Billnas Afungukia Tuhuma Za Kuwa Mariooo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Billnas amefunguka na kukataa kata kata tuhuma alizorushiwa na Steve Nyerere kuwa ni mariooo.

Hivi karibuni Billnas na Steve Nyerere walijikuta katika vita kali ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Steve kumtuhumu Billnas baadhi ya mambo ikiwemo kuwa Marioo.

Billnas ameibuka na kukana taarifa hizo sio tu kwamba sio Marioo bali pia amemnyooshea kidole Steve na kudai inawezekana yeye ndio marioo maana anaonekana tu.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemwagia povu hili Steve Nyerere:

Mimi siwezi kuwa marioo halafu ukishawahi kusikia msemo “Anayesifia mvua ujue imemnyeshea” basi ndiyo yule ukiona mtu amezidiwa anakimbilia umarioo basi ujue yeye ana fanya huo umarioo.

Kwanza sina hiyo lifestyle ya kimarioo na siwezi kuwa Marioo ndio maana nina vitu kama Tagi Ubavu kwaiyo asiongee kitu ambacho hakijui”.

 

Billnas Amtolea Uvivu Steve Nyerere na Kumtaka Apeleke Komedi Zake Majukwaani

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vyema na ngoma yake mpya ya ‘Labda’ amemtolea uvivu msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka apeleke komedi zake majukwaani.

Bifu kati ya Billnas na Steve Nyerere lilianza juzi baada ya Steve kumtolea maneno Billnas na kumuita Mariooo na maneno mengine ambayo yalipelekea wasanii hao kujibizana Kwenye Instagram.

Lakini sasa Billnas amemtolea maneno Steve na kumtaka aache kumfuatilia na kama nia yake ilikuwa ni kuchekesha watu kumpitia yeye basi amekosea ni bora angefanya komedi zake kwingine kwani alivuka mipaka ya utani.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemtolea povu hili Steve Nyerere:

Komedi zake asilete Kwenye vitu vyangu mimi ile ni kazi yangu yeye kama anataka kufanya komedi si yapo majukwaa ya komedi?.

Halafu isitoshe mimi sio mtu ambaye nina Vibe naye yaani sina ukaribu naye kihivyo mambo hayo angefanya mtu kama Idris ingawa hata yeye kuna mipaka hawezi kuvuka”.

Lakini pia Billnas ametoa onyo kwa watu ambao wamekuwa wakimtania tania kuhusu ishu yake na Nandy tangu itokee:

 Hata kama mtu anakutania isiwe too much maana siku hizi naona watu watu wanapenda kunivaa vaa yaani unashangaa mtu from nowhere anamuandika Billnas”.

 

Nimekoma Kuwa Kiongozi Msibani.;- Steve Nyerere

Msanii maaru­fu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema amekoma kuwa kiongozi misibani kwa sababu ya matusi anayovuna akishika nafasi hiyo.

Steve aliiambia Za Motomoto News wikiendi iliyopita kuwa, amekuwa akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve.

Steve Nyerere Atangaza Kujivua Uongozi Wa Misiba

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere amefunguka na kutangaza kujivua Rasmi nafasi ya kiongozi wa misiba mbali mbali inayowahusu wasanii wa Bongo movie.

Steve amesema ameamua kujitoa katika nafasi hiyo kutokana na fedheha ambayo amekuwa akiipata kutoka kwa watu kutokana na nafasi hiyo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Steve Nyerere amedai kuwa amekua akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.

Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida”.

Steve Nyerere amekuwa akirushiwa tuhuma mbali mbali na watu ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa Kula rambi rambi ambapo juzi juzi ndugu wa Agnes Masogange walilalamika kuwa hawa kupokea rambi rambi tangu ichangishwe na Steve.

Steve Aliyegomba na Mama Wema Leo Wako Pamoja, Mzazi Hakosei.;-Steve Nyerere

Msanii ambae amekuwa kama kiongozi kwa wasanii wengine siku zote panapotokea jambo lolote alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa wasanii na watu wote kwa ujumla wanapaswa kukumbuka kuwa kuna mungu na kumrudia yeye siku zote.

Akiongea baada ya kutulia kwa sakata la kugambania msiba wa mtoto wa Muna  love kati ya baba na mama steve anasema kuwa “inabidi watu wajifunze kutubu, na lakini pia kikubwa mnapaswa kujua kuwa wazazi wanaheshimia siku zote na hawajawahi kukosea”

Steve nyerere vambae aliamua kutolea mfano wa mahusiano yake na mama wema kwa sasa anasema kuwa kuna mambo mengi yaliwahi kutokea kati yake na mama yake wema lakini mwisho wa siku aligundua kuwa yule ni mama na hawezi kukosea na ndio maana hata yeye wapo pamoja na Mama Wema kwa sababu ni mama.

hakuna baba aliyewahi kukosea na hakuna mama aliywahi kukosea , leo mtashanga kuwa steve yule yule aliyegombana na mama wema leo wako pamoja pale wanakula na kunywa kwa sababu ni mama , pamoja na mama wema nae anayo ya kwake lakini ni mama , hakuna mama mbaya duniani.tujifunze kuwaheshimu wazazi.

steve nyerere Amaliza Utata Mazishi ya Patrick,” Muna na Peter Hawana Matatizo.”

Mwanabongo movies Steve Nyerere  ambae kila siku amekuwa kama kiongozi wa wengine katika mambo mengi ametangaza kutokuwa na matatizo yoyote kati ya muna na mzazi mwenzie Peter ambae hapo awali ilikuwa ikileta mkanganyiko kuhusu ni wapi maiti ya mtoto wao Patrick atafikia atakapopokelewa kutoka kenya mauti yalipomkuta akiwa katika matibabu.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari na mbele ya mzazi mwenzie na muna anaejulikana kwa jina la peter steve nyerer amethibitisha kuongea na msanii muna na kuyamaliza matatizo na migogoro iliyokuwepo na kukubaliana kwamba hakuna shida yoyote endapo maiti itafikia nyumbani kwa peter kutokana na ukweli kuwa pale ni kama nyumbani kwa muna pia.

Steve anasema kuwa kumekuwa na maneno mengi katika mitandano yanaychochea mambo hayo kuwa makubwa lakini kiukweli kuna muda mtu anaweza kuwa na hasira na kusababisha kuongea mambo yanayoweza kuwakwaza wengine au kukaririwa vibaya bila yeye mwenyewe kujua (akimaanisha muna) .

Hata hivyo baada ya kutoa tamko hilo, Steve alisema kuwa kuna baba wa ukweli na baba wa mitandaoni lakini kwa upande wake anamtambua Peter aliyekuwa pembeni yake kama baba wa mtoto lakini hayo mengina hayajui na ndio maana hata wamekualiana kuhusu maswala ya mazishi ya mtoto.

 

Steve Nyerere Amwagia Povu Zito Muna

Muigizaji wa Bongo movie na kiongozi wa moja wa wasanii wa filamu nchini Steve Nyerere amewajia Muna na Familia yake juu ya sintofahamu zinazoendelea hivi sasa juu ya msiba wa mtoto wa Muna , Marehemu Patrick.

Steve Nyerere amemvaa mama wa mtoto huyo (Muna) na kumwambia aache kuwayumbisha watu badala yake aungane na mume wake wa ndoa (Petere Zacharia) ili kusitiri mtoto wao kwa heshima kuliko kuwafaidisha watu kwa mameneno na mifarakano yao mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Muna Muna Muna Muna Muna, naomba unisikilize popote ulipo, huu muda si wakufukua makaburi.
Wewe muna kwangu ni mama bora, ulimpenda mwanao ulisimama na mwanao mpaka kipindi cha mwisho. MUNGU akupe nguvu Muna.

Muna embu kaa tena chini jifikilie, ulitumia nguvu akili na maarifa yako yote na WATANZANIA wakatokea kukusapoti kwa namna moja ama nyingine. Kila mtu ameguswa na msiba wa mwanao ndani ya nchi na nje ya nchi, basi nakuomba Muna tumia busara sana weka utoto pembeni, Mweke shetani pembeni shilikiano na MUME wako wa NDOA kumpumzisha mtoto wenu.

“Matatizo yenu wekeni kando kipindi hiki kigumu Muna msiwape watu faida Muna, Naimani umeokoka basi kwenye hili kuwa na HOFU na MUNGU, sizani Muna kama aya tunayo yasoma mara mtoto wa huyu mara wa huyu, mara niliolewa nikiwa na mimba kama yanakujenga.

Bali nazani yanabomoa heshima yako.Dada nakuomba Fumba macho hili lipite nazani ata Patrick uko alipo analia kuona mfarakano huuuu. Msimtese mtoto uko alipo, tumieni busara sana .Baada ya maziko ayo mambo yenu mtaendelea nayo kwa sasa ushauri wangu ungana na family muweze kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili.

Washauri wa Muna nawaomba unganeni na family ya Peter kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili sisi wangine tupo pande zote ila atupendezwi na haya tunayo yaona nilizani ni muda muafaka wote kukusanyika mwananyamala kwa Peter kuhakikisha tunampumzisha kijana wetu asante“.

 

Steven Nyerere Awatolea Uvivu Wasanii Wa Bongo Fleva Waliogoma Kufika Kwenye Msiba Wa Sam Wa Ukweli

Muigizaji wa Bongo movie Lakini pia mwenyekiti wa Bongo movie, Steve Nyerere amewajia juu wasanii wa Bongo fleva nchini kwa kutohudhuria msiba wa msanii mwenzao Sam wa Ukweli.

Wiki iliyopita msanii wa Bongo fleva Sam Wa Ukweli aliaga ghafla dunia kutokana na maradhi mbali mbali ambayo yamekuwa yakimsumbua.

Steve Nyerere amewapa makavu wasanii wa Bongo fleva na kudai hawana ushirikiano kwani wengi wao wameshindwa hata kuhudhuria msiba wa msanii mwenzao.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Steve Nyerere amedai wasanii hao hawana hofu ya Mungu bali wanachojali wao ni kutoporomoka kwa vipaji vyao:

Lazima tuwe na hofu na Mungu maana hakuna staa ambaye hatakufa kila mtu atakufa kama ambavyo kila aliyetangulia ametangulia lakini na sisi tunafuata”.

Bongo fleva wamesemekana kutokuwa na ushirikiano baada ya kuwa na idadi ndogo ya wasanii waliohudhuria msiba huo kulinganisha na jinsi ambavyo Bongo Movie walivyojitoa kwa wasanii wenzao kama Agnes Masogange.

Steve Nyerere Aingilia Kati Ugomvi wa Gabo na Duma

Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, ameingilia kati ugomvi baina ya Duma na Gabo Zigamba huku akimtaka Duma kuachana na masuala hayo kwa kuwa anaetaka kushindana naye yupo juu yake zaidi kwa kila kitu.

Steve ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz
huku akionekana kukerwa na kitendo hicho ambacho kimedumu kwa muda mrefu kwa wawili hao na kupelekea Steve kuwafananisha na wanyama aina ya mbuzi na kuku kutokana na tabia zao. “Hapa katikati kuna mbuzi na kuku, lazima tuheshimiane kutokana na urefu na hata jinsi mbuzi anapochinjwa kilo zake huwa kubwa na kilo za kuku ni ndogo. Kwa hiyo lazima waheshimiane hata kwa kilo, ukuaji. Wasifikilie kwamba ugomvi wanapokuwa wanagombana ulaya basi nasi Afrika tufanye ili tuuze sokoni maana wengine wanasema kugombana ni kiki, na kataa hilo muda mwingine ni kudhalilishana tu“, amesema Steve.

Pamoja na hayo, Steve Nyerere ameendelea kwa kusema “heshima sio lazima uwe umetoka nayo nyumbani kwenu hata unapokuwa heshima unakuwa nayo ili upate kumuheshimu kila mmoja upate connection na maisha ya kesho na kesho kutwa”.

Kigugumizi Cha Steve Nyerere Kuhusu Mtoto Wake

Msanii Steve Nyerere wikiendi iliyopita alipata kigugumizi kuongea moja kwa moja na kuweka wazi juu ya mtoto wake na msanii mwenzake Weru Sengo, picha ambayo ilisambaa sana katika mtandao wa kijamii ikimuonyesha mtoto huyo yupo katika picha ya pamoja na Steve Nyerere.

Hata hivyo baada ya picha hiyo kuweka , siri ilivuja baada ya Wema Sepetu kuongea moja kwa moja kwamba mtoto yule ni wa steve na weru sengo na ndipo waandishi wa habari walipoamua kumpiagi simu steve nyerere mwenyewe na kumuuliza ju ya ujume huo ambapo steve akipatwa na kigugumizi na kushida kabisa kuzungmzia swala hilo.

Alijibu ; mimi sijui chochote  waulize walimwengu wanajua…ama unataka abari naomba uandikke kuwa mimi nitawafutulisha wasanii wote siku ya jumamosi  katika viwanja vya leaders club, kuhusu hizi picha wala sio mimi niliezitupua.”

Kwa muda mrefu wasanii  hawa wamekuwa wakikata na kusema kuwa hawana uhusiano wowote na kwamba hawataki kulizungumzia hilo.

Steve Nyerere Anena Haya Baada Ya Lulu Kuachiwa Huru

Muigizaji wa Bongo movie na Mwanaharakati wa siasa Steve Nyerere amefunguka baada ya Muigizaji mwenzake Elizabeth Michael kuachiwa huru mapema jana.

Siku ya jana Jeshi la Magereza lilitangaza rasmi kupitia barua yao walioiachia Kwenye vyombo vya habari kuwa Elizabeth Michael ameachiwa huru rasmi na kwenda kutumikia kifungo cha nje.

Baada ya Lulu kuachiwa rasmi Steve Nyerere ambaye pia ni kiongozi Kwenye tasnia ya Bongo movie amemualika rasmi Lulu katika harakati za kuijenga upya tasnia hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Nyerere aliandika ujumbe huu:

LULU NI.JAMBO LA.KUSHUKURU SANA KWANI KILA PITO NAAMINI MUNGU YUPO.PAMOJA NAWE,NICHUKUE NAFASI HII KWA DHATI KABISA KUMSHUKURU MH RAIS JOHN POMBE MAGUFURI KWA MSAMAHA HUUU NAAMINI UMEFANYA JAMBO JEMA SANA RAIS WANGU,NIIPONGEZE MAHAKAMA PIA NA WADAU WOTE MLIO KUWA MNAMUOMBEA MWENZETU KUTOKA ,FAMILY, NJOO LULU TEJENGE TASNIA YETU SASA“.

Mara baada ya taarifa kusambaa kuwa Lilu ameachiwa huru wasanii wenzake wengi walionesha kufurahishwa na kitendo hiko.

Unalalamikia Michango, Ulichangia Nini Zaidi ya Kulia:-Steve Nyerere

Msanii wa bongo movies Steve Nyerere amefunguka tena kwa mara nyingine na kusema kuwa kwa watu wenye akili timamu hawezi kukaa aaongelea rambirambi ya marehemu wakati msiba haujafkisha hata arobaini  na wala  sio ndugu wa karibu wa marehemu.

Steve Nyerere anasema kuwa watu wengi wamekuwa na akili mbaya ya kuingia instagram na kulalamiia swala hilo bila kuwa na taarifa rasmi ya kitu hicho.

Steve Nyerere anasema kuwa ela hiyo yenye jumla ya shilingi mil2,1 bado ipo na kwamba kama kamati walipanga kufungua akeunti kwa ajili ya mtoto wa marehemu na wala sio kupewa ndugu za marehemu kama inavyosambaa katika mitandao ya kijamii,

Sidhani kama mtu mwenye akili timamu tena kama wewe ni ndugu  tena ambae hata arobaini ya marehemu haijafika unafikia hatua unaanza kuongelea swala la michango ya kwenye msiba  wakati michango mingine inatakiwa kwenda kwenye arobaini.

Niulize , unatokaje na kwenda kuzngumzia maswal aya rambirambi kwenye vyombo vya habari wewe umechangia nini, zaidi ya kulia, umechangia jeneza?

Lakini pia akiongelea swala hilo, zamaradi mketema alithibitisha kuwa pesa hiyo ipo kwake na kwamba wanafatilia taarifa za mtoto wa marehemu ili waweze kumfungulia akaunti yake.

Yusuph Mlela Amtolea Povu Zito Steve Nyerere Kisa Mzee Majuto

Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amemjibu muigizaji mwenzake na mwanasiasa Steve Nyerere baada ya kumtuhumu yeye na wasanii wenzake kwa kutafuta kiki Kupitia Mzee Majuto.

Steve Nyerere aliwajia juu wasanii wote walipoenda hospitali kumuona Mzee Majuto na kupiga naye picha kisha kuweka Kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutafuta kiki.

Lakini pia Steve aliwatuhumu wasanii hao kwa kuenda kumtembelea hospitalini hapo lakini hawa cha hii chochote Kwenye kitabu chake cha matibabu mwisho wa siku wanaishia kupata tu kiki.

Baada ya Tuhuma hizo, Yusuph Mlela akiwa ni miongoni mwa wasanii walioenda kumuona Mzee Majuto na kisha kupiga naye picha amemtolea povu zito Steve Kupitia kipindi cha Enews ya EATV:

Steve Nyerere ni Steve Nyerere sasa sijui alitaka akamuone mwenyewe ili hili tatizo lionekane lake peke yake sijui wakati hilo suala ni la kwetu sote lakini sijajua yeye mwenyewe alimaanisha nini maana siwezi kukaa nikaanza kulumbana naye maana nina vitu vingi sana vya kufanya lakini mimi nilifanya kwa ajili ya upendo na mzee”.

Mzee Majuto anasafirishwa wiki hii kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Le Mutuz Awapa Makavu Wasanii, Asema Steve Nyerere Ndio Kiongozi Anaewafaa.

Mwanahabari le mutuz ameshindwa kulifumbia macho tukio liliotokea hivi karibuni kuhusu matatizo waanayoyapata wasanii katika umoja wao na kuwaambia kuwa pamoja na yote lakini wasanii inabidi wakubaliane na ukweli kuwa Steve Nyerere nde kiongozi anaewafaa kwa sababu amekuwa kiongozi anaewafaa sana hasa kwa alichokionyesha kipindi hiki cha msiba wa msanii mwenzao Agness Masogange.

Le Mutuz amemsifia sana steve nyerere na kumwambia kuwa haikuwa raisi kwa mtu mmoja kuweza kupata habari za kushtukiza lakini akaweza kujipanga yeye na kuwapanga wenzake na kuweza kumzika Agnesss kwa heshima kubwa kuliko ambavyo mtu yoyote angetegemea, na hata Agness mwenyewe hakufikiria kama angeweza kufanyiwa hivyo.

hongera sana @steve nyerere kwa kusimama kwako kidete kama kiongozi  kwa kusimamamia na kufanikisha shughli nzima ambapo kwa siku ya kwanza msiba kutokea haikuwa raisi kutambua kama haya yangewezekana.umehangaika na kulala macho mpaka kumzika kiheshima .ujumbe wangu kwa wasanii ni kwamba aliye na macho aone na aliye na masikio na asikie kwamba  steve ndie kiongozi wenu anayewafaa,na ndie mnayetakiwa kumtumia kutafuta maendeleo yenu.. now its up to you..nazijua figizu figisu zenu lakini sasa make chini na kumpa uongozi rasmi  kwa sababu sio mara ya kwanza amesimama na kuwapa heshima nyie 

Mrisho Mpoto Amtaka Steve Nyerere Apunguze Gubu Baada Ya Kukosa Tuzo

Msanii maarufu Bongo Mrisho Mpoto amemuoa juu msanii mwenzake wa Bongo movie Steve Nyerere kumtaka apunguze gubu na kukubali matokeo baada ya kukosa tuzo za SZIFF.

Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zilifanyika wikiendi iliyopita na kuleta gumzo baada ya wasanii waliokosa tuzo kama Steve Nyerere kuanza kulalamika.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku chache zilizopita na Bongo 5 Steve Nyerere alilalamika yeye kukosa tuzo Lakini pia alidai pia kuna wasanii ambao angependa wapate tuzo lakini walikuwa kama vile Aunty Ezekiel, JB na wengineo.

Mrisho Mpoto amempa makavu na kumwambia aache kulalamika kwa sababu ameshindwa hilo ni gubu badala yake afanye juhudi ili Safari ijayo aweze kupata tuzo hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mrisho Mpoto ameandika mambo haya:

Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo.

Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…

Zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa”.

 

Steve Nyerere Alia na Waandaaji wa SZIFF

Msanii na kiongozi wa umoja wa bongo movie nchini amefunguka yaliyopo moyoni mwake na kusema kuwa waandaaji wa tuzo za sinema zetu iliyofanyika juzi katika ukumbi wa mlimanai city hawajafanya usawa kwa sababu wapo wasanii wengi ambao walistahili kuwekwa katika kategoria mbalimbali na wangeweza kushinda lakini wao wamebana sana.

Steve nyerere ambae pia hata hakutaka kuonekana katika tuzo hizo usiku ule huku akiwa kama kiongozi wa bongo movies anatoa sababu ya kutokuonekana pale na kusema kuwa wasanii wengi  wameachwa nyuma sana.

Steve anasema kuwa hajwenda kwa sababu kuna wasanii kama kina kitale, asha boko walitakiwa kutafutiwa nafasi zao ili kupata ushindi kwa sababu wanastahili lakini wao waandaaji wamechagulia watu waliokua wanawajua tu.

nitakiongea nilichokiona jana kwenye tuzo,kwani Ray, Jb, roams, aunty ezekile, Shamsa ford, Duma , Weru, Hemedi,Johari, Irene, Tausi , Batuli na hata Mainda wanaofanya vizuri wako wapi?na mbona sijawaona na kuna vijana wengi wazuri ambao ni machipukizi wako wapi

Tangu kumepita kwa tuzo hizi , kumekuwa na maneno mengi sana huku wengine wakisema kwa wasanii wengi waliopata tuzo hizo hawakustaili kuzipata kwa haki.