Gigy Money Azidi Kumchefua Mo Jay

Mwanadada Gigy Money amenaswa katika moja ya video alizokuwa akirekodiwa alipokuwa salon huku akitoa maneno machafu ya kumkshifu mwanaume aliyewahi kuwa nae katika mahusiano na kupata nae mtoto pamoja na kwamba baadae alikuja kutamka kuwa mtoto huyo so wa mo jay kama ilivyokuwa ikijulikana hapo awali.

Katika video hiyo Gigy Money anasema kuwa mwanaume aliyekuwa nae ( Moj ay ) hakuwa na uwezo wa kumtunza kama mwanaume aliyenae sasa hivi na hata alikuwa akishindwa kwenda saloni kwa ajili ya kutengeneza nywele kutokana na umaskini wa mwanaume huyo.

nguvu ya buku imetoa kimasomaso, kuonga mchezo alikuwa haniongi chochote , angeuwa ananionga ningekuwa nashindwa kuja hapa saloni kuweka nywele za millioni tatu.sasa hivi nimempiga chini kule nimepata ela za kuja hapa.

Kuangalia video hiyo bofya hapo katika link..https://www.instagram.com/p/BjHIgKbBnCo/?taken-by=jaymaudaku

 

Gigy Money Aomba Radhi Baada Ya Kumwaga Povu Zito

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameomba radhi baada ya ugomvi wake na Baba mtoto wake Mo J.

Gigy Money alimtolea maneno makali Ex wake ikiwemo kuweka wazi kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo kuwa mtoto wake Myra sio wa Mo J kwani alikuwa na mwanaume mwingine.

Gigy Money na Ex wake Mo J walirushiana maneno makali baada ya Gigy kumtuhumu kiwa hakuwa alimfunza kipindi cha ujauzito na kudai alihama na kila kitu baada ya kuachana.

Baada ya sakata hilo Mo J aliongea na vyombo vya habari na kudai kuwa ana uhakika kuwa mtoto wao ni wa kwake ingawa Gigy kwa ajili ya hasira anampa  mtoto mpenzi wake wa sasa.

Baada ya povu hilo Gigy Money ameibuka na kuomba radhi kwa maneno aliyoongea huku akidai ilikuwa ni hasira ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka ujumbe huu:

Nipo Tayari Kudanga Kumlea Mwanangu:-Gigy Money

Mwanadada  , msanii wa bongo fleva Gigy Money amejikuta akiwatolea povu baadhi ya watu wanaomsema katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuanza kufanya kazi  bila kujali kuwa mtoto wake hajatimiza hata 40 .

Watu katika mitandao wamekuwa wakimshambulia gigy money kwamba alitakiwa akae ndani mpaka pale itakapofika siku 40 ndipo atoke nje na kuanza kumuacha mtoto nyumbani na yeye kufanya kazi zake.haya yote yana kuja baada ya kusambaa kwa habari kwamba Gigy Money ameanza kazi na kuwa balozi wa kampuni moja ya kondom nchini.

Ogopa sana mapenzi ya mama kwa mtoto,yaani mama anaweza kujikuta anafanya lolote kwa ajili ya kesho ya mtoto wake  ata awe chizi hawezi kumtupa mtoto wake , haijalishi wakati ya mimba alipitia mangapi sasa hivi ninawaza kwa jinsi gani nitamtunza na kumlea mtoto wangu.hata kudanga nitadaga tu npo serious mjue na wale ambao mnanitukana  kwanini kipindi hiki ninafanya kazi , eti nimetoka kabla ya 40, naomba niwajibu kiufupi kama mkubwa utaelewa kama mtoto  endelea kunijazia comments za matusi  yaan ni iviii(utamaduni wa mtanzania ni njaaa ukiwa na njaa unaweza kufanya lolte bila kujali , sidhani kama ningekuwa napewa kila kitu ningetoka nje sasa hivi) so usilaumu kitabu kwa sababu nje umeona fuvu ukajua kuwa ni kitabu cha mazombie.

Gigy Money Aukwaa Ubalozi wa Kondomu

Mwanamuziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Gifty Stanford maarufu kama Gigy Money amebahatika kupata dili nono la kuwa balozi wa Kondomu.

Baada ya Amber Lulu kutangaza wiki iliyopita kuwa amekuwa balozi rasmi wa Kondomu hatimaye na Gigy Mahoney amekuwa msanii wa pili kupata dili hilo.

Gigy Money alitangaza habari njema hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

BALOZI WA BULL CONDOM (Jamani sahivi kwichi kwichi zangu zote natumia Kondomu mpaka Myrah akue)”.

Kwa upande wa gigy Money Dili hili limekuja katika wakati muafaka kabisa kwa sababu ndio kwanz amaetoka kujifungua hivyo ni wakati wake wa kusaka pesa.

Gigy Money- Marafiki Zangu Walinishauri Nitoe Mimba

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money aliyejifungua mtoto wake wa kike anayeitwa Myra wiki chache zilizopita amefunguka mambo aliyopitia kipindi cha ujauzito wake ikiwemo kupewa ushauri wa Kuutoa ujauzito huo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Gigy Money amesema kwa kipindi kirefu alikuwa njia panda juu ya ujauzito wake maana ulikuja kipindi kibaya ambacho hakutegemea na hivyo baadhi ya Mashoga zake kumshauri atoe:

Kwangu mimi ilikuwa ngumu kukubali kuzaa na kuwa mama maana ndio wimbo wangu wa papa ndo ulikuwa unahit vibaya mno hadi marafiki zangu wakawa wananiambia hiyo mimba yako bora utoe yaani unazaa mwanangu? Hivyo yaani lakini mimi moyo wangu ulikuwa mzito ningeweza kufa labda”.

Gigy pia amefunguka kuhusu ugomvi wake aliokuwa nao na Baba mtoto wake ambapo aliwahi kumtuhumu kwa kumpiga kipindi cha ujauzito na kumnyanyasa mambo aliyodai yalitokana na hasira zake na wivu wake mwenyewe.

 

Nilipokuwa na Mimba Nilikuwa Mdogo, Ukinichamba Nakuangalia:-Gigy Money

Mwanadada Gigy Money amefanya mahojiano kwa mara ya kwanza tangu alipojifungua ambapo hata siku 40 hazijapita lakini alipata bahati ya kuelezea hali aliyokuwa nayo kipindi yupo mjamzito na baadhi ya magumu aliyokuwa ameyapitia kipindi mjamzito.

Gigy Money anasema kuwa alipojigundua kuwa yeye ni mjazmito ilikuwa na muda wa wiki tatu lakini ilimuia vigumu kukubali kwa sababu alikuwa akiwafikiri mashabiki zake watamwambia nini, lakini pia alikuwa anaona kama mimba ingemfanya kufifia katika muziki kwa sababu kipindi hicho alikuwa ametoa hit song ya nampa papa ambayo ilikuwa ikifanya vizuri.

Gigy Money anaendelea kusimulia na kusema kuwa kikubwa alichofanya ni kwenda kwa mama yake ambae alimwambia kuwa kikubwa anachotakiwa kukiangalia ni kama yupo tayari kupata mtoto bila kujali baba wa mtoto ana nini au hana nini na ndipo alipoona kuwa hana haja ya kuitoa mimba kwa sababu hata ba bawa mtoto pia alikuwa akionyesha kuwa ana hamu ya kupata mtoto.

Kadri miezi ilivyosogea Gigy Money alianza kuumwa sana na kushindwa kula muda mwingi alikuwa ni mtu wa kunywa pombe tu na ndipo alipopata mawazo ya kuitoa mimba lakini alikuwa akisita kutokana na ukweli kuwa mwanaume mwenye mimba alikuwa akionyesha asana kumjali na kuwa nae karibu.

Gigy Money anasema kuwa katika vitu alivyokuwa navyo kipindi yupo mjamizto ni kuwa mpole sana, alikuwa mdogo kiasi kwamba hakuwanauwezo wa kujibishana na mtu yoyote, wengine waliokuwa wakimchamba alikuwa akiwaangalia tu.

Gigy money anamalizia kwa kusema kuwa maumivu ya uchungu wa kuzaa hayawezi kuelezeka zaidi ni kuombeana sana unapoona mwanamke yupo katika hali hiyo.

 

Gigy Money Atangaza Rasmi Hana Rafiki,ni Baada ya Wote Kushindwa Kutokea Alipojifungua

Mwanadada Gigy Money amaetangaza kuwa kwa sasa hana rafiki kwa sababu aliyokuwa akiwategemea kama marafiki zake wameshindwa kujitokeaza hata kumpanepi katika uzazi wake na kusema kuwa wamesahaunkuwa alikuwa akiwasaidia kwa zaidi ya miaka saba mjini lakini leo hii kama vile hawajui kilichotokea kwake.

katika ukurasa wake wa instagram, Gigy Money ameonekana kukerwa na baaadhi y rafiki zake wa kiek waliojifanya kuwa marafiki lakini sasa hivi wanakuwa hawajui kuwa amejifungua , aliandika

“Thanks aunty missa i love you shoga,jamani wengine mnajifanya mashost , twin boo , bae ila nepi tu zinawashinda natangaza rasmi sina shoga mjini hapa ni  washkaji tu byee, #ushoagakazinaujuekujitoa.

Kwa hesabu za haraka haraka marafiki wa karibu wa Gigy money ni pamoja na Amber Lulu pamoja na Tunda ambao walikuwa karibu nae , ingawa madongo haya hayajaweka wazi yamemlenga nai lakini ni marafiki wa karibu wa Gigy money.

 

Gigy Money Ahofia Kupotea Kwenye Gemu Baada Ya Kushika Ujauzito

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kwa Jina la usanii kama Gigy Money aliyetamba na kibao chake cha Nampa papa amehofia kupotezwa katika gemu ya Bongo fleva kipindi hiko ambacho ni mjamzito.

Gigy Money ameibuka baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku hali hiyo Ikiwa imesababishwa na kuwa mjamzito hivyo kukiri kuwa anashindwa kufanya kazi nyingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money ameongelea hofu yake ya kusahaulika kutokana na kuwa kimya na kuandika ujumbe mfupi uliosindikizwa na picha zake mpya:

Hapa mjini nikisema siposti msije mkanisahau bure nipo kiranja wa mashangingi hali ni mbayaaa hali ni teteee”.

 

Celebtities Wanaongoza Kuwa na Maisha Magumu-Gigy Money

Mwanamuziki mwenye jina lake na drama nyingi ambae kwa sasa ametulia sana kutokana na majukumu ya uzazi ,gigy money anasema kuwa mastaa wengi ndio wanaongoza kuwa na njaa na hiyo yote inatokana na kwamba mastaa wengi wanaogopa kufanya kazi na kujipatia kipato ila wanakuwa wanategemea kupewa ela .

Maisha, unajua maisha ni magumu wala tusidanganyane siujui make-up. sijui kope,maisha hayako hivyo ni magumu tu na kuna muda watu wanaongoza kuwa na maisha magumu ni ma-celebrities.na kwa sababu yote hiyo tunaendekeza ustar mbele.mtu unajisemesha eti eeh mimi nikashike sura ya mtu nimrembe, no mimi am a gigy men, na kama nataka kufanya kitu nafanya kwa sababu sitaki kudharirika kabisa.

Gigy anaongezea kuwa katika maisha yake anaona kuwa ni bora kufanya kazi hata kama ni ngumu lakini sio kumpigia mtu simu na kuanza kumuomba ela, hata hivyo anasema kuwa kuna mambo alishawahi kuyafanya na yakamleta manufaa na hiyo inatosha hasa aliyokuwa akiyafanya hapo mwanzo kama kupiga picha za uchi.

Mimi nikakae nimuombe mtu mia au mia tano wakati nina nguvu ninaweza kufanya kazi,ni bora nikakuremba unanilipa elfu 50 au 60 na nikala hata siku tatu.mimi sipendi kudharirika na hakuna mtu anaeogopa kesho yake kama mimi na ndio maana  kuna vitu siwezi kufanya tena kwa sababu nilishafanya vikanifaidisha kwa nini niendelee kufanya.

Gigy money anakiri kuwa kuna baadhi ya mastaa wamekuwa wakipiga picha na kuweka katika mitandao kwa ajili ya kpata kiki na umaarufu tu na wala sio kwamba wanakuwa wana maanisha kile wanachokuwa wanajibu baada ya kitu fulani kutokea.

Niliweza kupiga mapicha ya ajabu na nimeona yamenisaidia kupata fame kirahisi na nilikuja kujua baada ya kuonamtu anakupigia simu anakulipa mtengeneze kiki.

Gigy Money Akiri Kuacha Utoto,Ajiandaa Kuwa Mama Bora.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi Gify Stanford almaarufu kama Gigy Money amefunguka na kusema kuwa anataka kujitahidi kuwa mama bora kwa mtoto anaetarajia kumpokea hivi karibuni hivyo tabia za kitoto zote anaachana nazo kwa sababu huko siko aliko sasa.

Gigy Money amabe kwa sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua siku yoyote amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na  Showbitz extra na kusema kuwa hata yeye anajiona kuwa amebadilika na hii ni kutokana na ukweli kwamba unakuwa mjamzito hatua inayofuata ni kuwa mama na sio kurudi nyuma tena hivyo ili kuwa mama bora ni lazima kukubali hali hiyo na kuachana na mambo ya nyuma.

nimekuwa kwakweli unajua huu ujauzito umenipa funzo la maisha, na sasa naenda kuwa mama na hili niwe mama bora basi ni lazima  na kila kitu sio niendelee  na maisha yale ya kitoto niliyokuwa nikiishii zamani.- Alifunguka Gigy Money

Wikiendi iliyopita Gigy Money alifanya baby shower, sherehe ambayo ufanyiwa mama mjamzito kwa ajili ya kumpa zawadi na kumuandaa kwa ajili ya kujifungua kwake.

Gigy Money- Nitapenda Mwanangu Akifuata Nyendo Zangu

Msanii wa Bongo fleva Gifty Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka na kusema atapenda kama mwanaye atakuja kufunga nyendo zake hapo baadae akiwa mkubwa kwani anaamini kila yeye ni kioo cha jamii.

Gigy Money aliingia kwenye Sanaa kama mtangazaji na video queen lakini kitu kilichompa umaarufu mkubwa ni vituko vyake na kupenda kukaa uchi na kupiga picha za uchi zilizo make headlines.

Baada ya kupata umaarufu huo Gigy aliingia kwenye Sanaa ya kuimba muziki ambapo alipata mafanikio ya mara moja baada ya kutoa wimbo wake ‘Nampa papa’ ambao ulikuwa bonge moja la hit na kumuweka katika ramani kama msanii wa Bongo fleva.

Miezi michache iliyopiata Gigy Money alitangaza kuwa ni mjamzito na mara moja Gigy amesema anaamini kuwa atakuwa mama mzuri na tofauti na wazazi  wengi ambavyo wangependa watoto wao wajifunze Kwenye mazuri yao na waache mabaya yao waliotenda Gigy kasema atapenda kama mtoto wake akifuata nyendo zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Gigy Money alifunguka haya kuhusu mtoto wake anayetegemea kujifungua mwezi huu:

Mimi naamini mimi ni kioo cha jamii kwaiyo nitapenda endapo mwanangu atafuata nyendo zangu kama zinalipa na kuingiza pesa Tena nitamsapoti sana na nitafurahi kama mtu atakayechukua nafasi kama Gigy wa pili atoke kwenye tumbo langu mimi”.

Gigy MOney amefunguka na kusema anategemea kuzaa mtoto wa kike na anaamini kuwa atakuwa mama mzuri kuliko watu wengi wanavyo mfikiria kuwa hatakuwa mzazi bora kwa binti yake.

Gigy Money:Inawezekana Nimebeba Raisi Hapa.

Mwanadada machachari kabisa katika taswira ya muziki wa Tanzania ,Gigy Money ambae wikiendi iliyoisha alifanya baby shower na kuhudhuriwa na wadada mbalimbali wa mjini akiwepo Jackline Wolper na Hamisa Mobeto amefunguka na kusema kuwa inawezekana amembeba raisi wa nchi  katika tumbo lake akimaanisha kuwa inawezekana mtoto atakae mzaa anaweza kuwa raisi wa nchi huko miaka ya baadae.

Gigy Money ambae alikuwa akionekana mwenye furaha muda wote anasema kuwa swala la kufanyiwa baby shower kwake ni jambo kubwa ukitegemea kuwa ndio mara yake ya kwanza kuwa mama hivyo ni jambo la kumshukuru  Mungu.

Gigy Money pia anasema kuwa endapo mtoto huyo atataka kufuata nyayo zake basi hawezi kuacha kumsapoti kwa chochote na angetamani sana kama Gigy Money mwingine wa miaka ijayo angetoka kwake yeye mwenyewe.

mtoto ni mtoto, nisiseme kuwa natarajia kupata wa kike au wa kiume au yupi kati yao.Mimi binafsi napenda sana kupata mtoto wa kike.Lakini pia nikipata mtoto yoyote yule nitashukuru sana kwa sababu hata wakati nambeba sikujua kuwa nitambeba nani humu.inawezekana labda hata nimembeba rais humu.

Au hamuamini kuwa ninaweza kutoa rais humu,lakini pia anaweza kuwa msaniikwanini asiwe msanii wakati mimi mamake tayari  ni kioo .Nitamsapoti kwa kila kitu sana,natamani sana atokee Gigy Money mwingine  kutoka kwa tumbo langu mwenyewe.

Siku ya leo ni kubwa sana kwangu mimi sio kama nyie mnavyochukulia.

Gigy Money anatarajia kupata mtoto mmoja wake wa kwanza hivi karibuni na mpenzi wake Mo-Jay.

Picha: Baby Shower Ya Gigy Money

Msanii wa Bongo fleva Gigy Money alifanya kufuru siku ya Jumamosi baada ya kufanya bonge la sherehe kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya kumkaribisha mtoto wake ‘Baby shower’.

Halfa hiyo ilifanyika katika hoteli ya Africa House Lounge iliyopo Kinondoni kujibu Dar es Salaam. Tafrija hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa na mastaa mbali mbali kama Jacqueline Wolper ambaye alifunika kwa kumtunza hela za kibongo na dola lakini pia alikuwepo Hamisa Mobetto, Tunda Sebastian na Queen Darleen.

 

 

 

 

 

 

 

Gigy Money Akiri Kumaliza Mgogoro na Mpenzi Wake

Hivi kaibuni msanii wa bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money alisikika akilalamika kuwa mwanaume wake aliyempa ujauzito(Mo-Jay) amekuwa akimtesa na kutomjali hata kumpiga bila kujali kuwa hali aliyonayo anahitaji kuwa na matunzo na ukaribu wa muda mrefu na mtu anampenda.

Gigy Money ambae ni mjamzito kwa sasa wa takribani miezi saba , aliyasema hayo na kulalamika kuwa amekuwa mwanaume asiyejua majukumu yake kwa mke ilhali kwa hali yake hapswi kufanyiwa vitu kama hivyo.

Lakini jana alipouwa akihojiwa na  Showbiz xtra Gigy Money alifunguka na kusema kuwa kwa sasa wameyamaliza matatizo yao na wako vizuri kabisa  na wameweza kutatua matatizo hayo na sababu kubwa iliyokuwa inawafanya wagombane wameigundua hivyo wameweza kuyamaliza yote.

Sina shida yoyote na mpenzi wangu kwa sasa,kila kitu kipo sawa na yakiwepo ya kuzungumza na kama kuna matatizo ya kuzungumza nitazungumza huko mbele.lakini kw sasa hatuna matatizo yoyte kabisa.-Alisema Gigy Money

 

Gigy Money Atoa Sababu za Kutaka Kuzaa na Mo-J

Mwanadada ambae ni mwanamuziki aliyejipatia umaarufu siku nyingi kutokana na kazi ya kuonekana katika video za wasanii mbalimbali na kujifunza na maswala ya muziki huko huko, Gigy Money amefunguka na kuelezea sababu ya kubeba mimba na kwa nini aliamua kuzaa na mwanaume aliyezaa nae kwa sababu watu wengi walikuwa wakihoji kilitojea nini mpaka Gigy Money aliamua kuzaa na kijana huyo ilhali kwa muda mrefu amekuwa akitaka kuwa katika mahusiano na wanaume wenye sifa za kuwa na hela nyingi.

zawadi kubwa nilikuwa natamani ilikuwa ni kuzaa na mo-j,ingawa watu wengi walikuwa hawajui ila ukweli ni kwamba mimi ndio nilikuwa natamani kupata mtoto siku zote.Sababu first he is cute lakini secondly ana mapenzi ya kweli kwa watoto kwa sababu unaweza kukuta kijana ni mzuri , handsome anavaa milegezo  lakini hapendi watoto yaani ukiwa na mimba tu na yeye anaanza kubadilika.

mo hii sio mimba ya kwanza kuwa nayo ya kwake ila hii ni mimba ya kwanza kuamua kuzaa na nilishawahi kubeba nyingine zikawa zinaharibika , zingine ninaharibu mwenyewe kwa sababu nilikuwa sina utayrai kwa kuwa sikuwa nina amini kuwa eti huyu ndo baba wa mwanangu.

Gigy money ambae kwa sasa anatamba na kibao kipya cha Mimina ni mjamzito wa mimba ya miezi saba, ambapo hivi karibuni aliwahi kulalamika kuwa mwanaume huyo aliembmbea mimba amekuwa akimpiga na kumtesa  pamoja na kwamba yuko katika hali ya ujauzito.

 

Gigy Money Aponda Utaratibu Wa BASATA Kwa Video Vixens

Msanii wa muziki wa bongo ambae pia video vixen katika video za wasanii mbalimbali Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuongelea utaratibu wa Basata wa kuwaambia video vixen kutaka kujitambulisha huku wakichagua kwa baaadhi ya watu na kuwaacha baadhi yao.

Akiongea na xxl ya Clouds Fm, Gigy Money amesema kuwa anashangaa jinsi basata wanavyomtaka yeye kuisajili wakati kuwa watu wanaofanya kazi kama yake wengi na hawajaambiwa kufanya hivyo, kwanini masharti hayo anapewa yeye na wanzie wachache.

waliniambia nifanye hivyo lakini sasa Hamisa Mobeto anafanya nini, Tunda anafanya nini,officialnai anafanya nini au unataka kuniambia kuwa mavideo vixen wote wanajulikana basata kasoro mimi tu au ni kwa sababu walishaona gigy anapata chochote kitu.

Basata wataanzanje kujali utamaduni wa msanii kama hawajali ugali wake,haujui hata mfuko wake, wewe unaniona mimi nimekaa navaa napendeza unajua napoteza shingapi?

Malamiko ya Gigy Money yanakuja baada ya kutakwa kufika ofisi za basata kwa ajili ya kujiandikisha na kazi yake ya kutokea katika video za wasanii wengne.lakini pia hili ni agizo lililotolewa na Mh. rais baada ya kuona wasanii wengi hasa wa kike wamekuwa wakivaa na kuchapisha picha na video zinazowaacha uchi.

Naibu Waziri alianza kufanya utekelezaji kwa kuwafungua baadhi ya wasani na kuwambia wengine kuchukua funzo kutoka hapo.Hata hivyo Gigy Money aliamuliwa kufanya usajili wa kazi zake mara moja na kuacha kuchapisha picha za uchi katika mitandao ya kijamii.

Kwa sasa Gigy Money anatamba na kibao kipya cha mimina baada ya kufanya vizuri na kile cha papa.