“Sitaki Mtoto Wangu Aingie Kwenye Sanaa”-Yusuph Mlela

Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amefunguka na kusema kuweka wazi kuwa hajafikiria kuhusu kumpeleka Mtoto Wake wa miaka Sita aanzae kuigiza.

Yusuph Mlela ana Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka sita  aliyezaa na Mpenzi Wake wa zamani Lakini Baada ya kuachana amemuacha na Mtoto na yeye ndio anamlea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti Risasi Mchanganyiko, Mlela ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuingiza Mtoto wake kwenye Sanaa Mpaka pale atakapokuwa mkubwa na kuamua mwenyewe.

Hapana, sitaki mtoto wangu nimuingize kwenye uigizaji, nataka yeye mwenyewe kama atapenda ndiyo baadaye aingie, lakini sitaki nimtengeneze katika mazingira haya, nataka yeye mwenyewe ndiye achague maisha yake. Pia kama atapenda sanaa, nitamruhusu“.

 

Ukizaa na Mwanamke Sio Lazima Umuoe- Yusuph Mlela

Msanii wa Bongo movie Yusuph Mlela amefunguka na kusema kuwa kama mwanaume akizaa na mwanamke haina maana ya kwamba lazima amioe mwanamke yule.

Siku za nyuma Yusuph Mlela alitengeneza headlines Baada ya kusema kuwa hawezi kumuoa mwanamke aliyezaa naye kwa sababu haendani naye na ilikuwa bahati mbaya tu wakapata mtoto.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mlela amesema kuwa hakusema kuwa hawaendani au alimponda mama Watoto Wake bali alisema kuwa sio lazima kumuo mwanamke huyo.

Hapana, sikusema kwamba hatuendani, lakini siyo lazima mkizaa muoane, mnaweza tu mkazaa na mwisho wa siku kila mtu akaendelea na mambo yake na hiyo desturi siyo ya kwangu peke yangu ipo dunia nzima”.

Lakini pia Mlela alikataa kama alizaa na mwanamke huyo kwa makibaliano:

Haikuwa kwa makubaliano, lakini naweza kusema kwamba, ilitokea tu tukawa tumepata mtoto, lakini tabia zikawa tofauti kizuri tulikuwa hatujafunga ndoa wala kujitambulisha popote hivyo ilikuwa ni ruksa kuachana.

Atabaki kuwa mzazi mwenzangu ni mtu ambaye namheshimu kwa sababu amenizalia mtoto”.

 

Vijana Wanaingia Bongo Movie Wapate Majimama;- Yusuph Mlela

Msanii wa bongo movies , yusuph mlela ameongea na mwandishi na kutoa yake ya moyoni huku akisema kuwa wasanii wengi waliopo katika bongo movies sasa hivi wanaingia bongo movies sio kwa sababu wana vipaji lakini ni kutokana na kutafuta watu wa kuwalea.

Yusuph Mlela anasema kuwa ukweli utabaki kuwa tangu Kanumba amfariki basi na bongo movie imeshakufa hakuna anaefanya movies kwa kipaji bali kwa maslahi yao binafsi na vijana wengi wako kwa ajili hiyo.

tangu kanumba amfariki basi na bongo movies imekufa kabisa, vijana wengi wanaingia katika bongo movies kwa sababu ya kutafuta majimama tu ya kuwalea.

Akiwa kama mmoja  ya wasanii wa bongo movies hayo ndio maoni yake nayoona kutokana na soko la movies sasa hivi lilivyo, ingawa wapo wanaobishana na kauli hiyo ya kuwa kanumba amekufa nna bongo movis imekufa.

Yusuph Mlela- Diamond Anatakiwa Awapige Chini Wote Zari, Wema na Mobetto

Muigizaji za wa filamu za kibongo, Yusuph Mlela ameibuka na kumshauri Diamond awapige chini wanawake wote walio Kwenye maisha yake kwa sasa akimaaanisha Zari, Hamisa na Wema.

Mlela amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyefanya na Global Publishers alipoenda Kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Gabo siku ya jana.

 

Mlela alifunguka hayo alipoulizwa  anamshauri nini Diamond kuhusu maisha yake ya kimapenzi yanayoendelea kuchoreka Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Mlela alisema angekuwa yeye Angewapiga chini wasichana wote.

Kiukweli mimi siwezi kumshauri kitu, Diamond ana maisha yake na maamuzi yake pia, kwa hiyo yeye afurahie tu maisha yake its ok, mimi siwezi kumpangia. Ningekuwa mimi nisingekuwa nao wote (Zari, Mobeto wala Wema), siyo kwamba siwapendi, kwanza sitembei na watu maarufu ninatoka na watu wa kawaida tu”.

Diamond amekuwa akitengeneza sana headlines kutokana na Mahusiano na wanawake tofauti tofauti ambapo hivi sasa amekuwa akisemekana Kurudisha majeshi kwa Zari wakati yupo na Mobetto.

Yusuph Mlela Amtolea Povu Zito Steve Nyerere Kisa Mzee Majuto

Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amemjibu muigizaji mwenzake na mwanasiasa Steve Nyerere baada ya kumtuhumu yeye na wasanii wenzake kwa kutafuta kiki Kupitia Mzee Majuto.

Steve Nyerere aliwajia juu wasanii wote walipoenda hospitali kumuona Mzee Majuto na kupiga naye picha kisha kuweka Kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutafuta kiki.

Lakini pia Steve aliwatuhumu wasanii hao kwa kuenda kumtembelea hospitalini hapo lakini hawa cha hii chochote Kwenye kitabu chake cha matibabu mwisho wa siku wanaishia kupata tu kiki.

Baada ya Tuhuma hizo, Yusuph Mlela akiwa ni miongoni mwa wasanii walioenda kumuona Mzee Majuto na kisha kupiga naye picha amemtolea povu zito Steve Kupitia kipindi cha Enews ya EATV:

Steve Nyerere ni Steve Nyerere sasa sijui alitaka akamuone mwenyewe ili hili tatizo lionekane lake peke yake sijui wakati hilo suala ni la kwetu sote lakini sijajua yeye mwenyewe alimaanisha nini maana siwezi kukaa nikaanza kulumbana naye maana nina vitu vingi sana vya kufanya lakini mimi nilifanya kwa ajili ya upendo na mzee”.

Mzee Majuto anasafirishwa wiki hii kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Yusuph Mlela atoboa siri kali kuhusu msanii Nay wa Mitego

Na kwa kweli hii wiki si ya Nay wa Mitego hata kamwe.

Baada ya mama ya mtoto wake kutokea mitandaoni na kueleza Nay hashughuliki na mtoto wake na ila anatafuta kiki naye, muigizaji mkali Yusuph Mlela pia amejitokeza kukashifu Nay wa Mitego.

Akizungumza na global TV alieleza ya kwamba Nay wa Mitego alikuwemo Chokoraa miaka iliyopita na kuna mambo mbalimbali ya aibu iliyotokea wakati humo ambayo utayapata kwenye hii video:

“Nay nataka round 3 tu za boxing kwenye stage”Muigizaji Yusuph Mlela aomba kupigana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego  alitumia ukurasa wake wa Instagram kukosoa baadhi ya  wasanii wa Bongomovie huku akiwataka wafanye kazi bora pia.

Nay alidai kuwa wasanii wa Bongomovies wanapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya kwa lengo la kutaka wafanyabiashara wanaouza filamu za nje ya nchi wafungiwe kwani hawafuati  taratibu ambazo wasanii wa bongomovie wanazifata wakati wa usambazaji wa kazi zao.

Muigizaji Yusuph Mlela alikerwa na maneno aliyosema Ney na kuamua kumjibu kwa hasira –alimtukana na pia kuomba apigane naye ngumi.

Yusuph Mlela na Nay wa Mitego

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano.

“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela alisema.