Prezzo Kafulia Choka Mbaya- Gigy Money

Video vixen na Msanii wa Muzikiwa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameweka wazi msanii kutoka Kenya Prezzo hivi sasa amefulia vibaya mno.

Gigy Money alifunguka hayo wakati anaongelea uhusiano kati ya Rafiki yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Gigy Money ameweka wazi hivi sasa ukimuona Prezzo siyo yule uliyekuwa unamuona kwenye Tv amekonda vibaya mno yaani kafulia:

Yaani Prezzo kakonda kuliko hata unavyomuona Kwenye picha naona ni stress za kimaisha kwa sababu mimi nimeenda kuperfom juzi juzi Nairobi nimeondoka club nimemuacha Prezzo mpaka asubuhi saa saba za usiku hana direction yoyote.

Alikuwa ana jina zamani sio sasahivi hata wanavyomchukulia huko Nairobi sio tunavyomchukulia sisi huku Bongo yaani amefulia choka mbaya hayupo kwenye peak tena hata huku tunamuongelea sababu ya Amber”.

Gigy Money amedai Kenya wasanii wenye majina ni wasanii kama Nyanshinki, Will Paul, Khaligraph na wengine lakini ukimtaja Prezzo watu watakucheka sana.

Prezzo Awachana Wasiopenda Penzi Lake Na Amber Lulu

Mwanamuziki Prezzo kutoka Kenya ameibuka tena na kuwachana wasiopenda penzi Lao yeye na videi queen maarufu Bongo, Amber Lulu.

Prezzo ambaye ameweka wazi wiki chache zilizopita kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo Amber Lulu baada ya kuficha ukweli kuhusu uhusiano wao kwa kipindi kirefu kidogo.

Prezzo ambaye kwa mara ya kwanza alisemekana kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Amber Lulu baada ya kuonekana pamoja hoteli moja maarufu hapa Dar es Salaam wakilala kwenye chumba kimoja ingawa kwa muda ule aliendelea kukataa kwamba hana uhusiano naye.

Amber Lulu amekuwa akishika headline nchini Kenya baada kuingia kwenye vita ya maneno na mwanamuziki mwingine kutoka Kenya anayejulikana kama Noti Flow ambaye anadai pia ni mpenzi wa Prezzo ambapo siku chache zilizopita alidai kuwa Amber Lulu anajipendekeza kwa Prezzo akijua wazi kuwa ni mwanaume wake kwa kipindi kirefu.

Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Prezzo amewapa ujumbe wale wote wasiopenda penzi lake na Amber Lulu ambapo ameandika maneno haya;

Pilipili msioila yawawashia nini? Sisi tuko fresh kama chungwa #lulumafia #Rapcellency #Themakiniteam”.

Amber Lulu naye amezidi kuweka wazi hisia zake na kusema kuwa ana mapenzi ya kweli Prezzo japo kuwa wapo nchi mbili tofauti.

Amber Lulu Ni Msichana Mzuri Nimeshamtambulisha Kwa Mama- Prezzo

Mwanamuziki kutoka Kenya, Prezzo amekuwa akishika vichwa vya habari nchini Tanzania baada ya tetesi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na model na video vixen maarufu kama Amber Lulu.

Miezi michache iliyopita Amber Lulu na Prezzo walionekana pamoja kwenye kumbi mbali mbali za starehe pia kuna picha mtandaoni zikiwaonyesha wakiwa na ukaribu sana ingawa wote walikataa kuwa hawana uhusiano wowote zaidi ya urafiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Prezzo alisema kuwa Amber Lulu ni msichana mrembo na ikitokea siku wakawa wapenzi atakuwa na furaha:

Amber Lulu is a very good friend of mine you know ni mtu ambaye nimejuana naye muda mrefu unajua watu huwa wanachanganya mambo wakikuona uko na msichana wanajua ni mna mahusiano au mandate or something lakini Amber ni rafiki yangu watu wengi hawafahamu kuwa ana roho nzuri sana, ana roho ya huruma na ni mtu anayejali watu wengine hivyo kwakweli mimi sio Mungu siwezi kumhukumu mtu mwingine ila nam-judge Amber Lulu kwa uzuri wake ndio maana mimi na yeye ni mabeste”.

Pia Prezzo aliendelea kufunguka kuwa kama siku ikiwezekana anaweza kabisa kutoka na Amber Lulu;

lakini pia inawezekana siku moja nikawa na uhusiano na Amber Lulu ukitegemea Mimi ni mwanaume na yeye ni  mwanamke halafu ana roho nzuri na ni mrembo kwa nje na ndani unajua watu wanaweza kumuona yupo kwa TV akafanya vituko hivi na vile lakini na yeye ni binadamu so kuna wakati akijisahau amefika ukingoni lakini ana roho safi ndio maana nimeshamtambulisha kwa mama angu na ni marafiki wakubwa na pia mama ni shabiki mkubwa wa Amber Lulu”.