Alikiba adhihirisha yeye ni rafiki wa dhati na gavana wa Mombasa Hassan Joho

Alikiba amekua kando ya Hassan Joho mbaka wakati wa mwisho ambapo gavana huyo wa Mombasa alishinda kura na kuteuliwa kwa kipindi cha pili kama gavana.

Alikiba alisafiri kuelekea Kenya kumpigia debe Hassan Joho katika harakati zake za kutafuta kura katika jimbo la Mombasa. Staa huyo wa Bongo Flava ata alitunga wimbo kumsifu gavana huyo.

Kiba pia alitumbuiza Wakenya katika kampeni ya mwisho ya mrengo wa Nasa iliyofanyika Nairobi wikendi ya mwisho kabla ya Wakenya kupiga kura.

Alikiba, Hassan Joho na Raila Odinga wakiwa kwenye jukwa jijini Nairobi

Baada ya kufanya kampeni Nairobi, Staa huyo alirejea Mombasa na gavana Joho na alikaa na yeye mbaka vile uchaguzi ukaisha.

Alikiba alionekana akimsindikiza gavana huyo kwa kituo cha kuhesabu kura ambalo lipo Bandari College jijini Mombasa.

Ali Kiba na Joho wakiwasili kwenye kituo cha kuhesabu kura jijini Mombasa

Ali Kiba ajiunga na gavana wa Mombasa kumfanyia kampeni

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ni rafiki wa dhati wa Ali Kiba. Mara nyingi staa huyo wa Bongo husafiri kuenda Kenya kumtembelea tu gavana huyo.

Jumapili iliyopita Joho aliwafurahisha wafwasi wake alipomuita Ali Kiba kuwatumbuiza, gavana huyo wa Mombasa alikua akifanya kampeni zake Kisauni. Ali Kiba aliimba wimbo maalum ambayo alimtungia gavana huyo.

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akifanya kampeni zake

“Wa Ganjoni sema! Wa Mvita Sema… Joho Tena!” Ali Kiba aliimba huku akiwaomba wanainchi wampigie kura gavana huyo.

Gavaba huyo wa Mombasa amekua akiwaalika wanamuziki kadhaa kutumbuiza wanainchi akifanya kampeni zake jijini Mombasa.