Mbwana Samatta Na Ndoto Yake Ya Kumiliki Private Jet

Msakata kabumbu maarufu nchini Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa katika timu ya KRC Genk kutoka nchini Ubelgiji ameiweka wazi ndoto yake ya kumiliki private jet.

Samatta ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Tanzania ya Taifa Stars amesema hayo baada ya kuonekekana akiwa amepiga picha mbele ya private jet ya timu yake ya KRC Genk.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbwana Samatta ameandika maneno haya kuhusiana na ndoto hiyo:

Ndoto za kumiliki private jet zimeanza baada ya kupiga picha hii, sio kila ndoto inaweza kutimia lakini wacha vita ianze”.

Samatta anafanya vizuri sana katika klabu yake hiyo baada ya kung’ara katika michezo ya kufuzu kucheza UEFA europa League,baada ya kuisadia klabu yake hiyo kufuzu katika michuano hiyo.

Nilipenda Zaidi Kuwa Mwanajeshi Kabla Ya Soka- Mbwana Samatta

Msakata kabumbu la kulipwa katika KRC Genk ya Ubelgiji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka na kuweka wazi kuwa zamani alitamani zaidi kuwa mwanajeshi.

Mbwana Samatta ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ameweka wazi kuwa mwanajeshi ndio ilikuwa ndoto yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Muda mwingine mungu akupi unaloliomba ila anakupa linalo kustahili…
Kabla ya soka,nilikuwa natamani kuwa mwanajeshi,je kwa sura hii unadhani ningependeza kuwa soja?”.

Mbwana Samatta na kikosi kizima cha Taifa Stars wapo njiani kuelekea Uganda kwa ajili ya kuikabili timu ya Uganda ‘The Cranes’ ikiwa ni mchezo wa kuwania kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon mechi itakayochezwa tarehe 8 Septemba 2018.

Ali Kiba Atangaza Vita Na Mbwana Samatta Uwanja Wa Taifa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anayeendelea kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Mbumo wa Radi, atapimana nguvu na mchezo soka la kulipwa Mbwana Samatta uwanja wa Taifa.

Ali Kiba amajulikana kwa uwezo wa kucheza mpira uwanjani na alikwisha weka wazi kuwa ana mapenzi mazito kwa mpira wa miguu na hata kusema asingekuwa msanii basi siku nyingii angekuwa mcheza mpira.

Kwa mara ya kwanza uwezo wa kusakata soka ulionekana Kwenye mechi iliyohusisha wasanii wa Bongo fleva na wasanii wa Bongo movie miaka ya nyuma kidogo.

Habari njema kwa mashabiki zake ni kuwa utamshuhudia Ali Kiba Live kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 9 juni mwaka huu akiwa na Mshambuliaji wa timu ya taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta.

Ali Kiba ametangaza Habari hiyo njema kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika ujumbe huu:

Tukutane Taifa naomba unichagulie kikosi bora unacho kikubali kutoka team tofauti katika ligi ya TANZANIA bara.

Wawili hao watakutana kwenye mechi maalumu ya ubalozi wa kujitolea ili kuchangia elimu, hata hivyo orodha ya majina mengine ya wasanii yataendelea kutajwa kadri ya siku zinavyokwenda.

Mbwana Samatta ameandika ujumbe huu kutjibitisha kuwepo katika pambano hilo:

Nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?