Baa Ya Uwoya Yazidi Kuwa Gumzo, Meneja Wake Mbaroni

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Irene Uwoya amerudi tena Kwenye headlines kuhusiana na baa yake kupata matatizo Tena hii umekuja baada ya meneja wa baa hiyo kuswekwa rumande.

Irene Uwoya animiliki baa inayojulikana kama Last Minute Pub ambayo inapatikana maeneo ya Kinondoni. Hivi karibuni Baa hiyo imekuwa ikikumbwa na kashfa kibao huku mmiliki wake Irene akihusishwa.

Ni juzi juzi tu kulikuwa na skendo gazeti ni juu baa hiyo ambayo ilisemekana wahudumu wa baa hiyo maarufu kama ‘baamedi’ waliacha kazi baada ya kudai bosi wao Irene hawalipi mishahara yao stahiki.

Siku ya jana Tena Global Publishers wanaripoti kuwa meneja wa baa hiyo amewekwa rumande kwa kile kinachodaiwa kuwa baa hiyo inachelewa kufungwa kila siku na kulikuwa muda maalumu uliowekwa na serikali.

Chanzo cha habari hii kimeripoti kuwa baa hiyo inachelewa kufungwa kila siku wakati kisheria unatakiwa ifungwe saa tano lakini wenyewe walikuwa bado wanaendelea kutoa huduma kwa waters wao ndipo Askari wa doria alipomtia ndani meneja.

Uwoya alipotafutwa na kuulizwa kuhusu suala hili alifunguka yafuatayo:

Mimi sifahamu chochote kuhusu kukamatwa kwa meneja wangu wewe ndio unanijulisha mimi ndio naamka halafu sikuwepo eneo la tuki, sijasafiri ila tu sipo huko kazini”.

 

Irene Uwoya: Wanawake Jamani Acheni Roho Mbaya

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amewatolea povu zito marafiki wa kike ambao amedai kuwa ni marafiki wanafki.

Siku za hivi karibuni Irene amekuwa akitengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii kuanzia uhusiano wake na ndoa yake na Msanii Dogo Janja lakini pia stori ya mgahawa wake pia imekuwa ikivuma ambapo ametuhumiwa kutowalipa wafanyakazi wake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Irene Uwoya aliwatolea povu hilo marafiki wote wa kike ambao amedai kuwa ni wanafki;

Hivi kwanini wanawake tunakuwa hatupendani??? Yaani tunajiulizaga sana…badala sisi tushirikiane ndio kwanza tunarudishana nyuma…yaani unamsikia mtu kabisa anakuponda alafu mbaya zaidi hajawahi hata kugombana nae na pengine unamsaidiaga tu Sanaa…yaani unashangaa wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako….afu ukifanya mabaya ndio wanakusifia balaa ili uendelee kuharibu …afu sasa yeye akifanya yake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwahi kufanya hivyo yaani kuna mijitu ina roho daaah!!! Mimi sahivi nimeamua si sapoti mtu yoyote asiye ni sapoti…na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiyekuwa na umuhimu kwenye maisha yako atakurudisha nyuma tu! Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote kwenye maisha yako….badilika achana na marafiki wanaokushauri starehe siku zote….kaa fikiria katika hao rafiki zako kuna siku hata moja walikushauri kitu cha maana cha kuingiza pesa??? au bata tu? Punguza watu wasio na mashko kwenye maisha yako..Punguza marafiki wasio na faida!!!”.

Irene Uwoya Adaiwa Kushindwa Kuwalipa Wafanyakazi Wake.

Habari zilizopo chini ya kapeti zinasema kuwa msanii wa bongo movies Irene Uwoya ameshindwa kuelewana na wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakifanya kazi katika baar yake moja iliyopo jijini dar maeneo ya  Magomeni kwa Fundikira kutokana na ukweli kuwa wafanyakazi hao wamekuwa wakilalamika kutokulipwa mishahara kwa zaid ya miezi mitatu sasa.

Moja ya wafanyakazi wa bar hiyo ambae aliomba kutoandikwa jina lake alipokuwa akiongea na kampuni ya habari ya GPL, alisema kuwa wameshindwa kuvumila tabia hiyo ya bosi wao kwa zaidi ya miezi mitatu sasa wamekuwa hawalipwi mishahara yao hivyo yeye na wenzeke watano wameona ni bora waache kazi kwa sababu wanashndwa jinsi a kuishi bila mishahara ilhali wanafanya kazi.

ukweli ni kwamba kama mtu anafahamu ubinadamua uweiz kumuacha mtu hakufanyie kazi kwa zaidi ya mwezi alafu anateseka wewe unashindwa kumlipa mshahara,ukizingatia maisha ya sasa ni magumu sana tumevumilia mpaka tumeshoka kwa kweli.

Mfanyakazi huyo alisema kuwa mara kwa mara wamekuwa wakimuomba bosi wao kuwalipa mshahara lakini amekuwa akiwaambia kesho kesho siku ambayo kwao kila siku imekuwa haifiki.Hata hivyo wafanyakzi hao waliona ni bora kugoma kwa sababu wamechoka kupigwa kalenda kila siku.”siku hizi kazi ni ngumu kupata lakini mpaka mtu anaamua kuacha kazi  ujue kuna taizo kubwa:”

Jitihad a za kuwatafuta zilianza na bahati nzuri alipatikana rafiki wa karibu wa irene uwoya , Mariam Ismail , ambapo yeye pia alikubali kuwa ni kweli bar hiyo imefungwa lakini kwa ajili ya matengenezo kwa sababu mahala hapo palikuwa padoga sana na wateja walikuwa wengi.

Ni kweli kuwa pale pamefungwa kwa sababu  kuna matengenezo tunayafanya ya kupaongeza pale pamekuwa padogo, na wateja wengine walikuwa wanakosa nafasi ya kukaa.

 

 

Irene Uwoya Akiri Kunyooshwa Na Mwaka 2017

Staa wa bongo movies mwenye mvuto sana Irene U woya amefunguka na kusema kuwa mwaka uliopita ni moja ya mwaka ambao   ameweza kupitia mambo mengi ambayo hatoyasahau kuliko mwaka mwingine wowote.Irene amesema hayo na kuthibitisha kuwa 2017 ni moja ya miaka yake ambayo mambo mengi yametokea na yamemfanya aweke historia.

Irene anasema kuwa kuna mwaka ambao mambo mengi yanaweza kukutokea na yapo yatakayokuwa mazuri sana au mabaya sana , lakini kwa upande wake mwaka 2017 ulikuwa n mwaka wa maumivu kutokana na kuumizwa na badhi ya matukio ikiwemo lile la kumpoteza aliyekuwa mume wake wa ndoa Hamad Ndikumana Kataut.

Mwaka 2017 umepita lakini ni mwaka ambao  wangu nilikutana na mambo mengi , mengine ya kufurahisha kidogo lakini pia mengi yamekuwa ya kuumiza sana.kubwa zaidi lilikuwa lile la kumpoteza mume wangu  na ninamuomba tu mungu mwaka huu wa 2018 uwe mwaka wa amani na baraka tele kwangu.

mwaka uliopita irene alikuwa ni moja ya wasanii wa kike walisema sana katika mitandao ya kijamii kutokana na atukio mengi yalikuwa yakimtokea, ambapo alimpoteza mume wake na kifo hicho bado kilisemekana kuwa kimesababishwa na yeye mwenyewe kutokana na kuolewa na mwanaume mwingine bila kupeana talaka na  mumewe huyo.

Shamsa Ford Awatolea Povu Waliomchamba Baada ya Kusema Uwoya Mzuri Kuliko Wanawake Wote Bongo movie

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewatolea povu mashabiki wote wanaomsema vibaya baada ya kusema kuwa Irene Uwoya ndiye mwanamke mzuri kuliko wanawake wote kwenye tasnia ya Bongo movie.

Siku ya Jana ilikuwa ni sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo movie Irene Uwoya kama kawaida mastaa wenzake wengi walimtumia salami za kumtakia kheri mmoja kati ya watu hao ni rafiki yake Shamsa Ford.

Shamsa aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kumwagia sifa kibao kuwa ni mzuri kuliko wanawake wengine wa Bongo movie, baada ya kusema hivyo mashabiki walimjia juu kwa maneno na mateso.

Shamsa alishindwa kuvumilia maneno hayo na kuwatolea povu hili:

Yani Jana kusema huyu mwanamke ni mzuri kuliko wanawake wote wa Bongo movie imekuwa shida. Yaani mpaka mnanitumia msg za matusi? Binadamu nyie ni watu wa ajabu aisee….huo ndio ukweli mbishe mkatae kwa upande wangu na ninyi wote mnakubali moyoni machoni mnakataa huyo ndio mzuri. Hana kasolo hata moja kea vitu vya muonekano. Amejaaliwa na mwenyezi Mungu kuanzia juu mpaka chini. Mimi huwa nalionaga kama jini akipita lazima ustuke. Wanawake kusifiana ni ngumu lakini mimi huwa siwezi kuacha kumsifia mtu. Narudia tena Irene ni mwanamke mzuri na mwenye mvuto kuliko wanawake wote wa Bongo movie”.

Baada ya kusema hayo watu walizidi kumjia juu Shamsa huku wakitaja wasanii wengine wa Bongo movie kama Wema, Jennifer Kyaka, Wolper, na kudai kuwa ni wazuri kuliko Irene.

Alichojiandika Irene Uwoya Kwenye Kumbukumbu Yake Ya Kuzaliwa

Msanii wa kike Irene Uwoya ambae  ame-trend katika mitandao kwa muda mrefu sana kutokana na mfululizo wa matukio yake katika maisha yake hivi karibuni ambae jana alikuwa akitimiza miaka kadhaa katika  kumbukumbu ya  siku yake ya kuzaliwa alijiandikia maneno yenye kujitia hamasa lakini pia kuonyesha kuwa ni kwa jinsi gani alivyopitia magumu lakini bado anajitia moyo na kujifariji kuwa yeye ni moja ya wanawake wajasiri wenye kupambana na maisha yao bila kusumbua watu wengine.

Irene katika ukurasa wake wa instagram alisema kuwa amepitia mengi magumu lakini bado ameweza kusimama na kuwa katika hali ya kawaida na Mungu peke ndie aliyeweza kumuongoza kufika hapo.

I am strong woman…everything that hit me I have dealt with  on my own, i’ve cried  my self to sleep , picked my self back up and wiped my own tears I have grown myself from things that meant to break me , I get stronger by the day and  I have God to thank for that …… Happy Birthday to me.

Kwa mwaka huu ambao inaweza kusemwa kuwa umekuwa mwaka mwenye kumpa changamoto irene baada ya kufunga ndoa na dogo janja alisemwa sana katika mitandao kwa maamuzi hayo, lakini pia alipata ,msiba wa kufiwa na aliyekuwa mume wake  Ndikumana , lakini pia bado mambo yanazidi kuwa mabaya kutokana na kuvuja kwa picha zinazomuonyesha yuko kitandani akiwa na moja ya vijana wadogo .

T-Bway Akacha Mahusiano na Uwoya

Baada ya kusambaa na kuvuja kwa picha ikimuoyesha msanii na mjasiriamali Irene Uwoya ambae pia ni mke halali wa ndoa wa msanii wa bongo fleva Dogo Janja na mwanahabari na mtangazaji T-bway wakiwa wameonekana wakiwa kitandani faragha, mwanaume huyo ameamua kufunguka na kusema kuwa picha hiyo ni ya zamani kabla hata wawili hao hawajafunga ndoa.

Irene Uwoya mabe amekuwa akiingia kwenye skendo hivi karibuni tena hasa baada ya kufunga ndoa na Dogo Janja ambae ni mdogo kwake kiumri ameonekana kuwa ni tabia yake kutembea na wanaume walio chini ya umri wake maarufu kama vi-ben 1o kwa sabau hata huyo T-bway ni mdogo kiumri.Hata hivyo baada ya picha hiyo kuvuja katika mtandao bado ilileta tafrani kwa sababu Dogo Janja na Irene hawana muda mrefu tangu kufungwa kwa ndoa yao hivyo inakuwaje tena Irene kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine.

Akiandiak katika ukurasa wake wa instagrma Dogo Janja alionekana kutokujali kwa maneno na picha hizo na  alisema kuwa hawezi kugombana na mke wake huyo mpendwa kwa sababu ya maneno ya watu kwa sababu anampenda sana mke wake,

Hata hivyo nae R-bway hakuwa wazi sana kuhusu maneno yake ila alisema kuwa wamekuwa wakimsema kuhusu picaha hiyo ilhali ni ya zamani.

when you wake up in the morning  and you find out everything  everything is going west  but you decide to go east #YAZAMANIKABISA-Aliandika t-bway katika ukurasa wake.

Inasemekana kuwa wawili hao walikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu zamani kabla mwanadada huyo hajaolewa na kuwa mke halali wa Dogo Janja.

Picha zilizovuja zikiwaonyesha Irene Uwoya akiwa na T-bway faragha,

Familia Ya Ndikumana Imempa Uwoya Baraka Zote Kuendelea na Maisha Yake ( Picha na Video)

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amekuwa katika kipindi kigumu sana kwani mara baada ya kufunga ndoa na mumewe Dogo Janja mume wake wa zamani Hamad Ndikumana alifariki dunia hali iliyozua utata kwani habari zilisema kuwa Uwoya alikuwa na ugomvi na familia ya marehemu mumewe hadi kufikia hatua ya kukatazwa kuhudhuria msiba.

Baada ya Uwoya kusafiri na familia yake kwenda Nyumbani kwa Ndikumana na familia yake nchini Rwanda alionekana kupokelewa na hata kuweka wazi kuwa tofauti na watu walivyokuwa wanadai kuwa wakwe zake walimshutumu kuwa kamuua mtoto wao lakini wameonyesha kumpokea vizuri na hata kulia naye na mwishoni wamempa baraka zote ili akaendelee maisha yake na mume wake mpya.

Tangu kifo hicho kitokee Uwoya hajaongelea sana bali aliandika maneno haya machache kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Mungu wewe ndio unajua moyo wangu ukinijua wewe inatosha…My trust is in you Gid.. R.I.P Baba Krish”.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazomuonyesha Uwoya akipewa baraka zote na familia ya Ndikumana huko nchini Rwanda:

Mwenye Jina La Tatoo Ya Uwoya Akana Kumjua Mrembo Huyo

Kulikuwa na tetesi kuwa moja ya vijana matajiri Tanzania anaejulikana kwa jina la Salaah alikuwa na uhusiano wa mapenzi na msanii Irene Uwoya, lakini tetesi hizo zilikanushwa na kijana huyo baada ya kuulizwa kuhusu habari hizo.

Kipindi cha nyuma kidogo Irene Uwoya alionekana akijinadi na tatoo kubwa mgongoni kwake iliyokuwa imechorwa  jina la Salaah, na ikathibisha kuwa mpaka mrembo huyo kuweza kumchora tatoo hiyo basi ni kweli kuwa wawili hao watakuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini tetesi hizo zilikuja kuzimwa baada ya mwanadada Irene Uwoya kuolewa na msani mwenzie Dogo Janja.

 

Muonekano wa tatoo ya  yenye jina la kijana mmoja tajiri  mgongoni mwa Uwoya.

Moja ya watu wa karibu wa Irene aliwahi kuthibitisha na kusema kuwa jamaa huyo alikuwa amekufa na kuoza kwa mrembo Irene na kutokana na upendo huu mwanadada aliamua kumuonyesha kwa kumchora tatoo hiyo ya jina lake mgongoni.

Hata hivyo moja ya magazeti pendwa kutoka Global walitaka kumtafuta Irene Uwoya , hii ilikuwa kabla hajapata matatizo ya msiba lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda, lakini waandishi hao hawakutaka kuishia hapo ndipo walipoamua kuanza kutafuta namba za kijana huyo tajiri nchini ili kuulizia kuhusu tetesi hizo.

kijana huyo alipatikana kwa njia ya simu lakini alisema kuwa yuko nje ya nchi hiyo hawezi kuonana nao lakini walipata nafasi ya kumuuliza papo kw apapo kuhusu tetesi  hizo na kijana huyo alisema kuwa hana lolote analolijua kuhusu msichana huyo na kuhusu tatoo yeye hausiki na chochote.

Sikilza hayo mambo unayozungumzia  mimi siyajui kabisa, wala huyo unaemtaja mimi simjui kabisa  na ndo kwanza nakusikia wewe hapo unamsema , kwaio tafadhali kabisa naomba msiniusishe na hayo mambo.  -Aliongea kijana huyo katika simu

Inakuwa kazi kwa baadhi ya watu wanaojikuta wakichora tatoo za kudumu katika miili yao na kushindwa kufutika kwa sababu wanapoachana na wapenzi hao alama hizo zinabaki katika miili yao.

Irene Uwoya  kwa sasa yupo katika kipindi kigumu kutokana na kufiwa na mwanaume aliefunga nae ndo kanisani na mzazi mwenzie Hamad Ndikumana Kataut.

Huu Ndio Ujumbe Mzito Ambao Marehemu Ndikumana Alimuandikia Mkewe Irene Uwoya

Aliyekuwa mume wa muigizaji wa Bongo Movie Irene Uwoya, Hamad Ndikumana Kataut amefariki leo kwa kile kinachodaiwa ni ugonjwa wa moyo.

Kwa muda mrefu sasa Uwoya amekuwa hana maelewano na mzazi mwenzie huyo ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume. Sio siri Ndikumana hakuwa na furaha siku ambayo Uwoya aliolewa kwani bado kisheria na kidini alikuwa mke wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ndikumana aliamuandikia Uwoya ujumbe huu mzito akimsihi amruhusu anyone mtoto wao ambaye hakumuona kwa miaka miwili:

Ungekuwa na roho ya kibinadamu ungekuwa hata unataka niwasiliane na mtoto wangu, ila miaka miwili hujawahi kuchukua simu unipigie umpe mtoto niongee naye, hata picha tu hutaki kunitumia but naelewa kwanini unafanya hivyo na baada ya yote haya naamini hutotaka nimuone tena but its OK Mungu yupo na ipo siku Irene ulichoniambia umeota juzi hujakosea hata kidogo ni kwa vile ulinifundisha mengi ndio maana hayaonekani na siwezi kuyaonesha but ndoto yako hukukosea, nadhani nilikwambia mpaka umeniota basi nataka kufa na nikifa usihangaike, krish na Baasit kipo nilichowaandalia kwa siku zijazo na ninamuamini anachokisimamia wakati nitakaokuwa nimendoka atatekeleza vizuri sana. Ulilia kwa muda mrefu sana kuwa unataka talaka uolewe Tena mimi sina pingamizi”.

Marehemu mpaka mauti inamfika alikuwa mcheza mpira katika klabu ya APOP kinyras Peyias

Uwoya Akerwa Na Tabia ya Kubadili Marafiki

Akiwa ni mmoja ya wasanii wa kike walioshikwa headline katika vyombo vya habari wiki chache zilizopia, mwanamama Irene Uwoya amefunguka na kuongelea tabia ya baadhi ya wasichana kuwa na tabia ya kubadilsidha marafiki na mashoga mara kwa mara na kusema kuwa kwa upande wake yeye hicho kitu kilishamshinda na moja ya vitu vinavyomsaidia kufanikwa katika maisha yake ni kuwa na marafiki wa kudumu amabo wakekuwa wakimsaidia katika maisha yake.

Uwoya anaongezea kuwa kwa muda wa takribani miaka nane amekuwa na marafiki wale wale ambao waliweza kusomana na kujua hivyo imekuwa rahisi kwao kukaa pamoja na kufanya maisha kwa sababu wameshakuwa kama ndugu sasa.

Kitu ambacho kilishanishinda mimi katika miasha ni kubadili marafiki na mashoga ,lakini pia tabia yangu ya kuwa nakaa na mashoga muda mrefu imekuwa ikinisaidia sana kuepukana na vitu vingi mno. na ndio maana marafiki zangu mimi huwa ni haohao na kwa sasa wameshakuwa kama ndugu zangu kabisa.-Alisema Irene

Wasanii wengi wamekwa wakishindwa kukaa na marafiki kwa muda mrefu na kusabaisha kila siku kuwa na mtu mpya kiasi kwamba inafika sehemu msanii anakuwa na skendo nyingi na kuvujishwa kwa siri zake nyingi bila kujua ni ani aliefanya hivyo, hii nikutokana na kuwa na  marafiki wengi ambao pia unakuwa unashindwa kuwaamini.

Mfano mmoja ni wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiteswa sana na marafiki ni Wema Sepetu ambae amekuwa akiwakaribisha watu wengi kuwa nao karibu kama marafiki lakini wengi wamekuwa wakishindwa kukaa nae na kumsaliti na wengne kumfanyia vitu vibaya na kumuumiza.

Marafiki ni watu muhimu katika maisha kwa sababu sio kila muda utakiwa ni mwenye furaha tu ipo kipindi utahitaji watu watakaokusaidia katika matatizo pia, hivyo ni bora kuwa na mtu unaeweza kumuamini na kumfanya kama ndugu katika kila jambo unalolifanya.Tena kwa wasanii wanapswa kuwa wanachagua marafiki ambao watakuwa watu wasioweza kuwasaliti na kuchafua majina yao na hata kushusha hadhi zao kwa mashabuiki wao .

Ndoa Ya Irene Na Ndikumana Haijavunjika

Baada ya kusambaa kwa picha nyingi za harusi kati ya msanii wa bongo fleva Dogo Janja na msanii wa bongo movie , mwanadaada mlimbwende katika tasnia hiyo Irene Uwoya  na hata baadae watu hao kuamua kuthibitisha ndoa iyo ingawa baadhi ya mashabiki na watu wao wa karibu bado wakiona ni kama kitendawili kilichokosa majibu kwa wawili hao kuoana.

Hata baada ya kusambaa kwa picha hizo , mume wa kwanza wa Irene Uwoya  anaefahamika kama Ndikumana ambae walifunga nae ndoa ya kikristo kanisani pia alijibu mapigo kwa kuweka post akiwa na mwanamke mwingine inaesemekana kuwa ni wa nchini kwao.Wawili hao walitengena bila idhini ya imani yao iliyowaunganisha kukubali wao kutengana .

Akizungumza na moja ya waandishi wa habari wa gazeti pendwa hapa nchini moja ya waasisi wa dini ya kikristo ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa hata kama Irene Uwoya ameamua kuolewa na mwanaume mwingine lakini bado ndoa yake na mumuwe wa kwanza aliefunga nae  kanisani bado inatambulika palepale kwa sababu kanisa lilichukua jukumu la kuwaunganisha kwa makubaliano na pia ilitakiwa warudi tena kanisani kupata ushuruhishi wa matatizo yao.

Ndoa yao bado ipo hai kabisa kanisani kwa sababu kanisani kwetu hauna talaka,talaka itatoka pale kumegundulika tatizo kubwa kama mmoja atakuwa anazini na ushahidi ukawepo kabisa au kutokee  tatizo la kinyumba  ambalo haliwezi kutatulika ndio kibali cha talaka kitatolewa na ndoa itabatilishwa  lakini kimsingi kabisa kanisa halitambui talaka.

Hata hivyo kiongozi huyo alisema kuwa kwa kile anachokifanya Irene na muwe wake huyo wa ndoa kwa kubadilsha wanawake kila siku ni dhambi ya kizini ambayo kanisa pi inaikataza.

Kanisa linakataza kabisa uzinzi na wanachokifanya wao kwa sasa ni uzinzi,kitendo hicho hakimpendezi mungu kabisa, kwa sababu ni kinyume na biblia inavyosema na imani ya kikristo.wanatakiwa wabadilike wakae  wamalize tofauti zao.

Irene Uwoya na Ndikumana walifanikwa kufunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja ambae , kwa sasa Irene ameolewa ndoa ya kiislamu na kuachana na ndoa ya kikristo aliyokuwa nao kwanza.

Mama Wa Dogo Janja Alitoa Baraka Za Harusi Ya Mwanae na Uwoya

Mama mzazi wa msanii Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya mwanae kuoa tangu mwaka jana, ingawa kwa mara ya kwanza Dogo Janja hakumwambia kama anafunga ndoa na mwanamke gani. Mama huyo akiongea kwa njia ya simu alisema kuwa hata baada ya kuambiwa kuwa Irene Uwoya ndio mwanamke anaeolewa na mwanae bado hakusita kutoa baraka kwa sababu anaamini kuwa huo ni uamuzi wake.

“Sio kupata taarifa tu,Dogo Janja aliniambia kabisa kwamba anaoa tangu zamani,na nilimpa baraka zangu zote za yeye kuoa, na mimi nilimwambia kuwa kama atakuwa tayari atanijulisha, basi alipokuwa tayari alinijulisha lakini kwa sababu mambo yalikuwa yameingiliana basi nikaona isiwe shida nikamkabidhi kwa Madee kwa sababu Madee ni kama baba yake, aliweza kumchukua tangu mdogo na kumsimamia

Hata hivyo mama huyo alipoulizwa kuhusu mwanamke aliemuoa mwanae,mama mzazi wa Dogo Janja alisema kuwa alikuwa  anajua kabisa na kwa dini yao kuona ni suna”Nilikuwa najua kabisa ni Irene Uwoya, na kwa dini yetu ya kiislamu kuoa mwanamke aliekuzidi umri ni suna, maana hata kuongozi wetu mkubwa alioa mwanamke mkubwa, na kwa upande wa umri kwangu wala sio shida kikubwa tu ni maelewano katika ndoa lakini umri wala haijalishi”

Irene Uwoya na Dogo Janja katika picha ya pamoja na watu wao wa karibu

Hata hivyo mama huyo aliendelea kusema kuwa yeye na Irene Uwoya hawajawahi kuonana lakini wamekuwa wakiwasilina sana , na kuna kipindi Irene alikwenda Arusha lakini yeye hakuonanan nae, kuhusu mahusiano yake na mkwewe huyo mama anasema kuwa Irene amekuwa akituma zawadi mbalimbali kwa mama mkwe wake huyo na wanawasilina karibia kila siku.

Mama mzazi wa Dogo Janja amenasema kuwa ingawa ndoa imekuwa ya haraka haraka lakini wanategemea kufanya sherehe kubwa ya harusi itakayo fanyika Arusha kwa ajili ya familia kumtambua, na kwa upande wake yeye ameridhika kabisa wala hana wasiwasi na uamuzi aliochukua mwanae.Akisema kuhusu yeye kutokuudhuria ndoa hiyo anasema kuwa yeye alikuwa ametingwa na baadhi ya mambo lakini anamwamini sana Madee kwa sababu  ndie aliemlea tangu alipokuwa mtoto.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja ilifungwa wiki iliyopita na kuacha gumzo katika mitandao kutokana na umri wa watu hao wawili kupishana sana na hata hivyo wawili hao walishakataa sana kuhusu kuwepo kwa mahusiano baina yao.

 

 

Mume Wa Uwoya Amedai Hajali Wala Hana Habari Kama Mkewe Ameolewa na Dogo Janja

Moja kati ya stori ambazo zimeshika headline sana siku mbili hizi ni hii ya Uwoya kuolewa na Dogo Janja huku yakiwa yanasemwa mengi ikiwemo ni kuwa wawili hao hawajafunga ndoa bali ni kiki tu kutoa wimbo mpya.

Stori inazidi kupata mkanganyiko kwani Irene Uwoya anayedaiwa kuwa no bibi harusi na kuolewa na mwanaume mwingine kiukweli ni mke wa ndoa halali kabisa ya kanisani ya mcheza mpira kutoka Congo anayejulikana kama Kataut Ndikumana. Ndikumana na Uwoya walioana miaka michache iliyopita na kwapamoja wana mtoto mmoja wa kiume.

Baada ya sakata hili kutokea watu wengi wamekuwa wakijiuliza inakuaje kuwa Uwoya anaolewa wakati tayari mke wa mtu? Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Ndikumana alimjibu shabiki aliyemuuliza kama kweli mkewe Uwoya ameolewa na Dogo janja na Ndikumana alijibu;

Huyo Irene aolewe asiolewe mimi sina habari naye nina msimamo wangu na maisha yangu binafsi mda mrefu tu, kwani sins habari na mtu nadeka zangu kwa mpenzi wangu”.

Ndikumana aliweka ujumbe huo akaambatanisha na picha ikimuonesha akiwa amekumbatiana kimahaba kabisa na mpenzi wake kuonesha hajaumizwa na ndoa ya Irene.

Ukweli wa ndoa ya Uwoya na Dogo Janja lilizidi kuingia doa baada ya jana msanii Keisha kuweka picha ya Uwoya na Dogo Janja na kusema kuwa ile ni kiki kwa ajili ya kundi la Tip top connection ambapo inasemekana wanataka kurudi upya na ngoma mpya hivyo haikuwa Ndoa ya kweli.

Ndoa Ya Dogo Janja Na Uwoya Ni Kiki

Ikiwa bado kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu ndoa ya msanii wa muziki Dogo Janja na mwana bongo movie Irene Uwoya, ebu tuangalie jinsi wasanii hawa ambavyo wanataka kuchanganya akili za mashabiki na watu wanaowapenda lakini wanashindwa kufunguka na kusema ukweli wa mambo yao yote.

Baadhi ya vyombo vya habari vilianza kuwatafuta wasanii hawa mara tu baada ya picha za msanii Irene Uwoya kusambaa zikionyesha amevaa gaunu la harusi.alipopatikana dodgo janja alijibu tu kwa mkato na kusema yeye hajui chochote.Jitihada zilipoendelea irene uwoya alipatikana na moja ya waandishi wa gazeti pendwa nchini, katika simu irene alijibu” mimi ni wa kuolewa, na ntaolewa na nani?” hata hivyo mwanadada huyo aliongezea na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni movie tu inachezwa.

Madee akiwa kama mtu wa karibu kabisa na Dogo Janja alikuwa ni moja ya watu waliokwepa kwa muda mrefu kutoa taarifa zozote kuhusu ndoa ya Dogo Janja lakini baadae katika ukurasa wake wa instagram Madee aliposti picha yenye kuashiria kujua kiundani tukio ilo

Ndoa ni jambo la kheri, itakuwa ni tatizo kama inakuwa vigumu kwa msanii huyo kuweka wazi swala lake la ndoa hasa mwanaume wake anaeenda kukaa nae katika ndoa hiyo.Leo tarehe 30 Oktoba, Irene Uwoya aliposti picha yake nyingine na kusema kuwa ameolewa na mwanaume anaempenda huku akimshukuru na kumtag dogo janja kuwa ndie mwanaume wa ndoto zake.

Kwa kumbukumbu zinazoonyesha,katika akaunti ya instagram ya mwandada Irene Uwoya zipo baadhi ya picha zinazohusiana na ndoa iyo, moja ya picha hizo zilionyesha kadi za harusi hiyo, je ni kweli tunashindwa kuhoji mbona jina lililopo katika kadi ni tofauti na jina la mtu tunaeambiwa kuwa ndie aliefunga nae ndoa.Nani amegundua hili

Hii ni kadi ya harusi  ya Irene Uwoya , ambae inavyoonyesha na kwa jinsi ilivyosemekana ni kuwa alibadil jina na kuitwa Sheila baada ya kuabdili dini na kuamia upande wa mwanaume anaemuoa.

Nadhani kuna kitu hapa wasanii hawa wanataka kutuchezea,kuwa wazi ni vizuri zaidi ingawa italeta gumzo sana kutokana na umri wa Dogo Janja na irene uwoya ,lakini pia wawili hawa walishasikika mara nyingi wakikanusha tetesi za kuwa wapenzi.je nini kinaendelea?, kwanini Irene hataki kumuweka wazi mwana harusi?, au wanatengeneza kiki kutokana na mitandao inavyowapa muda mwingi kuwazungumzia.

Irene Uwoya Kuolewa Tena Kwa Mara Ya Pili

Malkia wa filamu za bongo Movies  ambae anaingia kwenye orodha ya wanawake wenye mvuto  kwa wasanii  wa kike Tanzania, amezua gumzo mtandaoni baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akionekana amevaa nguo ya harusi(shera) .Gumzo ilo linaunganishwa na baadhi ya matukio ya picha za mwanadada huyo siku chache zilizopita alipoweka picha ya pete na kuandika “i cant wait…”, lakini baada ya hapo aliaweka picha nyingine zinazomuonyesha akiwa amevaa shela la harusi.

Katika post hiyo Irene aliandika”pre-wedding with family and friends..my friday will be super than ever….. kuna wakati  tunanyang’anywa tuvihisivyo vizuri kwetu,na kuletewa bora zaidi, ili tujifunze na kuthamini maradufu..asante kwa hili MUNGU”

Kuna baadhi ya watu wameonekana kuwa na wasiwasi na kusema kuwa inawezekana ikawa ni project mpya ya movie inayokuja kwa sababu wamekuwa na mashaka ya kuolewa kimya kimya kwa msanii huyo ingawa kwa sasa imekuwa kama fashion kwa baadhi ya watu maarufu kufunga ndoa zao kimyakimya , na kupost picha tu.

Hii itakuwa ni kwa mara ya pili Irene Uwoya kufunga ndoa, mara ya kwanza alifunga ndoa na mcheza mpira maarufu  kutoka Rwanda Hamad Kataut Ndikumana ambapo walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume lakini baadae walikuja kuachana bila sababu ya kuachana kwao kuwekwa wazi.

Inawezekana Irene hasiwe msanii wa kwanza kufunga ndoa zaidi ya mara moja na kushindwa kukaa na kudumu katika ndoa, au in awezekana pia sasa ikawa ndio uamuzi wake wa kuolewa umefika, wasanii wengi wamekuwa hawadumu katika ndoa na mahusiano yao labda kwa sababu ya kuwa na scandal nyingi kutokana na umaarufu mkubwa walionao.Ingawa pia wapo wanaopiga picha za harusi kwa sababu tu ya kufanya project fulani ya kazi yake ,hivyo Irene Uwoya anatakiwa aandike na kuongelea swala hilo ili kuwatoa kimasomaso mashabiki zake ambao wamekuwa na hamu kubwa kujua juu ya picha hizo.Kama kweli amefunga ndoa basi Kila lenye kheri kwake.