapoti biashara yenu ya kuuza chilli nchi nzima na nje ya Tanzania jamani mimi naomba nimshukuru sana Diamond na hii ndio sofa kubwa ya watoto wa Kigoma na hii tafsiri yake ni kwamba huyu Diamond ni mkarimu kwani amekubali kukutangazia bidhaa yako bure buree na Shilole usingeweza kumlipa mama huyu ndio supastaa wa nchi alishashindikana tumejaribu wee sasa tumenyosha mikono acha atutangulie siku akifa na sisi tutapanda pale juu alipo kumzidi Diamond hatuwezi labda tumsubirie afe”.

 

Ali Kiba Aibuka Kidedea Tena Amgaragaza Diamond na Wasanii Wengine Kibao

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Ali Kiba ameibuka kidedea kwa kutajwa kama msanii mwenyewe ushawishi mkubwa Tanzania.

Tuzo hizo zinazojulikana kama 100 Most Influential Youth zilizoandaliwa na Advance Media organization zilitangazwa rasmi mwaka Jana na mastaa kibao walitajwa kuwania tuzo hizo.

Baadhi ya Mastaa walioshindanishwa katika tuzo hizo ni pamoja na Alikiba, Jokate, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Idris Sultan, Faraja Nyalandu, Nancy Sumari, Dina Marios, Millard Ayo na wengineo wengi.

Siku ya Jana ilitangazwa rasmi kuwa Ali Kiba amembwaga hasimu wake namba moja Diamond baada ya kutajwa kuwa ndio msanii mwenye ushawishi Mkubwa sana na kupewa medani ya sanaa na burudani katika tuzo za advance media 2017/2018.

Matokeo ya kura zilizokuwa zikipigwa za 50 Most Influential Tanzanians (vijana 50 wenye Ushawishi zaidi) yametoka na katika kipengele cha burudani (Entertainment) Mshindi ni Ali Kiba huku akimshinda hasimu wake Mkubwa Diamond ambaye yeye amechukua nafasi ya pili , akifuatiwanam Wema Sepetu aliyechukua nafasi ya tatu huku nafasi ya nne imechukuliwa na mchekeshaji Joti na nafasi ya tano imechukuliwa na Vanessa mdee huku Jokate Mwegelo akichukua nafasi ya sita .

Baada ya ushindi huo Ali Kiba alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika salamu zake za shukrani kwa mashabiki zake baada ya kumpigia kura:

 

Thank you for voting for me to become the most influential Young Tanzanian in Entertainment Industry Nawashukuru sana #Kingkiba”.

 

 

WCB Wazidi Kurushiana Mpira Skendo ya Mjengo, Babu Tale Afunguka Kuununua Kwa Bilioni 1

Kundi na moja kati ya label kubwa ya mziki nchini ya WCB inayoongozwa na mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz imezidi kujikuta kwenye maji ya moto kuhusiana na skendo inayowazunguka hivi sasa ya nyumba.

Wiki iliyopita Diamond alitangaza kuwa amenunua mjumba kwa bilioni 1 ambayo itatumika kama makao makuu ya label yao ya Wasafi Classic Co. Lakini pia ndio makao ya stesheni mpya ya redio na TV zinazotarajiwa kufunguliwa na Diamond hivi karibuni.

Lakini utata ulikuja jitokeza pale ambapo habari zilitoka na kudai kuwa in fact mjengo ule hawakuununua kwa bilioni 1 bali waliupangisha kwani mmiliki wa mjengo huo yupo jela kwa sasa.

Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond amefunguka na kudai kuwa mjengo ule hawajaununua kama taarifa zilivyosambaa lakini pia hawapo tayari kulizungumzia jambo hilo kwa madai kuwa wanangojea muongozo kutoka BASATA.

Hatujanunua nyumba, tungesema kama tumenunua ila hatujawa tayari kuongea lolote muda ukifika tutaongea kwa sababu sisi tupo chini ya BASATA hatuwezi kuongea bila wazazi wetu BASATA kuwepo kwaiyo tunasubiri BASATA wakiwa tayari tutaita media ofisini kwetu”.

Suala hili zima la nyumba hii limechanganywa zaidi na madalali walioshughulikia Nyumbani hiyo kwani dalali aliyesimamia Nyumbani hii anayejulikana kama Scober au dalali mwanamke amedai kuwa Diamond alinunua mjengo huo kwa shilingi Bilioni moja lakini pia alidai ufunguzi rasmi wa men go huo utakuwa February 2 jambo ambalo Babu Tale amelipangua kwa kudai “Aliyekwambia February 2 ni nani ni mimi ni fela ni nani? Scober anaongoza WCB? Unataka kumsikiliza Scober unanisikiliza Mimi, hatuko tayari kuzungumza”.

Diamond Atangaza Nia Yake ya Kununua Mjengo Mwingine Nchini Rwanda

Mwanamuziki machachari wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kudai kuwa ana mpango Mkubwa wa kununua mjengo mpya nchini Rwanda.

Diamond ambaye wiki iliyopita tu alitawala vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa amenunua mjengo mpya maeneo ya Mbezi beach, Africana ambao utatumika kama makao makuu ya Label yake ya Wasafu Classic lakini poa ndipo stesheni yake mpya ya redio na televisheni vitakuwepo.

Lakini taarifa hiyo ya kununua mjengo huo wa gharama uliingia doa baada ya taarifa kusambaa mtandaoni kuwa jumba lile walilodai wamenunua sio kweli bali kilichotokea ni kwamba Diamond na time yake nzima ya Wasafi wamekodisha jengo lile na in fact anayemiliki mjengo ule kabinti kadogo ka miaka kumi na moja.

Ikiwa hatawiki haijapita tangu sakata hilo lianze Diamond ameonekana kutokujali maneno ya watu kwani Jana ametangaza tena Kuwa ana mpango wa kununua men go mpya lakini safari hii sio nxhini Tanzania bali anavuka boda na kwenda kuangalia mjengo nchini Rwanda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond alitangaza taarifa hiyo na kuandika maneno yafuatayo:

I am looking for a properly to buy in Kigali, my future new home for the Simbas! My Rwandese fam any ideas..? Ningependa kuwa na kakibanda Kigali, Rwanda maana ni moja ya nchi niipendayo…hivyo ningefurahi kuwa na moja ya makazi..eti ndugu zangu wa Rwanda ni maeneo gani yanaweza kunifaa?”.

According to dalali wa Diamond nchini amedai kuwa Diamond ana jumla ta mijengo 29 nchini hapa na pia ana jumba nchini South Africa analoishi na mpenzi wake Zari.

Mange Atoboa Siri ya Nyumba ya Diamond Adai Sio Yake

Mwanaharakati wa siasa Mange Kimambi amerudi tena kwenye headlines kwa mara nyingine safari hii amemuumbua msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai nyumba alyotangaza kuimiliki jana siyo yake bali amepangisha tu.

Siku ya jana Diamond alitangaza kupitia ukurasa wake kwamba amenunua nyumba ambayo itatumika kama makao makuu ya WCB na itatumika kama studio mpya za redio na television station mpya anayotaka kufungua hivi karibuni.

Baada ya kitrnd sana na watu kumsifia kununua mjengo huo wa kifahari unaoelekea kuwa wa thamani kubwa sana Mange ameibuka na kuweka wazi kuwa jumba lile sio la Diamond bali linamilikiwa na mrembo anayeitwa Resty ambaye ni mfanyabiashara maarufu Instagram.

                            Diamond Akiwa na Wamiliki wa Jumba hilo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alifunguka yafuatayo kuhusiana na mjengo huo:

Hii ndio siri ya mjengo mpya wa Wasafi, ile nyumbani ni ya baby daddy wake na Resty anaitwa John huyo John yuko jela kwa sasa. Hiyo nyumba alimjengea huyo mwanaye aliyezaa na Resty, huyo Hailey (Huyo mtoto hapo juu) Nyumba ilijengwa miaka mitano iliyopita na hakuna mtu ambaye amewahi kuishi hapo toka imejengwa ipo maeneo ya Shoppers Plaza ya Mbezi beach karibia na kanisani. Wasafi wameipangisha na pesa za kodi zinatmika kumsomesha huyo mtoto kwa sababu nyumba ipo kwa jina la huyo mtoto… Bababke mtoto yupo jela kwaiyo wakaona nyumba ipangishwe ili kodi imsaidie mtoto. Unaambiwa hiyo nyumba ni matata ngazi zipo gold plated ni balaa tupu! Lakini hata kupangisha ni maendeleo pia sio kila mtu anaweza kupangisha hiyo nyumba, hongera Wasafi”.

Mpaka hivi sasa sio Diamond wala Wasafi hakuna aliyejibu tuhuma hizo za kupangisha nyumba kisha kuupotosha uma kwa kudai kuwa imenunuliwa kwani hata dalali wa hiyo nyumba amefanya mahojiano na vituo mbali mbali na kudai kuwa nyumba imenunuliwa.

Diamond Amepanga Kufanya Mapinduzi Haya Kwenye Sekta ya Burudani Kwa Mwaka 2017

Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz ameweka wazi rasmi mpango wake wa kuteka kabisa sekta ya burudani kwa mwaka 2018 kwa kufungua kituo chake cha redio na TV.

Mara ya kwanza meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alidokeza taarifa hiyo mwezi uliopita alipokuwa anasherehekea sherehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa ambapo baada ya ujumbe wake alidokeza ‘New radio and TV coming soon’.

Diamond alipokuwa nchini Kenye kwa ajili ya kufanya shoo wiki iliyopita alikaa chini na kupiha stori na kituo cha televisheni cha K24 katika kipindi cha K24 Alfajiri ambapo alitangaza rasmi kuwa anatimiza lengo lake la siku nyingi la kufungua kituo chake cha redio na TV.

Kufungua kituo cha redio na televisheni kutasaidia kuutangaza zaidi mziki wake lakini pia biashara zake nyingi kwani kama tunavyojua Diamond ni moja kati ya was a nice wachache ambao ni wajasiriamali kuanzia kuwa na Chibu perfume, Diamond Karanga lakini pia ana kampuni yake ya Wasafi Classic Co. ambayo inasimamia kazi zake lakini pia kazi za wasanii wengine wengi Kama Rayvanny, Harmonize, Queen Darleen, Mbosso, Lava lava, Rich Mavoko.

Baba Diamond Amtaka Bi. Sandrah Aache Kumpiga Hamisa Vijembe

Baba mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma amemjia juu mzazi mwenzake mama Diamond ‘Bi.Sanura’ kuacha vijembe vyake mara moja anavyompiga Hamisa Mobetto.

Tangu Diamond azae na Hamisa na aweke wazi kabisa kuwa hawezi kumuacha mzazi mwenzake Zari kumekuwa na bifu kali ambalo limekuwepo kati ya Hamisa na Zari kwa muda mrefu sasa lakini wiki iliyopita walimalizia hasira zao mtandaoni kwani kila mmoja alimrushia mwenzake maneno mazito mtandaoni.

Katika kipindi chote hiki Mama Diamond amekuwa akionyesha waziwazi kuwa yupo upande wa Zari na huwa mara kwa mara hupendelea kumpiga vijembe Hamisa wazi wazi.

Baba Diamond amemchana Mama Diamond na kumtaka kuwa na busara na aache kuchagua upande mmoja ambao anaunga mkono kupitia Instagram:

Namwambia Mama Esma awe na busara yeye ni mzazi tabia yake ya kuchagua upande na kuendeleza vijembe siyo nzuri kwani anajua Wazi kabisa kuwa mtoto wa Mobetto ni wetu kabisa siyo vizuri yeye kama mzazi angewashauri nina uhakika wangemsikiliza lakini nashangaa ameamua kuchagua upande mmoja wa Zari”.

Lakini pia Baba Diamond amewatolea povu Zari na Hamisa kwa kitendo chao cha kurushiana maneno ya kejeli mtandaoni na kudai wanaibisha wao kama wazazi badala yake amewataka Zari na Hamisa wakae kimya na kila mmoja afanye mambo yake na yeyote atakayeanza kunyamaza huyo ndio atakuwa mke wa kuoa.