Roma aweka wazi kuwa amewasamehea na kuwasahau waliohusika na kutekwa kwani

Roma ambaye ni msanii wa hiphop bongo alitekwa miezi kadhaa iliyopita lakini akapatikana baada ya siku kadhaa kitu ambacho yeye Kama mwanadamu hajaweza kusahau.

Hivi karibuni akizungumza na Times FM, Roma alifunguka kudai kuwa tangu awachiliwe serikali ya Tanzania haikumsaidia kwa njia yoyote. Msanii huyu alisema kuwa familia, marafiki na mashabiki ndio walisimama na yeye hadi kupona kwake. Alipoulizwa ikiwa Serikali ilimjulia hali wala kumshughulikia alijibu kwa kusema,

“Lahashaa! Hapana juu kwa juu tuu polisi, polisi Mwananyamala PF3 sijui nini ile, baada ya pale nikajiongoza mimi mwenyewe na familia yangu,so ikawa hivyo tuu“

Hata hivyo Roma alisema kuwa ameshawasamehe na amewasahau wote waliohusika na kutekwa kwake.

“Yaliyopita yamepita tunasamehe,tunasahau waliohusika Mungu atawahukumu na mkono wake na Mungu atupe neema uvumilivu na neema ya kuwasamehe…Lakini usidanganyike na mtu anakwambia sijui alikuja akatoa bugana lake au sijui akatoa hela ya panadol, Lahashaa!“

Mke wa Roma aeleza alivyozunguka vituo vyote vya polisi kumtafuta mumewe ambaye hajulikani aliko

Mke wa Roma, Nancy amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mumewe, Roma kupotea. Kulingana na stori mitandaoni kuna fununu kuwa Roma na rafiki yake walichukuliwa na polisi wakiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Kama Watanzania wenzake Nancy hafahamu alipo mumewe ambaye ni baba ya mtoto wake, Ivan. Akizungumza na wanahabari, Nancy ameeleza kuwa amemtafuta mume wake katika vituo vya polisi lakini kila andako hakuna anayerecords za Roma Kutiwa mbaroni. Alisema,

Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu jana saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine. Baada ya hapo nikaanza kutafuta watu wa kunisaidia, baadhi ya ndugu zangu wameangaika vituo vyote vya polisi Roma hayupo, hadi sasa hivi sifahamu yuko wapi, kwa ufupi sina ninachokijua wala ninachokifahamu. Jitihada zangu za kutafuta kwenye vituo vyote vya polisi nimemaliza.

Hivi sasa watanzania kwa ujumla wameungana mikono katika jitihada za kumtafuta Roma ambaye mpaka sasa hajulikani aliko.