“Hakuna Mwanamke Aliyeniliza Kama Wema”- Diamond

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz anazidi kutengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii Ikiwa albamu yake ya ‘A boy From Tandale’ Ikiwa sokoni kwa hivi sasa.

Diamond amefunguka na kueleza ya moyoni mwake ambapo amekiri kuwa hakuna mwanamke ambaye alikuwa kumliza kwenye mapenzi kama Wema.

Diamond amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya nchini Kenya na Citizen Radio na Willy .M. Tuva, ambapo amedai Wema ni mwanamke ambaye alimtambulisha sana machozi.

Mara ya mwisho kulia kwa sababu ya mapenzi ni nilivyokuwa na uhusiano na Wema Sepetu dah yule mwanamke ameniliza sana hadi nakumbuka kuna siku nilikuwa pale home nipo gym babu Tale akawa ameona kuna maambo mabaya mabaya mtandaoni akaniambia mdogo wangu si uachane naye? Mi nakumbuka nikamwambia yaani sikudanyi bosi yule mwanamke nikiwa naye najisikia kama niko peponi  kwaiyo hata tulivoachana alikuwa haamini”.

Lakini pia Diamond amesisitiza kuwa ni kweli amemwaga na Zari na wala sio kiki kama watu wengi wanavyodai ila amesema kwa sasa hataki kumuongelea Zari kwani ameelekeza nguvu zake kwenye kuitangaza albamu yake iliyotoka siku chache zilizopita.

 

Familia Ya Diamond Imecharuka Baada Ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani

Familia ya msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, inadaiwa kuja juu na kutofurahishwa na kitendo cha Zari kuwapeleka watoto wao kanisani.

Zari na Diamond waliachana mwezi uliopita lakini katika Mahusiano yao walifanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Latiffah na Nillan ambao wanaishi na kama yao Africa ya kusini.

Habari zilizoifikia gazeti la Amani zimedai kuwa siku chache baada ya Zari kuonekana akiwapeleka watoto wake wote kanisani siku ya Jumapili kimewacharua familia ya Diamond ambao ni way mini wa dini ya kiislamu hivyo moja kwa moja wanataka watoto wao wafuate dini yao.

Gazeti la Amani linaripoti kuwa mwanafamilia mmoja  wa familia ya Diamond ambaye aliomba jina lake lisiandikee gazetini amesema kama familia wamekasirikishwa na suala hilo kwani walijua labda wataenda mara moja tu lakini imekuwa kila jumapili:

Awali Zari alipotupia picha ya kwanza ikionesha ameenda kanisani na watoto, tuliona labda ni maombi ya mara moja na pengine haiwezi kuwa tatizo lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, tunaona amekomaa na kanisani sasa tunaona kama inaweza kuja kuwa tatizo hapo baadaye na watoto wakawa njia panda.

Si unajua wale watoto ni waislamu kwa sababu siku zote watoto huwa wanafuata kwa baba, sasa baadaye watakaporudi kwa Diamond na wakawa wameshazoea kwenda kanisani itakuwaje?” 

Baada ya kupewa taarifa hiyo gazeti hilo lili Fanta jitihada ya kumtafuta Diamond na Mama Diamond ambao wote hawakupatikana lakini walipomsaka Baba Diamond Abdul Juma aliweka wazi kuwa kama familia hawajafurahishwa na kitendo cha Zari kuwafundisha kuhusu mafundisho ya Kikristo pekee.

Hatukatai dini ni dini tu lakini kilichotushtua ni kwa nini tunaona anawapeleka upande mmoja tu.
Unajua hata kama yeye ameamua kurudi kwenye Ukristo lakini watoto anapaswa kuzungumza na mwenzake ili waamue pamoja”.

Baba Diamond alimalizia kwa kutoa msimamo mkali kuwa, kama familia watamsisitiza Diamond azungumze na mzazi mwenzake na waangalie uwezekano wa kuwapeleka watoto hao madrasa ili pia waifahamu dini ya baba yao.

Albamu Ya Diamond Mbaya Kama Sura Yangu – Harmorapa

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka na kuiponda Albamu ya Diamond na kudai ni mbaya kama ilivyo sura yake.

Harmorapa alijipatia umaarufu kwa kupenda kiki katika maswali kadhaa kuliko muziki wake na leo ameibuka na jipya kuhusu Albamu mpya msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Albamu ya Diamond inayoitwa ‘A boy from Tandale’ imetoka rasmi jana usiku ambapo ilifanyiwa uzinduzi rasmi nchini Kenya.

Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameinanga Albamu ya Diamond na kudai ameitangaza sana alafu ametoa kitu kibovu:

Bro Chibu naye kelele nyingi za Albamu miezi saba mwisho wa siku anatutolea albamu mbovu kama sura yangu sokwe, cha kukushauri Simba kama mkataba wako wa karanga umeisha kaa dukani kwa dada yako Esma umsaidie kuuza vitenge”.

Lakini Harmorapa amejitamba na kudai kuwa albamu yake ambayo atakuja kuitoa itakayoitwa Uthigawepathi itakuwa kali kuliko hiyo lakini pia amesema albamu ya Ali Kiba itafunika kupita maelezo.

Diamond: Media Zinazokataa Kupiga Nyimbo Zangu Zinapotea

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa chombo chochote cha habari ambacho kinaibania WCB kwa njia yoyote basi kitapotea kwani yeye ni kama maji usipokunywa utayaoga.

Diamond amekuwa mmoja wa wasanii ambaye amekuwa na migogoro na media mbali mbali ambapo siku za hivi karibuni Kumekuwa na sintofahamu kati yake na mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba.

Hii imekuja baada ya Diamond kutangaza kuanzisha stesheni zake za redio na Tv ambazo ni Wasafi Radio na Tv ambavyo amesisitiza vitacheza nafasi kubwa katika kukuza mziki wake na hata wasanii kutoka WCB kwa ujumla.

Diamond hivi sasa yuko nchini Kenya, Nairobi ambako ameenda kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ ambayo inategemewa kuanza kuuzwa hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Diamond amefunguka kuhusu albamu yake ambayo ndani yake kuna nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii kadhaa ikiwemo Rick Ross, Neyo na Omarion.

Lakini pia Diamond amefunguka kuhusu Wasafi Tv na Redio ambavyo vinategemea kuanza kuruka hewani siku za hivi karibuni lakini Diamond ameshangaa media zinazotaka kubania mziki wake kwani yeye ndio burudani yenyewe kwaiyo wao kumzuia yeye wanapotea:

Yaani mimi nimejiwekea mazingira ambayo hata nikilala chumbani lazima utaniongelea huwezi kulala bila kunitaja aidha utawataja watoto wangu, au wasanii wa WCB au hata wapenzi wangu yaani Diamond ni kama Azam vile au mimi kama maji aidha utaninywa au utanioga yaani utajua mwenyewe lakini mimi huwezi kulala bila kunitaja kwaiyo media zinazozuia kazi zangu wanapoteza muda maana mimi ndio burudani na mzalisha burudani”.

 

Diamond na WCB Wamuegemea RC Makonda

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label maarufu ya WCB, Diamond Platnumz na timu yake nzima imefunguka na kusema inamtegemea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kusimamia suala la nyimbo kufungwa.

Siku chache zilizopita Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza rasmi kuwa jumla ya nyimbo 13 za wasanii mbali mbali zimefungiwa akiwemo Diamond ambaye alifungiwa nyimbo zake mbili ambazo ni Halelujah na Waka waka.

Tangu taarifa zisambae kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefungiwa Kumekuwa na hisia hasi juu ya suala hilo na sio ndani tu ya Tanzania bali hata kwa mashabiki walio nje ya Tanzania.

Lakini tangu sakata hilo litokee Diamond hajaongelea chochote kuhusiana na ishu hii lakini uongozi wake meneja wake Salaam Sk amefunguka na kusema hawawezi kuongelea suala hilo ila kama kuna mtu ana maswali juu ya hilo akaongee na malezi wao RC Makonda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Salaam SK aliandika ujumbe huu juu ya ishu hiyo:

Habari za muda huu waungwana, Tumepigiwa simu na waandishi wa habari kila kona kuhusu nyimbo mbili za Diamond zilizofungiwa, nimeona kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama WCB tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa Paul Makonda ambaye ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana kwaiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka ameziridhia yeye binafsi zitoke, kwaiyo sioni sababu ya nyimbo ya halelujah na wakawaka kufungiwa kama inavyosemekana  maana sisi hatujapata barua ya nyimbo hizo kufungiwa na kama zimefungiwa mlezi wetu ataongea zaidi”.

 

 

“Mimi na Diamond ni Marafiki Hakuna Kingine Kinachoendelea”- Wema

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amesisitiza na kusema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Diamond zaidi ya urafiki na ukaribu wa kawaida.

Tetesi za wawili hawa kurudiana ziliibuka mwezi uliopita baada ya Wema kuibuka kwenye moja ya party za WCB na kuanza kukumbatiana na Diamond kimahaba kabisa na ishu hii ilizidi kupamba moto baada ya Zari kukiri kumuacha Diamond kisa kumkumbatia Wema.

Diamond na Wema Enzi za mapenzi yao

Tangu sakata hilo Diamond ameshakataa tuhuma hizo na kusema yeye na Wema ni marafiki tu hawana uhusiano mwingine wowote na Wema pia ameibuka na kuthibitisha hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Wema alifunguka na kusisitiza kuwa yeye na Diamond wamebaki kuwa marafiki wa karibu tu:

Mimi na Diamond ni marafiki ni marafiki wazuri, nadhani kinachowafanya wengi washangae ni kwa sababu mimi na yeye tulikuwa hatuongei kwa muda mrefu tangia tulivyoachana lakini sahivi tumeamua kukua na we decided to just put all those things behind us na maisha yaendelee kwaiyo hakuna cha kushangaza mimi kuongea naye au akinikaribisha kwenye party za WCB lakini kilichowashangaza ni mimi kuenda kwenye partu akaja kunisalimia mimi and Diamond we did not kiss nilimhug I hug my friends”.

Wema ameendelea kusisitiza kuwa yeye na Diamond ni marafiki tu hakuna cha zaidi na mambo aliyofanya na Diamond pale anaweza kufanya na mtu mwingine yoyote ambaye ni rafiki wa kawaida.

Mimi Mars Amefungukia Mahusiano Yake na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Mimi Mars aliye chini ya Mdee Music anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘papara’ amefunguka na kueleza uhusiano alionao na supastaa wa mziki wa Bongo fleva, Diamond Platnumz.

Kumekuwa na taarifa nyingi ambazo zimedai kuwa Mimi Mars ametoka kimapenzi na msanii Diamond Platnumz.

Mimi Mars amekataa kata kata habari hiyo na kuiita ya uongo kwani anajua kwa nini watu walizusha jambo hilo ambapo amedai kuwa kuna video ilisambaa mtandaoni akicheza wimbo wa Diamond baada ya kuona vile wao wakazua yao.

Kwenye Interview aliyofanya na Times Fm kupitia kipindi chao cha The Playlist Mimi mars amefunguka haya zaidi juu ya tuhuma hizo:

Taarifa hizo hazina ukweli kabisa kwanza cha kushangaza wakati nacheza huo wimbo hata sikujua kuwa ni Diamond, nilikuwa nimeenda kwa fundi akawa ameweka mziki akasema hebu cheza kidogo so I was just dancing kwaiyo hakuna ishu yoyote mbaya”.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee anafanya vizuri kwenye gemu na sio kuimba tu lakini pia Mimi ana kipaji cha utangazaji Mc kitu ambacho watu wengi hawakijui.

Diamond: Hakuna Ushindani Kati ya Wasafi Tv & Radio na Vituo Vingine

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kuweka wazi kuwa kituo chake cha Wasafi Tv na Radio habilitation kwa ajili ya kushindana na vituo vingine.

Tangu ijulikane kuwa Diamond ana mpango wa kufungua Tv na radio station yake kumekuwa na maneno mengi yanasemwa hasa kwa sababu ya kauli ambazo Diamond ameshawahi kuzitoa kuhusiana na vyombo vya habari kutokuwa na umuhimu kwenye kazi zake.

Lakini pia kumekuwa na drama nyingi ambazo zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii hasa wiki chache zilizopita bifu lililotokea kati ya Meneja wa Diamond na Ruge kitu kilichopelekea habari kusambaa kuwa Diamond ana bifu na Clouds fm.

Wiki hii Diamond alitangaza kuanza shughuli za kutafuta watangazaji kwa ajili ya kufungua Wasafi Tv na Fm ambapo yeye na timu yake walisafiri mpaka visiwani Zanzibar kwa ajili ya kusaka vipaji.

Akiwa Zanzibar Diamond alifunguka na kusema kuwa Vituo hivyo ni kwa ajili ya kukuza mziki na kuondoa matabaka miongoni mwa wasanii:

Ninaomba watu waelewe kabisa chombo hiki hakipo kwa ajili ya kushindana na kitu chochote au na chombo chochote”.

Siku ya jana visiwani Zanzibar Waziri Mwakyembe alitoa rasmi hati ya   usajili wa WAsafi Tv na Radio.

Diamond Alia na Vijana Kwenye Suala la Ukosefu Wa Ajira

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kueleza machungu yake kwa vijana wote ambao wanatafuta ajira kwa hivi sasa ambapo amedai kuwa aingawa angependa kuwapa ajira vijana wengi kwenye Wasafi Tv lakini kwa sasa ni ngumu.

Sio siri Tnzania kama ilivyo nchi yoyote ya Africa swala la ajira kwa kweli ni tatizo na janga hivyo kumepelekea vijana wengi kumaliza masomo yao ya elimu ya juu lakini huishia kujikuta hawana ajira.

Diamond anategemewa kufungua televisheni stesheni yake hivi karibuni na tangia mapema alitangaza kuwa atapita kutafuta vijana watangazaji ambao wataonyesha umahiri wa hali ya juu, kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika haya kwa viajna:

Laiti nigelikuwa na uwezo ningemuwezesha kila kijana mwenzangu aliye mtaani aweze kupata kazi lakini uwezo huo sina lakini kwa nafasi ndogo niliyonayo najitahidi kadri yauwezo wangu kila nipatapo fursa niweze kuitumia vyema niweze kuitumia na wenzangu nikiwa kama mwanamuzi niliyepiga hatua fulani ninaamini nina deni kubwa kwa Watanzania…Hiyo ndio sababu kubwa ya mimi kufunga chombo hiki cha Wasafi Tv nikiamini kesho na keshokutwa kitakuwa mchango wangu kwa Watanzania ambacho kitaongeza wanahabari, watangazaji na wahitimu wa vyuo mbali mbali m”.

 

Zamaradi Mketema Kuoneka Mubashara Ndani ya Wasafi Tv

Muigizaji mkongwe Zamaradi Mketema amethibitishwa kuanza kuonekana live kama mtangazaji katika redio station na televisheni station mpya ya Wasafi Tv and Radio inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz.

Suala hili Limekuja baada ya ukimya mrefu aliokuwa nao Zamaradi Kwenye anga ya utangazaji. Mara baada ya Zamaradi kumuacha aliyekuwa mpenzi wake na Baba watoto wake mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na kuolewa na mwanaume mwingine mwaka jana Zamaradi aliacha kazi Clouds Fm pia.

Mapema mwaka huu kuna tetesi zilisambaa kuwa Zamaradi atajiunga kwenye redio mpya ya Diamond lakini zilikuwa ni tetesi tu lakini mpaka jana usiku tunaweza kuthibitisha kuwa ni taarifa za kweli kabisa na mpaka hivi sasa Zamaradi yupo na timu nzima ya WCB.

Hamornize alithibitisha taarifa hizi kwa kuweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram na kusindikizwa na ujumbe wa kumkaribisha Zamaradi ndani ya Wasafi Tv:

Let’s go Mama Juju welcome to th Family Wasafi Tv”.

Zamaradi na Diamond Pamoja na timu nzima ya WCB wapo visiwani Zanzibar kwa ajili kufanya zoezi la kusaka vipaji vipya vya watangazaji ambao watafanya kazi katika kituo hicho kipya cha Wasafi tv.

 

Diamond Awapa Ujumbe Huu Watoto Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameendelea kukaa kwenye headlines za mitandao ya kijamii tena kwa siku ya leo baada ya kumpost mtoto wake aliyezaa na Hamisa.

Tangu Diamond Akiri kuzaa na Hamisa miezi michache iliyopita Kumekuwa na sintofahamu kwenye familia yake kwani watu mbali mbali wamekuwa wakimlaumu kwa kupendelea watoto wake wawili aliozaa na Zari na kumtelekeza mtoto aliyezaa Na Hamisa.

Siku ya leo Diamond kamuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram mtoto wake aliyezaa na Hamisa anayeitwa Dylan lakini pia kamuweka na Nillan aliyezaa na Zari na kuwaandikia ujumbe huu:

Pamoja na uzuri mlioenda kurithi kutoka kwa mama zenu halafu mkaenda kuniletea wakwe vijuso….dah mtanisikitisha sana…”.

 

Lakini ni pia siku ya jana familia ya Diamond ilionekana ikimposti Dylan tangu azaliwe ambapo dada wa Diamond, Esma Platnumz alimuweka Dylan na watoto wake pamoja na watoto wa Zari:

Ney wa Mitego Amefunguka Baada Kumtabiria Diamond Kushuka Kimuziki

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Ney wa Mitego amefunguka na kuongelea jambo ambalo lilimfanya atengeneze headlines kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo kuhusu Diamond kushuka kimuziki.

Ney wa Mitego alishangaza watu wengi alipoanza kumponda Diamond ukitegemea wamekuwa marafiki kwa kipindi kirefu na hata wamefanya mziki kwa pamoja ambapo amemshirikisha kwenye nyimbo yake iliyofanya vizuri sana miaka ya nyuma ‘Muziki gani’.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa Instagram, Ney aliweka picha ya mnyama simba akionekana akiuwawa kikatili jambo lilitafsiriwa kuwa yule ni Diamond kutokana na tayari inajulikana jina jingine la Diamond ni Simba akimaanisha yeye ni mfalme wa mwituni.

Kwa kuweka picha ya Simba akiuwawa ilisemekana kuwa au ilitfsiriwa kuwa Ney wa Mitego alikuwa anatabiri Diamond kushuka kimuziki. Kwenye mahojiano aliyofanya Times Fm katika kipindi cha The playlist Ney amesema hakukusudia jambo lolote baya ama hakua na nia mbaya dhidi ya Diamond kwa sababu ni mshkaji wake.

Diamond ni mshkaji wangu tumefanya kazi kubwa sidhani kama imefika hatua ya sisi kuwa maadui kiasi hicho na siwezi kumuombea mabaya kiasi hicho lakini tunaona changamoto anazopitia. Nilijua tu ile picha wabongo kila mmoja ataongea la kwake lakini sina tatizo na Diamond lakini hata kama lipo basi tutalimaliza lakini ile picha ilikuwa haimuhusu”.

 

Diamond Atangaza Ziara Mpya Nchini Marekani

Msanii maarufu wa Bongo fleva ambaye pia ni president wa label ya WCB, Diamond Platnumz amezidi kuonyesha upande wake wa mafanikio katika mziki wa Bongo fleva.

Pamoja na kwamba skendo zimekuwa zikimzunguka sana siku hizi chache Diamond hajazipa nafasi ya kumfanya aache kufanya anachokifanya zaidi ambacho nacho ni kutoa burudani kwa mashabiki zake.

Diamond yuko mbioni kutoa Album yake inayosubiriwa kwa hamu kubwa kabisa inayoenda kwa jina la ‘A boy from Tandale’ mapema mwezi ujauzito lakini pia mapema ametangaza baada ya albamu hiyo kutoka atakuwa anafanya ziara yake nchini Marekani kwa ajili ya kuitangaza zaidi.

 

Ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond alitangaza ujio wa tour hiyo ambayo ataenda kutumbuiza kwenye majimbo zaidi ya 12 kama vile New York m, Dallas, Houston, Los Angeles, Minnesota na mengineyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika:

Kuelekea kuachiwa rasmi kwa albamu yangu ya ‘A boy from Tandale’ ndugu zangu mlio Marekani mjiandae kwa ziara ya A boy from Tandale USA tour”.

 

Hii Ndio ‘Michepuko’ Iliyomfanya Mpaka Diamond Akatoswa na Zari

Habari za Diamond na Zari kuachana bado zinatawala kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakiwa wameshtushwa kusikia kuwa couple iliyokuwa inapendwa na mashabiki zao imevinjika.

Huku sababu ya Zari kumwaga Diamond ikiwa ni wazi kabisa kuwa ni michepuko ambapo Zari ameweka wazi sababu juu iliyomfanya mpaka akafikia uamuzi wa kumuacha Baba watoto wake ni yeye kuzidisha kuchepuka.

Kwenye mahusiano yao yote kumekuwa na tetesi za Diamond kuwa na mahusiano na wanawake wengine ingawa mara nyingi amekuwa akikataa na kudai ni uzushi lakini pia na Zari amekuwa akimsamehe na wawili hao huishia kurudiana.

Baadhi ya michepuko ambayo inasemekana kuchangia kuvunja uhusiano wa Diamond na Zari ni hawa hapa:

1. Hamisa Mobetto 

Hamisa anatajwa kuharibu uhusiano wa Diamond na Zari tangu mwaka jana alipojitokeza na kukiri kuzaa naye kuanzia hapo mahusiano ya Diamond na Zari ikaanza kuyumba ingawa alimsamehe lakini bado kulikuwa kuna mpasuko tayari.

2. Irene / Officiallyn

Irene na Diamond wametajwa kuwa na mahusiano kwa muda mrefu sana tangu alipotokea kwenye video ya kwetu ya Rayvanny kama video queen kumekuwa na tetesi kuwa walikuwa wote South Africa at the same time akiwa na Zari na familia.

3. Shady

Huyu ni mwanamitindo kutoka nchini Rwanda tetesi za Diamond kutoka na Shady zilianza kusikika alitoa za kusafiri na kuelekea nchini Rwanda lakini zilipamba moto alipoenda Rwanda mwezi uliopita baada ya picha wakiwa pamoja kusambaa mtandaoni.

4. Mia

Mwezi uliopita kuna video ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Mia akiwa Madale ambapo baadae ilikuja kuonekana kuwa alienda pale na dancer wa Diamond ambaye alikuwa na mahusiano naye jambo ambalo Mia alikuja kulikana na kusema alienda pale na Diamond ambaye aliishia kulala naye.

5. Tunda

Uhusiano wa Tunda na Diamond ulikamata sana headlines ambapo inasemekana amekuwa mchepuko wake wa siku nyingi sana video iliyowaonyesha wakiwa pamoja ilisambaa mwezi uliopita tu.

6. Wema Sepetu

Wema na Diamond walitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kuonekana wakikumbatiana na kubusiana hadharani kwenye party huku kukiwa kuna tetesi kuwa wamerudiana.

Diamond Akiri Kuwa Bado Hajajua Atakuwa na Nani ‘Valentines Day’

Mwanamuziki wa Bongo fleva na mmiliki wa label ya WCB, Diamond Platnumz amefunguka na kukiri kuwa bado hajajua mipango yake ya Valentine’s Day imekaaje mpaka hivi sasa.

Ikiwa siku ya Wapendanao ‘Valentines Day’ ili njiani inakuja siku ya kesho tarehe Kumi na nne ambayo ni siku maalumu kwa wale wapendanao ikiwa ni sherehe inayosheherekewa dunia nzima.

Diamond ambaye ametengeneza headlines kila kona kwa wiki hizi chache zilizopita ambapo kila mwanamke anasemekana katoka naye kuanzia Mia aliyesambaza video clip akiwa Madale, mpaka kwa Wema aliyeonekana akipeana mabusu hadharani mpaka kwa Tunda ambaye amesemekana ana ujauzito wake lakini yupo Zari.

Zari ndio mwanamke pekee ambaye Diamond amemkubali kuwa anaweza kusheherekea naye sikukuu ya wapendanao siku ya kesho.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online Diamond alifunguka na kusema kuwa hajajua atasherekea nani mpaka hivi sasa labda atajua ikifika siku yenyewe:

Sasa itategemea Valentines yenyewe itanikutia wapi kama itanikutia South Africa kwa mzazi mwenzangu basi atakuwa yeye lakini pia kama itanikutia hapa Tanzania basi Valentines wangu watakuwa ndugu zangu na marafiki zangu”.

Lakini pia Diamond ameendelea kuwasihi Watanzania wampokee Mbosso vizuri na wampe sapoti yao yote.

“Diamond Sio Mmiliki wa Diamond Karanga, Chibu Perfume Wala Wasafi Tv/ Radio”- Mange

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, mrembo Mange Kimambi ameibuka tena na kumnyooshea kidole staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai yeye ni balozi tu sio mmiliki wa mali hizo.

Tangu siku za nyuma kuna habari zimekuwa zikienea kuwa Diamond sio mmiliki halali wa Diamond karanga na hata ilidaiwa kuwa karanga hizo zilikuwa zinaitwa Diamond karanga kabla hata ya kushikiliwa na Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika haya:

Hizi karanga zinaitwa Diamond karanga miaka na miaka, wamebadilisha rangi ya paketi na kurembesha ila jina la Diamond karanga ni la miaka yote ila zinatengenezwa na kampuni ile ile ya smart. Kilichotokea ni kwamba Joseph Kusaga alinunua ubia kwenye hicho kiwanda halafu akamleta Diamond aje amfanyie promotion na ndio maana wenye karanga zao baada ya tifu wametoa siri kuwa Diamond ni balozi wao tu”.

Lakini Mange hakuishia hapo pia amedai kuwa mali nyingine tunazozitambua kama za Diamond si zake ambazo ni perfume yake inayoitwa Chibu Perfume na pia vituo vya redio na televisheni anavyotegemea kuvizindua hivi karibuni vya Wasafi Tv na Radio ambapo Mange pia amesema;

Lakini pia Wasafi Radio na Wasafi Tv Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80 na Diamond anamiliki 20% ikimaanisha kuwa uwekezaji wote wa Wasafi Radio na Tv umefanywa na Joseph Kusaga. Lakini pia Wasafi Online ambayo wasanii wanatumia kuuza nyimbo zao 95% inamilikiwa na Kusaga. Chibu Perfume 100% inamilikiwa na Johainna Kusaga, mke wa Joseph Kusaga”.

Mpaka hivi sasa sio Diamond wala uongozi wake ulioongelea tuhuma hizo nzito zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, ingawa kwa mtazamo wangu hata kama mali zote sio zake na yeye ni balozi tu haina shida ilimradi pesa inaingia kwenye akaunti kilichotakiwa ni kusema ukweli, Je wewe nini maoni yako? Tafadhali andika hapo chini.