ShiiKANE- Diamond ni Msanii Anayejituma Hata Kama Humpendi, Utakubali Kazi Zake

Kundi la muziki kutoka Nigeria linaloundwa na wadada watatu wanaojulikana kama ShiiKANE wamefunguka na kumkingia kifua staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Miezi michache iliyopita Diamond alishinda tuzo ya msanii bora wa kuime nchini Nigeria na kuwabwaga mastaa wakubwa kama Davido kitendo ambacho kiliwakera Wanigeria ambao waliweka wazi kuwa hawakupenda Diamond kushinda.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kundi hilo la ShiiKANE kutoka Nigeria linasema Diamond alistahili tuzo hiyo kutokana na ukweli usiopingika kuwa ni mchapakazi na kazi zake ni nzuri.

Ni mtu anayejituma hata kama haupendi au kupenda muziki wake lazima ukubaliane na anachikifanya kwa sababu anastahili kushinda alichokishinda. Kila utakapomuongea basi jua ndivyo anavyozidi kuwa juu”.

Katika tuzo hizo Diamond alishinda katika kipengele cha Best Male MVP na kuwabwaga wasanii kama Runtown, Davido, Olamide, 2face Idibia, Wizkid, Shatta Wale, Navio na Sarkodie.

ShiiKANE- Tunatamani Kufanya Kazi na Diamond Lakini Ali Kiba Kwanza

Mastaa wa muziki kutoka Nigeria ShiiKANE wamefunguka na kuweka wazi kuwa wanatamani sana kufanya kazi na Diamond lakini mpaka wakishafanya kazi na Ali Kiba Kwanza.

Wasanii hao watatu wanaounda kundi hilo la ShiiKANE wapo nchini Tanzania kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa nchini hapa Lakini pia kwa ajili ya kutangaza muziki wao.

Wasanii hao wamekiri kuwa wanatamani kufanya kazi na wasanii wa Bongo Diamond na Ali Kiba lakini mmoja wa wadada wa kundi hilo Shay amekiri kuwa wanataka kufanya kazi na Ali Kiba kwanza.

Wasanii hao walifunguka hayo Kwenye mahojiano waliofanya na Bongo 5:

Tunatamani kufanya kazi na mtu kama Diamond ila kwanza Alikiba kisha Diamond ila tayari tumesha fanya kazi na Chin Bees ambaye ametufundisha Kiswahili kidogo katika kazi tuliyofanya“.

Lakini pia mbali na Diamond na Ali Kiba ShiiKANE wamesema Msanii wanaye ramani kufanya naye kazi ni Vanessa Mdee kwani wamekiri wanavutiwa na kazi zake sauti  yake na hata urembo wake.

Shikaane Wafungukia Muziki wa Tanzania, Wawataja Vannesa, Alikiba na Diamond.

Wasanii wanaofanya vizuri nchini Nigeria wanaotaka katika familia moja wanaojulikana kama shiikane  wamefunguka mengi kuhusu muziki wa Tanzania na jinsi walivyojipanga kwa ajili ya kuuendeza muziki wao Tanzania na Afrika mMashariki kwa sababu hawajawahi kufika kabisa  pande hizi.

Wadada hao ambao mmoja akuita kuonyesha hisiazake kwa mwanadada Vannesa Mdee alisema kuwa  anatamani sana kuonana na Vannesa na kufanya nae kazi huku akisema”i like she is pretty, beautiful and talented  and very nice voice, i like her a lot, we love  to work with her  and we will . we love to work with diamond, ooh alikiba , we love to work with alikiba actually, and we already work with chin bees.

Wakiongea huku wakionekana wenye furaha wadada hao watatu wanasema kuwa wanatamani sana koabo yao ya kwanza wafanye na alikia sana na wanatamani kufanya nae kazi nyingi alkifatiwa na Diamond.

Shiikane wanasema kuwa kazi yao kubwa iliyowaleta Tanzania ni kwa ajili ya kutangaza kazi zao na kuangalia jinsi ya kufanya kazi na kujenga uhusiani mzuri na wasanii wa Tanzania.