Gigy Money Yupo Tayari Kuwa Mama- Amber Lulu

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Gigy Money anayeendelea kutamba na ngoma yake ya ‘Nampa papa’ alitangaza ujauzito wake wiki chache zilizopita baada ya kuenda BASATA kuripoti kwa Naibu waziri.

Gigy Money aliingia matatizoni na BASATA kutokana na vituko vyake ambavyo vilijumuisha picha zake za utupu alizokuwa amezoea kupiga lakini pia maneno aliyokuwa anaongea na vyombo vya habari hasa interview aliyofanya na kutaja orodha ya wanaume aliotembea nao.

Gigy Money alificha ujauzito wake na kuufanya siri lakini ulipogundulika ndipo maneno yalipoanza watu wengi wamehoji uwezo wake wa kuwa mama kutokana na historia yake na matendo yake aliyofanya kipindi cha nyuma.

Lakini mbali na mawazo ya watu wengi kuwa Gigu hataweza kuwa mama mzuri kutokana vitabia tabia vyake rafiki yake wa karibu Amber Lulu amefunguka kuwa anadhani Gigy Money yuko tayari kuwa mama bora.

Amber Lulu alifunguka hayo yote kwenye interview aliyofanya na Enews ya East Africa TV:

Kwanza hayo mawazo ya watu sio mazuri kwa sababu binadamu tunabadilika tunakuwa watu wapya kila siku na tunafanya vitu vikubwa, Gigy ambaye wanamuongelea wa 2017 na Gigy tunaemuongelea 2018 naweza sema ni watu sita tofauti  mnavyomuona kwenye social media hiyo inakuwa ni sehemu ya kazi kwaiyo vile mnavyomuona mtandaoni sivyo alivyo kwenye maisha yake halisi Gigy ni mwanamke mmoja tu poa na sahivi typo tayari kuwa mama na ndio maana amefungua sehemu yake ambayo inaweza kumuingizia kipato Kwaiyo ivo yaani tayari ameshakaa tamarind kuwa mama na Mimi namuona kabisa”.

Lakini pia Amber Lulu amefunguka na kudai kuwa endapo na yeye siku moja atakuja kuwa mama hatogopa kwasababu ya vituko alivyofanya kwani anaamini kuwa anataka mtoto wake ajifunze kutokana na makosa yake.

Gigy Money Ajutia Kutaja List ya Mabwana Zake.

Miaka kadha nyuma iliyopita msanii Gigy Money katika kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds Media mtangazaji alikuwa ni Zamaradi Mketema alitaja list ya wanaume aliyowahi kutembea nao na historia yake ya mapenzi kwa ujumla huku akiwa anajinadi kwa kutembea na watu wengi maarufu.Katika list hiyo ambayo Gigy Money aliisema aliwataja wasanii wengi akiwemo Alikiba na mdogo wake Abdul Kiba.

Hivi karibui mwanadada huyo alisema kuwa katika vitendo anavyojutia katika maisha yake ni kuwataja wanaume aliowahi kutembea nao kwa sababu anaona kuwa amejidharirisha sana na anatamani hata siku zirudi nyuma ili aweze kufuta yale aliyokwa ameyasema mwanzo kuhusu wanaume hao.Lakini pia Gigy anasema kuwa kwa sasa inakuwa kama fashion kwa mtu kutaka kujulikana anataja mabwana aliotembea nao wakati yeye hakufanya hivyo ili kupata kiki.

kutajaga watu niliowahi kutembea nao, natamani hata siku zirudi nyma ili niweze kuyafua maneno yangu ili watu wasijue kuwa nilishawahi kutembea na nani na wangapi katika mahusiano yangu.-Alisema Gigy Money.

haikunisumbua kipindi ninaongea lakini sasa hivi ndio naona kama haikuwa na haja , ninaona kama ninawaharibia wengine wanaotoka kwenye fani kwamba akitembea na mtu basi na yeye aje wenye media aseme.watu wameshafanya kama ndio kiki ya kutobolea.

Gigy Money ambae kwa sasa ameshangaza watu wengi kwa kuamua kutulia na kubeba ujauzito wa mja ya ma-dj nchini na kuamua kuzaa anasema kuwa najuta kwa sababu kitu chochote kibaya unachofanya huwa ni ngumu kufutia katika mawazo ya watu na ubaki katika mitandao na hivyo kinaendlea kukuchafua.

Hata hivyo alishawahi kusikika Gigy akisema kuwa maisha yake ya nyuma yalikwa yametawaliwa na utoto hivyo mambo mengi alikuwa akiyafanya kwa sabau alikuwa aajayajua maisha bado.

Gigy Money Amejibu Tuhuma Za Kudanganya Ana Mimba Kubwa Ili Serikali Imuhurumie

Msanii wa Bongo fleva, Gifty ‘Gigy Money’ amefungukia tuhuma zilizomkabili za kudanganya ni mjamzito ili tu aonewe huruma na waziri wa habari Mh. Juliana Shonza.

Wiki iliyopita Waziri Juliana Shonza aliuwasha moto baada ya kuwataka wale wasanii wote wanaovaa mavazi ya utupu kuwasili ofisini kwake na baadhi ya wasanii aliowataja ni Preety Kind, Gigy Money na Sanchoka ambapo Pretty Kind aliishia kufungiwa kufanya mziki na kazi zozote za sanaa kwa muda wa miezi sita.

Baada ya Gigy Money kuwasili Basata siku husika alionekana akiwa ni mjamzito na tumbo lake likiwa ni kubwa tu na mwenyewe alieleza kuwa ana ujauzito wa miezi Saba na alipoulizwa ni kwa nini alifanya siri alidai kuwa aliogopa kutangaza maana angepigwa juju.

Lakini baada ya haabari hiyo ya mimba kusambaa mtandaoni stories mbali mbali zilizuka huku watu wengi walidai kuwa mimba ile ilikuwa ya uongo alivaa matambara tu ili atakapo tinga BASATA wamuonee huruma kumfungia mama mjamzito.

Gigy Money alikiri Kuwa hakukusudia kuwajulisha watu kuwa alikuwa mjamzito kwani isingekuwa waziri Juliana Shonza kumuita basi katu wasingejua kuwa alikuwa mjazito kwani hakuwa na mpango wa kumwambia mtu.

Gigy Money alifunguka haya alipofanya mahojiano na EATV:

Kwanza mumshukuru yule waziri maana msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea tu Bahati mbaya wati wakauona, halafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma Mimi nina undugu na serikali? Halafu kama mtoto anaokotwa subirini wangu nami ntamuokota”.

 

Gigy Money Amefunguka Sababu Iliyompelekea Kuficha Ujauzito Wake Kwa Miezi Saba

Mwanamuziki wa Bongi fleva Gift Gigy Money ambaye bado anafanya vizuri na ngoma yake ya nampa papa amefunguka na kueleza ni kwa nini alificha ujauzito wake kea miezi Saba.

Siku ya jumatatu Gigy Money aliwashangaza wengi alipotinga Basata akiwa na mimba kubwa aliyodai ni miezi Saba huku watu wengi walipigwa na butwaa kwani hakuwahi kuonekana vile kabla a siku ile.

Gigy Money alienda Basata kwenda kuonana na Naibu waziri wa Habari Juliana Shonza baada ya kuitwa kutokana na kilichodaiwa kuwa anakiuka maadili ya kitanzania kwa kuvaa mavazi ya nusu uchi na kuimba nyimbo zisizo na maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahohiano na Millard Ayo TV Gigy Money alitaja sababu za yeye kuficha ujauzito wake kwa miezi Saba:

Watu lazima wajiulize hapo kwanza wananijua kabisa mimi mpenda kiki lakini ujauzito wangu mpaka unafikisha miezi saba hakuna mtu anayejua? Kun mtu anakua ndani yangu kwaiyo kadri ninavyokuwa akili inaongezeka na nyingine inapungua nimepunguza akili ya kukaa utupu sahivi nataka niwe mwenyewe na maisha yangu private siwezi kukataa Kuwa nilikuwa nafanya uchakaramu kwa kweli nilikuwa nafanya nilikuwa napiga kweli lakini sahivi ni mama mtarajiwa nimetulia na aikutaka kutangaza mimba yabgu sana mwenzangu wanga wengi hapa mjini”.

 

Gigy Money:Hakuna Uhuru Tena

Msanii wa nyimbo za bongo fleva nchini Gigy Money ambae pia alianza kwa kujulikana katika tasnia ya sanaa kwa kuwa video vixen, jana aliitikia wito wa kuitwa na ofisi za BASATA  baada ya kuingizwa kwenye list ya wasanii wa kike wanavaa vibaya na kutupia picha za uchi katika mitandao ya kijamii.Gigy Money ambae inasemekana kuwa alipigiwa simu na Naibu Waziri wa habari na michezo  Mh. Juliana Shonza lakini hakujibu simu wala meseji jana aliamua kufika baada ya taarifa za kuitwa kwake kumfikia kupitia vyombo vya habari.

Hata hivyo mwanadada huyo baada ya kutoka katika ofisi za BASATA alionekana mwenye huzuni na kumwaga machozi kutokana na kile alichokutana nacho ndani ya ofisi hizo  japokuwa hajasema moja kwa moja kuhusu nini ameambia kufanya kama adhabu au marekebisho makubwa ya kazi yake lakini bado amepewa maagizo ya kuonana na Naibu Waziri..

Akiendelea kuongea na waandishi wa habari Gigy Money alisema kuwa kwa sasa hakuna tena uhuru kama zama.”Mimi nitaongea na  naibu waziri kama wanavyodai, lakini there is no freedom, hamna freedom  tena, no freedom trust me mtu anakuja na ku-judge pia ya March.”

Lakini pia Gigy Money anasema kuwa BASATA  wamemwamuru kujitambulisha na kujiandikisha kwa sababu amekuwa akifanya vitu bila kuwa na kibali cha kuwa msanii au video vexen kwa kipindi chake chote alichokuwa katika sanaa.

Akiendelea kuongea Gigy Money pia ametoa malalamiko yake na kusema kuwa amehangaika sana kulitengeneza jina laka e na kuna kipindi alikuwa mpaka akilia na kulalamika alipokuwa akilipwa ela ndogo chini ya kiwango cha kazi zake lakini hakuna aliyetokea kumsaidia kwanini sasa hivi watokee na kumhukumu tu.

Kwa kumalizia Gigy Money alisema kuwa kama haki yake ipo na basi itapatikana tu , lakini atafata kama walivyomtaka afanye na ataonana na naibu waziri ili kuitikia wito.

Gigy Money anaingia katika list ya wasichana watatu waliotajwa juzi  na mh juliana shonza kuwa wanongoza kwa kuchapisha picha za uchi katika mitandao yao ya kijamii na kuwa wamekuwa mstari wa mbele kuvunja maadili, ambapo wenzie wawili ni msanii Pretty Kindy na Sanchi.

Gigy Money Akiri Kugandwa na Mpenzi wake.

Mwanamusiki wa bongo fleva Gift Stanford Maarufu Gigy Money adaiwa kugandwa na mpenzi wake anaejulikana kama  Mourad Alpha maarufu kama ‘MO’ ambae wanafanya nae kazi sehemu moja katika kituo kimoja cha radio.Baadhi ya mashabiki na watu wa karibu na gigy money walithibitisha kwa kusema kuwa mwanaume wa gigy money sasa hivi amekuwa akienda na Gigy Money karibu kila sehemu mpaka katika shoo zake amekuwa akimsindikiza hata zile za mikoani.

Moja wa watu wa karibu wa Gigy Money  anasema kuwa wawili hao kabla ya kuachana kwa mara ya mwisho walikuwa wana maisha ya kawaida tu lakini baada ya kurudiana sasa hivi mwanaume huyo amekuwa akimsindikiza Gigy Money  kila sehemu anayokuwa anaendaa katika shoo anazofanya hata kama ni nje ya mkoa.

Mwanadada huyo alipotafutwa kuulizwa kuhusu teteis hizo alikubali kuwa ni kweli sasa hivi mwanaume huyo amekuwa akimganda  kwa watu wamekuwa wakiongea sana kuhusu yeye  hivyo ameona  ni bora achunge mzigo wake.

Unajua watu wamekuwa wakiongea sana kuhusu mimi,ndio maana mwanaume wangu kaona isiwe shida ni bora kila abiria achunge mzigo wake hasa ili watu wakose cha kuongea kabisaa, na ni kweli kuwa hata kwenye shoo huwa anataka kunisindikiza. Alikiri Gigy Money

Hata hivyo kuna tetesi zilizokuwa zikisambaa katika mitandao kuwa penzi la wawili hao limekuwa likizidi kumea kutokana na tetesi kuwa Gigy Money kwa sasa ni mjamzito na mimba ni ya Mo

Gigy Money- Najutia Baadhi Ya Mambo Niliyofanya Ikiwemo Kutaja Listi Ya Wanaume Niliotembea Nao

Video vixen aliyeukia mziki wa Bongo fleva Gigy Money anayefanya vizuri na kibao chake cha Nampa papa amefunguka na kudai kuwa anajutia natendo yote aliyofanya kipindi cha nyuma na anatamani ayafute.

Gigy Money alianza kupata umaarufu wake kutokana na umbo lake lilivyokuwa hasa makalio yake lakini pia mavazi yake anayovaa pia humletea attention fulani lakini vituko vyake ndio vilivyompa umaarufu sana hasa alipofanya mahojiano na Zamaradi Mketema na kuweka wazi kuwa alianza kulala na wanaume alipokuwa na umri wa miaka 16.

Lakini pamoja na hayo yote Gigy ameonyesha kujutia yale yote aliyoyafanya siku za nyuma. Gigy alifunguka na kukiri Kuwait anaamini alichofanya hakikuwa sahihi hivyo kuwataka watu kuyaacha yale mabaya aliyotenda badala yake  kuyaangalia mazuri pia.

Gigy Money alifunguka hayo alipokuwa ana perform kwenye tamasha la Coca cola 5select ambapo aliwasihi wanafunzi wate waangalie na wafuate mazuri aliyofanya na waachane na mabaya:

Najutiaga kutaja listi ya wanaume niliotembea nao yaani natamani nirudi nyuma nifute watu wasijue how many guyz I slept with na kipundi naongea nilikuwa naona sawa kwa sababu niliona bawakomoa wale wanaume panini sasahivi naona kulikuwa hamna haja ya kufanya hivyo so nawashauri wait wachukue mazuri nilofanya kwa mwaka huu mabaya wayaache na haya mambo yote niliokuwa nafanya kwa sababu mimi ndio mzazi wa maisha yangu sina baba na mama yangu ni mshkaji tu ciz nampa hela kwaiyo ni tofauti na wait waliolelewa na baba na mama kwaiyo sahivi nakua najutia Yale niliofanya Latino sahivi nimebadilika”.

 

Gigy Money Awaamkia Wanaotangaza Kuwa Ana Mimba

ingawa mimba huwa ni jambo la kheri lakini inakuwa tofauti kwa baadhi ya wasichana hasa wasanii wa tasnia za sanii nchini, wengi wamekuwa wakikana kuwa na mimba au hata kama wanazo baadae tutaona zinayeyuka na kushindwa kujitetea wapi imekwenda.Kutunza mimba na kutoa mtoto mwenye afya njema na mipango ya Mungu lakini pale inapogundulika kuwa uma mimba swala linalofuata ni kushukuru Mungu na kutulia.

Hivi karibuni msanii gigy money aliweka picha katika mtandao wa instagram ambayo ilionyesha tumbo lake kuwa kubwa na watu kuanza kusema kuwa inawezekana gigy money atakuwa na mimba kutokana na picha hiyo lakini pia kutokana na maneno aliyokuwa ameandika katika posti ile.Hata hivyo Gigy Money aliwajibu baadhi ya mashabiki walihisi kuwa ana mimba na kuwakanushia taarifa hizo.

Akiongea na Star Mix ya GPL ,Gigy Money ambae alikuwa akionekana kweli ameanza kunawiri na kitumbo chake kuanza kuonekana kama mtu mwenye  ujauzito amesema kuwa watu waache kumuandama. Gigy money anasema kuwa yeye kuwa na mimba au kutokuwa na mimba haimuhsu mtu na hata kama ana mimba sio lazima kutangaza na kila mtu kujua swala hilo.

Kama nina mimba au sina mimba haimuhusu mtu, kwa sababu mimba sio kitu cha matangazona kama ninayo tu mtajua kwa maana mimba haifichiki kabisa, kuhusu mwili wangu kuanza kuongezeka ni kweli mara ya kwanza nilikuwa nina stress sana  sasa hivi niko poa sana  ndio maana nimeanza kunenepa. 

Gigy money ambae sasa hivi yupo kwenye mahaba mazito na mtangazaji mwenzie anaejulikana kama DJ Mo inasemekana kuwa kweli walnategemea mtoto ingawa Gigy Money mwenyewe anakanusha taaarifa hizo.

Gigy Money na mpenzi wake

Lulu Diva Amefunguka Kuhusiana Bwana Anayemgombania na Gigy Money

Msanii kike wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa, Lulu diva ameongelea bifu au ugomvi unaosemekana upo baina yake na msanii mwenzake anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Papa’ Gigy Money huku ikidaiwa Kisa kikubwa cha bifu hilo kikiwa ni mwanaume.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva na Gigy Money hawapikiki chungu kimoja hata kwa sekunde moja na hata wakikutana sehemu hawawezi kuzungumza lakini pia inadaiwa Kisa na mkasa ya uhasama huo ni kuwa kuna mwanaume ambaye warembo hao wote wawili wanamtaka kwa wakati mmoja kitu kinacho sababisha mikwaruzano.

Tetesi hizi zilizidi hasa hapa Kati baada ya warembo hao kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii, kwenye mahojiano na East Africa Tv kupitua kipindi cha Enews, Lulu Diva alikana kata kata taarifa hizo na kudai kuwa hana ugomvi na Gigy Money:

Amchukue bwana angu ampeleke wapi labda? Kwanza mi nawashangaa sana mimi sinaga ugomvi na Gigy Money na wala sijawahi kugombania naye bwana labda saa nyingine maneno yanavyo ongelewa inakuwa ni showbiz tu lakini mimi na Gigy Money tunajuana wenyewe ananipenda na mimi ninampenda yaani in short tunapendana na pia tunasapotiana kwenye kazi zetu mimi naimba nyimbo zake na vice versa yaani tupo fresh kabisa halafu isitoshe mwanaume wangu hana time na wait walio kwenye media mimi mwenyewe nimejuana naye kabla sijawa staa yaani Nina uhakika ningekutana naye wakati nimekuwa maarufu asingenitamani”.

 

Gigy Money Amtolea Matusi Mazito Afande Sele

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gigy Money anayetamba na wimbo wake wa ‘Papa’ ameibuka na kumtolea matusi ya nguoni Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Afande Sele.

Siku chache zilizopita Afande Sele alifanya mahojiano na kituo cha redio cha East Africa ambapo aliongelea mmomonyoko wa maadili katika mziki wa Bongo fleva na kudai kuna baadhi ya wasanii wapya ambao wanakuja na kuharibu muonekano wote wa mziki wa Bongo fleva.

Afande Sele aliongeza na kudai kuwa Gigy Money hamfahamu kwa sura na wala hajawahi kumuona machoni lakini anasikia kuwa anapenda kuvaa uchi na kufanya vitendo vya ajabu ambavyo vinapelekea mmonyoko wa maadili.

Gigy Money anaonekana hakufurahishwa na maneno yale kwani kea kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtolea Afande Sele povu zito;

Wasanii wa Zamani naomba mnipumzishe midomoni mwenu maana kwenye kila interview zenu mnanitaja taja tena mnikomee….Mnafikiri mkinitaja mimi indio interview zenu zitamfikia Trump Marekani? new taarifa yenu mnanipa kiki tu kama hamjui alafu makorodan**  yanawaning’inia au madada nyie? Mnikome kabisaa maana akili zangu sio nzuri ntawaharibia wengine badala ya wakate nywele zao eti wanatoa ushauri mxiuuu embu pelekeni bangi zenu maskani hukoo”.

Afande Sele alidai kuwa nyimbo ya Gigy Money inayojulikana Kama ‘papa’ haina maadili na pia msanii mwingine aliyemtaja Kama anaimba nyimbo zenye mmomonyoko wa maadili ni Zaiid anayetamba na wimbo wak unaoitwa ‘Mwanaume mashine’.

Gigy Money Amtaka Rado Kupambana Na Hali Yake

Mwanadada ambae kila siku amekuwa na drama za hapa na pake kutokana na kuwa na skendo zisizoisha katika mitandao amefunguka na kumjibu rado ambae awiki iliyopita alisemakuwa wasanii wa bongo  hawan adili kwa sababu kwa sasa wanajioa wenyewe.

Rado ambae ni msanii wa bongo movie amekuwa akionekana kuwasema vibaya sana wasanii wa kike wa bora na hii haitakuwa mara yake ya kwanza kuwakashifu wasanii wa kike.Hata hivyo Gigy Money alikwazwa na maneno ya msanii mwenzie hivyo kumwambia kuwa yeye ndio hana ela ya kuwaonga wanawake wa bongo kwaio ni bora apambane na hali yake.

Gigy amesemahayo alipokuwa akiongea na Radio East Africa na kusema kuwa mwanaume huyo  apambane na hali yake kwa sababu hana hela ya kuwapata watoto wazuri wa bongo ndio maana anaongea vitu vya ajabu na vya kuwakatisha tamaa watu wengine.

Hata hivyo gGgy Money alimjibu msanii huyo na kumwambia kuwa kwa sasa hivi kuolewa wala hakuna dili sana kama zamani ndio maana wanawake wengi hawaangaiki na kutafuta ndoa.

Wadada wengi wa bongo ni kweli kwa sasa wamekuwa hawaolewi na hata wakiolewa hawadumu katika ndoa zao,Gigy money ameamua kufunguka ukweli kuhusu hisia za wasanii wengine wakike kuhusu swala la kufunga ndoa.

Rado: Wanawake Wa Bongo Fleva ni Wahuni Sana

Muigizaji wa Bongo movie anayetizamiwa kuja kuwa tishio kwenye tasnia hiyo Rado, amefunguka na kudai kuwa wasichana wengi kutoka Bongo fleva hawafai kuolewa na pia tasnia hiyo inaongoza kwa kuzalisha wasichana wahuni na masela.

Rado alifunguka maneno hayo mazito kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi Chao cha Enews ambapo Rado aliwavaa wasanii hao wa like na kudai kuwa wengi wao wamejaa wahuni tu kwenye tasnia hiyo:

Kiufupi tu hakuna mwanamke wa kuoa kwenye Bongo fleva, hakuna sababu yoyote ya sisi wasanii wa bongo movie na bongo fleva kuingiza malumbano yasiyokuwa na msingi lakini ifike wakati Tanzania na wanamuziki wajue brand ya tasnia yoyote ile inatengenezwa kwa kupitia mgongo wa Bongo movie, hawajui kuwa Bongo movie ndio inatengeneza wale models wanaowatumia katika nyimbo zao hata ukiangalia uzalishaji wa wasanii kati ya Bongo movie na Bongo fleva sisi ndio tunazalisha wasanii wengi wa kike kwa mwaka kuliko wao, sasa kama rapa anaitwa Chemical nani atamuoa yule si msela kabisa? Bongo fleva inazalisha masela tu lakini sisi tunazalisha warembo ambao wao wanawatumia kwenye video zao kwaiyo waheshimu tasnia yetu maana wengi wao wanatumia wanawake wetu kupata umaarufu. Msanii wa kike ninayemuona angalau atakuja kuwa msanii mkubwa wa kimataifa ni Gigy Money tu”.

Hivi karibuni kumeibuka mabifu Mengi sana kati ya Bongo movie na bongo fleva ambapo kila upande wanarusha maneno wakifai wao ni bora zaidi.

Gigy Money Agoma Kumuomba Msamaha Mjumbe Baada Ya Kumtukana (Video)

Msanii anayetamba na wimbo wake wa ‘papa’ Gigy Money anayejulikana zaidi kwa vituko vyake vya kila siku aliingia kwenye vichwa vya habari mapema wiki hii baada ya video kusambaa akiwa anagombana na kumtukana mjumbe wa nyumba kumi katika mtaa anaoishi.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo watu walimjia juu na kudai kuwa kumtukana mama mtu mzima kiasi kile ni kukosa adabu kwa sababu yule mama anafaa kuwa mama yake kwani Gigy alimpiga singi, alimuokotea mawe na kutishia kumpiga na matendo mrngine ya dharau. Kwenye mahojiano na East Africa Tv, Mama huyo mjumbe alilalamika kuhusu kutukanwa na Gigy Money;

Yaani Gigy akaanza kunitukana wewe nani na umekujaje hapa? nikamwambia dada mimi ni mjumbe utakapopata tatizo lolote lazima upate barua kutoka kwangu lakini aliendelea kunitukana na kunitishia kuwa baba yake ni polisi”.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa kupitia kipindi cha 5Select, Gigy alipoulizwa kama atamuomba msamaha yule mjumbe mama mtu mzima alifunguka:

Kwanza kabisa sijafikiria kumuomba msamaha na pia kuna watu wanachukulia kuwa ukishakuwa kioo cha jamii kila kitu inabidi utupiwe! hapana yule mama mimi amenikosea sana kwa sababu ameniletea waandishi wa habari nyumbani kwangu hiyo ilikuwa mara ya nne unajua yule mama ana kashfa alafu ana maneno ambayo akikuongelea lazima utapanick kwaiyo pale nilipanick”.

Gigy Money Akiri Mahali Anapokaa Hapamstahili

Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu msanii wa bongo music akutane na kitimbi cha kutukanananna mjumbe wa nyumba kumi  pamoja na mama mwenye nyumba anayoishi ambapo yeye mwenyewe anakiri kuwa aliamua katika nyumba hiyo hivi karibuni na alikuwa mgeni katika mtaa huo.Hata hivyo baada ya video hiyo kusambaa na kuenea katika mitandao watu walianza kuhoji mahali hapo ambapo pameonekana katika video hiyo kwamba ndipo  Gigy Money anasema anakaa hapafanani na hali yake kama msani mkubwa na anaefanya vizuri katika game.

Hata hivyo akiongea na Five Selekt ya EATV, gigy ameamua kugunguka na kusema ukweli na  kukubali kuwa pale ndipo anapokaa kwa sasa lakini ameamua kukaa pale kwa muda kutokana na kipindi kigumu anachopitia sasa kwa sababu kule alipokuwa akikaa mwanzoni pamesombwa na maji baada ya kutokea sakata la mafuriko ambalo liliathiri nyumba nyingi jijini na vitu vyake vyote vimekwenda na maji kwaio ili aweze kujikinga amelazimika kutafuta eneo la bei rahisi ili aweze kujistili kwa muda kwa sababu ndio kama anaanza maisha mapya.

Unajua nimetoka ktika mafuriko, katika nyumba niliokuwa nakaa maji yalijaa na kusomab kila kitu changu hapa nilipo nins stress sana ni mimi mwenyewe tu ndo ninajua.hapa nilipo ninaanza maisha upya kabisa sian kitu hata kimoja.nikaona nitafute nyumba sehemu na nikapata hapa, pale ninapokaa hata sistahili kukaa pale lakini mimi pia ni binadamu ninapitia magumu pia. -Alifunguka Gigy Money

Watu wengi wameshindwa kuamini katika eneo lile kwa sababu kwa jinsi msanii huyo amekuwa akijigamba katika mitandao ya kijamii ni uongo na hauendni na mazingira anayoishi sasa, hata hivyo  Gigy Money amekubali na amesema kuwa kama binadamu matatizo yanaweza kumkuta mtu yeyote hivyo kwa sasa yeye ndio anaanza maisha mapya.

Gigy Akiri Kuishi Kwa Kudanga

Mwanadada asiyeisha vituko katika mitandao ya kijamii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema kuwa jinsi anavyoishi yeye ni tofauti kabisa na vile watu wanavyomchukulia kwa sababu watu wanahisi yeye ana ela sana lakini kumbe maisha yake ni magumu tu na anaishi kwa kudanga  na kufanya badhi ya madili ya mtaani.

Gigy anasema kuwa kwa kifupi jina lake limekaa kipesa pesa ndo maana wengi  wanafikiria kuwa yeye anapesa nyingi sana lakini ukweli ni kwamba wala hayuko hivyo kabisa zaidi ya kupigika kimaisha. Gigy anasema kuwa anachoshangaa ni kwanini watu wamekuwa wakivutiwa sana na jina lake hili.

Jina langu tamu sana,maana yake hata jinsi linavyo-sound  ni jina moja zuri ambalo limekaa kipesa pesa tuu, lakini ajabu pamoja na uzuri wa jina langu hilo  maisha yangu mimi mwenyewe hayafanani kabisa na jina langu, naishi kwa kudanga tu na kufanya madili ya hapa na pale

Gigy Money  alishawahi kukiri kipindi cha nyuma katika chombo kimoja cha habari kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuuza mili kwa wattu mbalimbali ikiwepo vigogo ili kuweza kujimudu kimaisha.

Ukiachana na kuuza sura katika video mbalimbali lakini pia Gigy Money kwa sasa amejiingiza katika kazi ya sanaa na pia ni mtangazaji wa kipindi fulani katika radio moja jijini, mashabiki wamekuwa wakishangazwa na mwanadada huyo ambae amekuwa na vipaji tofauti tofauti lakini bado anakiri kuwa yeye ni mdangaji.

Haitakuwa kauli ya  kwanza kwa Gigy Money kuongelea maisha yake na biashara hiyo ya udangajiLlakini pia hii ni moja ya tabia ya wasichana wengi Tanzania wanojifanya kujiingiza katika muziki huku wakitumua sanaa kama mwamvuli  wa kuwafunika huku nyuma ya pazia wakufanya mambo mabaya kama hayo ya udangaji.

Lakini kwa kuwa Gigy Money amekuwa ni mmoja wa watu waliopewa vipaji vingi ikiwemo hiki cha muziki nadhanisasa anapaswa kuacha kutaka kuishi maisha yasiyo ya kiwango chake na kujikitazaidi katika kazi halali itakayompa ela

 

Gigy Money Bado Anamuwinda Diamond Platinumz

Mwanamuziki kutoka Tanzania asiyeishiwa na matukio kila kukicha Gigy Money  ameibuka na kuongelea jinsi gani anavyotamani kila siku kutoka kimapenzi na msanii mkubwa kutoka bongo Diamond Platinumz.Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha papa ambacho kinafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka bila kuwa na wasiwasi kuhusu hisia zake kwa msaanii huyo mkubwa kutoka Tanzania.

Akihojiwa na moja ya waandishi wa habari , aliulizwa kuhusu ndoto aliokuwa nayo muda mrefu ya kutaka kutoka kimapenzi na Diamond Platinumz, Gigy Money alisema kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakiwindana kwa muda mrefu sana lakini yeye hana wasiwasi anaamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa maana hajui kitu gani mwanamke mwenzie atakosea na yeye akapatia ili kuwa na Diamond lakini anaamini kabisa ipi siku hataweza kutoka na Diamond

iyo ndoto kama chemchem inachemka tu sijui lini mwenzangu,mimi na Diamond tunawindana, tukipishana baadhi ya sehemu tunaambiana tu wewe..wewe , lakini ninachoamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa mambo mazuri hayataki haraka, na inawezekana hata tukadate, you never know wenzie watakosea wapi na wewe utapatia wapi, kila kitu kinawezekana” alifunguka Gigy Money

Gigy Money alishawahi kutangaza katika vyombo vya habari kuwa alikuwa na mahusiano na alikiba na kusema kuwa endapo wameacha lakini huwa wanakutana na kukumbushia mapenzi yake, hata hivyo alipoulizwa tena kuhusu hisia zake kwa msanii alikiba gigy money alisema kuwa kwa alikiba alishapita wala hana ya kurudi tena huko yeye saivi na diaond tu“kwa alikiba tulishapitaga huko, unajua ukipita sehemu kuja kurudi inakuwa  sijui unaonaje ..haaaa unarudiaa, saivi tunaenda mbele kwa mbele  kama ccm

Gigy Money ni moja wa wasichana wanaokwa wazi sana anapokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii, hivi karibuni amekuwa akiongelea sana kutamani kuwa na mahusiano na Diamond Platinumz huku akikana kurudiana na Rich Mavoko. Hata hivyo Gigy Money alikuwa katika mahusiamo na mtangazaji mwenzake wa radio moja wapo hapa nchini  na haijafahamika kama wameshaachana au la.