Hamisa Mobetto Ndani Ya Bifu Zito na Familia Ya Diamond

Mzazi mwenza na mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amejikuta katika kiti cha moto baada ya familia ya Diamond kumgeuka na kumuwashia moto kwenye mitandao ya kijamii.

Sakata hili lilianza siku ya Ijumaa baada ya  Diamond kuachia wimbo na video yake mpya ya wimbo unaoitwa Iyena aliomshirikisha Rayvanny ambapo ndani ya wimbo huo Video Queen ni Zari.

Sio siri kuwa Hamisa pamoja na kwamba amerudiana na Diamond lakini hana uhusiano mzuri na familia ya Diamond ambayo ilishaweka wazi kuwa hainpendi na haimaanishi kwani ni juzi tu kulikuwa na sakata kati ya Hamisa na Mama Diamond.

Baada ya wimbo huo wa Iyena kutoka mara moja ya Mama Diamond alianza kuposti wimbo huo na vijembe juu kwa hamisa na kudai kuwa ni mchafu hajui hata kutandika kitanda huku akimsifia Zari na alionyesha wazi kuwa anataka mwanaye arudiane na Zari.

Hata Dada wa Diamond, Esma alimtolea povu Hamisa na kuweka wazi kabisa kuwa amemiss Zari na kuandika ujumbe huu:

Familia ya Diamond ilionyesha wazi kuwa hamtaki Hamisa huku ikidaiwa chanzo cha kumchukia ni baada ya Hamisa kuwaitia Shilawadu siku walioenda hospitali kumuangalia alipokuwa amejifungua.

Nimeviona Vya Diamond Kuliko Mwanamke Yoyote Adai Hamisa

Mzazi mwenza wa Diamond, Hamisa Mobetto alifanikiwa kufanya sherehe ya mtoto wake mwishoni mwa wiki hii na alikuwa na mengi ya kuongea kuhusu mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea mtandaoni.

Maneno mengi yamesemwa juu ya uhusiano wa Diamond, Zari na Hamisa na kwa mara ya kwanza Hamisa ameongea.

Hamisa aliweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond na kuongelea kesi aliyomfungulia mahakamani:

Watu inabidi waelewe kitu kimoja, mwanamke hawezi akainuka straight akaenda mahakamani kabla hajaenda mahakamani kuna hatua anatakiwa achukue, unajua mpaka mwanamke aamue kuzaa na mwanaume  ni mpaka mjadiliane na mkubaliane mlee mimba kwa miezi tisa hawezi kurupuka tu akakupeleka mahakani unless huyo mtu hajawahi kupenda, Diamond nimekuwa nae kwenye mahusiano naye kwa takribani miaka tisa siwezi nikaamka tu asubuhi nikakurupuka na kumpeleka mahakamani nakumfungulia mashtaka, kwa sababu hakuna jipya coz kama vitu vya Naseeb hakuna mtu aliyeviona Kama Mimi yaani hakuna mwanamke anamjua vizuri kama mimi ninavyomjua kwa miaka tisa. Kuhusu kufungua kesi yeye ndio aliniambia nitafute mwanasheria ili tutafute njia ya kumhudumia mtoto bila tatizo lolote na lilikuwa wazo lake na sitapendelea kulizungumzia sana hili suala kwa sababu kesi ipo mahakamani”.

Pia Hamisa aliongelea uhusiano wake na Zari na kudai kuwa Hana tatizo lolote na Zari na kusema kuwa hamchukii Zari na ni matumaini take ipo siku wataelewana na kuwa familia kwani watoto wao ni ndugu na hicho ndo cha muhimu.